ukishuka uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere jijini dar usishangae utapokutana na maninja wenye maski na makoti meupe wataokupa fomu ya kujaza kueleza unajisikiaje mara baada ya kutua. hii ni mojawapo ya tahadhari zinazochukuliwa kudhibiti mafua ya nguruwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Kaka Misupu hawa jamaa wa ukaguzi wa chanjo airport wanakera sana! Japo wanafanya kazi nzuri tena nafahamu kuwa wako kazini lakini hawazingatii wewe ni msafiri, ulikuwa katika ndege zaidi ya masaa 12, umetoka pengine nchi tofauti kuuganisha ndege, umechoka, tena sana.

    Ukifika tu wanakuambia kaa pembeni, tena kwa ukali na dharau ya ajabu. Kisa? Huna kadi ya chanjo ya yellow fever na TB. Mimi nikajaribu kujieleza - kwa kuwa sikuwa na taarifa kuwa inahitajika kuonyeshwa hapo hiyo kadi yangu nimeisahau home, because kiafya unatakiwa hii chanjo upewe kila baada ya miaka 10 if i'm not wrong. Lakini bado tu jamaa akaendelea kunighasi huyo, eti "hujui kuwa unabishana na mimi ni mtumishi wa serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania?"

    Nikastaajabu sana, maana hata mimi ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na tena nina haki yangu ya kikatiba. Sijafanya kosa kusahau kadi ya chanjo, na kwa nini wakati napewa ticket yangu, au napita immigration kuondoka nchini wasiniambie kuwa nikirudi bila ya kuwa na kadi ya chanjo sitoruhusiwa kuingia nchini? The public needs to be informed! Waweke matangazo kama walivyoweka kuhusu sheria ya kusafiri na liquids of 100ml!

    Sio mimi tu, kuna wageni wengine walikuwa wametoka Oman, family ya watu 4 kama sikosei, nao pia wakawa wanaghasiwa, yaani nilisikia huzuni sana. Eti kila mmoja wao alipe $50 kupewa chanjo! Wakaanza malumbano. Then akaja mchanga mwingine hapo kuambiwa hivyo tu, naye akaanza kubongoa kimombo cha Kibosho, "aise usinilethee mimi hapa nikae pembeni kwani nimebeba unga? Aise ngoja nimpigie Masawe..... ikawa kama tuko sokoni vile... kichwa kikaanza kuniuma sana, nusu nizimie kwa makelele.

    Naomba niwaombe waTanzania wenzangu wote wanaosafiri kwenda nje ya nchi ili wasipate adha niliyoinonja mimi, muOman, na kaka yetu toka Kibosho, please please please nendeni mkapate chanjo, na siku mnarudi Tanzania hakikisheni kuwa kadi zenu mnazo mkononi maana ni mateso kusema kweli. Pia kama ulishawahi kuchanjwa miaka kadhaa ilyopita ni vyema kadi yako uipekue ulipoitupa ili uwe nayo wajameni maana usijwe ukatiwa hatiani.

    ReplyDelete
  2. Ah wapi na nani kasema huo ni uzushi mtupu kujaza makaratasi haitoshi kuthibitisha una mafua ya nguruwe wachukue vipimo kama namna gani ala!ila poa tu tutafika!

    ReplyDelete
  3. Samahani hivi ndivyo wenzetu walioendelea wanavyofanya kudhibiti mafua ya nguruwe au tunatania.kumhoji mtu unajisikiaje?sijui

    ReplyDelete
  4. Ni kupotezeana muda tu. Hata hao wenye mafua wanasema wanajisikia vizuri.

    ReplyDelete
  5. sijui, ila kwa zile fomu zinavyouliza, sidhani kama yupo mtu atajaza kuwa anajisikia vibaya, wakati kila mtu ana haraka ya kufika home! kila la kheri kwao

    ReplyDelete
  6. kaka, hizo fomu hazina hata follow up...unaweza ukaandika hata jina la uongo ukawapa wala hawa cross check na passport yako unawatupia unaenda zako immigratio huyo unatoka....tena kuna jamaa mmoja hao wa makoti meupe nilishuka juzi toka dubai akaniuliza faza unakazawadi kidogo....duh nilichoka

    ReplyDelete
  7. hizo fomu ni uzushi tu maana wanakupa ujaze hakuna mfatiliaji ukimaliza kujaza unaiacha mezani huyooo unalala mbele sasa sioni hata umuhimu wa hizo fomu kazi kuletea watu usiku tu sasa faida ya kujaza hizo fomu ni nini? mie nilijaza kiduchu nikaona haina maana nikaiacha mezani nikatambaa zangu

    ReplyDelete
  8. huo ni ulaji tu, hapo hao watu watataka uwape kitu kidogo kama huna hivyo kadi ya chanjo, kila mtu anakula kazini kwake, maisha bora kwa kila mtanzania! Ukisubiri Kikwete akultee hayo maisha bora utakufa njaa!

