Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa baada ya mkutano wake na viongozi waWilaya na Halmashauri ya wilaya ya Monduli kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo,Arusha, Novemba 27, 2009. Mkutano wake ulihusu hali ya njaa na ukame wilayani humo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. kwa nini tunatumia, Waziri mkuu au Raisi mstaafu hali kuwa tunajua mara nyingi kwamba waziri kama huyu kajiuzulu na Raisi aliyestaafu Tanzania ni Nyerere tu. wengine wote sio kwamba wamestaafu bali Katiba haiwaruhusu kugombea tena. je kama Raisi akishindwa kwenye uchaguzi baada ya miaka yake mitano ya kwanza tutatumia mstaafu pia? mimi naona neno zuri ni Raisi aliyepita.

    ReplyDelete
  2. Ndugu acha jazba na kujichanganya mwenyewe! Rais wa nchi anapoapishwa kuanzia dakika aliyomaliza kuapishwa ni Rais kulingana na katiba, hata akifa baada ya dakika moja baada ya kuapishwa jina lakuwa Rais halitafutika katika historia ya nchi, kwahiyo Marais waliostaafu au muda wao kuisha kulingana na katiba wataendelea kuwa na sifa ya Rais hata baada ya kufa. Nafikiri hujui hata maana ya kustaafu ni nini tafuta walimu wa kiswahili wakufasirie nini maana ya neno kustahafu. Katiba imewastahafisha huko ni kustahafu Mwalimu Nyerere aling'atuka hakustahafu kwa taarifa yako! Nafikiri ungeandika jina lako kwa msaada wa pembeni inaelekea umekurupukia mada usiyoijua. Pole ndugu.

    ReplyDelete
  3. Kufa kufaana,

    ReplyDelete
  4. ha ha haa eeeehhhheeee former president clinton kwenye cnn kila leo wanatamka namna hii je kiswahili chake ni kipi??

    ReplyDelete
  5. candid scopeNovember 28, 2009

    Kiswahili safi hapa tungesema waziri mkuu wa zamani ingeleta maana nzuri na kulinda heshima yake bila watu kuanza kuchokonoa yaliyosahaulika. Waziri tofauti na Rais. Kwa maana hiyo waziri anapoacha au kuachishwa kazi yake hapo ndio unaanza mwanzo wa kuitwa waziri wa zamani wa wizara fulani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...