    ReplyDelete
  9. MTU MMOJA HAPO AMESEMA NI SAWA HATA NCHI ZILIZOENDELEA WANAFANYA HIVYO HUO NI UONGOATAJE NCHI GANI ILIYOENDELEA WANA FANYA HIVYO? NI CHINA TU NDO WANAFANYA HIVYO KWA VILE CHINA SI NCHI YA KIDEMKRASIA NI YA UONEVU TU. UK, USA, JAPAN, CANADA HATA HUKO YALIKO ANZIA HAWAFANYI HIVYO, HAKUNA MTU AIRPORT ANAYEKUSUMBUA JUU YA UGONJWA HUO MASWALI MBUZI KIBAO HUO NI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NA UTENDAJI MBOVU HAPO WANACHOFANYA NI KUTAKA KUTISHA ILI WAKUTOWE RUSHWA WANATAKA KUNUNULIA MAGARI HAPO HAPO NA KUJENGA MAGOROFA, WATANZANIA JAMANI KITU KIDOGO BASI NDO MWANYA WA RUSHWA, SI KOSA MTU KUTOKUWA NA MAKARATASI HANA MPIME AKIWA NA MAFUA MPE DAWA APONE ILI ASIAMBUKIZE WENGINE KWANI KUNA MTU ANATAKA KUUMWA, BASI WATU WAPIMWE NA UKIMWI, ACHENI MAONEZI NA UKIUKWAJI WA KAHI ZA BINADAMU, WAZIRI WA AFYA NA MAMBO YA NDANI NA HATA OFISI YA RAIS TUNAOMBA UFAFANUZI JUU YA UTENDAJI MBOVU WA HAWA JAMAA.

    ReplyDelete
  10. wewe anon wa kwanza uliyezungumzia mambo ya airport. Sijaelewa umuhimu wakusema akaja mchaga ikawa kama mko sokoni. Yaani kuongea lugha yake ndio mko sokoni? Unajua watu wengine wana prejudice lakini hawajijui. Unaweza ukawa unaongea kitu cha maana lakini unaharibu the whole point kwakua off point au kuwa na prejudice. Kama wewe ulivyo raia wa Tanzania na yeye ni member wa kabila mojawapo la Tanzania hivyo ana uhuru wa kuongea lugha yake. Kama tatizo likikua ni kelele sema na sio kumu-identify kabila lake kama joke.Elimu sio shule tu lazima tujifunze kuwa sensitive na culture,race, gender etc za watu.

    ReplyDelete
  11. mim nakubaliana nao wwako pale kudhibiti mafua ya nguruwe kwa "kumwangalia mtu tuu kimwili" kama hiyo ndio system walioiunda basi ni failure. huwezi kumwangalia mtu eti ujue kama ana mafua au hana..huo ni uzushii..pili kwanini mfumo mzima wa tz ni wakuuukaribisha rushwa????kama kweli wana taka kuzui mafua ya ngurue basi waige kama wenzao nchi za asia kutumia sophisticated equipment...maana hata system ya kuchkua visa airport ni mfumo wa rushwa....wakati mwingine unatarajia watu waliosoma wajiweke kiusomi lakini wapiii....ujinga mtupu...na dharau zisizo na kikomo.
    ukinuiliza mimi je nimepata chanjo za TB na mafua ndio nitakuambia...nchi nyingi za magharibu hawana system ya raia atembee na card..kwani umesikia watu wana "gaiwa unga wa kaya"...hilo hawalijui hao maafisa wa afya??? MIMI NITAWAPA CARD YA DR WANGU WAMPIGIE YEYE ATAWAMBIA KWENYE SIMU...KWANI WENZETU KILA KITU KWENYE MITANDAO....ILA WASIJE WAKASHINDWA KUPATA CREDIT ZA KUMTWANGIA

    ReplyDelete
  12. Na kwa HIV tungekuwa makini hivi ingekuwa vizuri sana.

    ReplyDelete
  13. kusema kweli tanzania wako nuyma sana kimaendeleo kutokana na rushwa na tamaaa mbele mie nakereka zaid pale ninapo fika nyumbani ninapoambiwa funguwa begi umetia nini humu au hichi nini wkati sie tumetoka nchi ziloendelea huku one world mzigo hautoki mpaka uscaniwe wahakikishe usalama leo ukifika nyumbani ufunguwe wapekure aibu wanatufedhehesha lkn wazungu hawawafungulishi tabiua hiii itaisha lini jamani ujinga punguzeni nyumbaniii watu mbele kwambele

    ReplyDelete
  14. Anon wa 08:12 pm. Acha jazba! Umeanza na prejudice mwenyewe kwa kuwa na hasira sana, nadhani unahitaki kujoin ka course ka anger management! Na bado unajidai kupreach what you cant practice. Hii ni blog ya jamii, na wachagga ni watani zetu wa jadi. Usijidai kutuletea uzungu usio kuwa nao, ebo! Tambaa huko na wala hujaongea kitu cha maana...

    ReplyDelete
  15. makaratasi huwa yanapotea sasa kulazimisha mtu tena kwa ukali ndo nn?awa wanataka siku ngumi zishuke pale airport wee ngoja,asanteni wadau kutupa hii nilikua cjui..
    ni kweli annon apo juu,ni fedheha SANA SANA tunapopekuliwa mabegi yetu ilhali wadosi na wazungu akhaaa wanatambaa,hainiingii akilini kabisa,,,ngoja tutabanana na uyo sijui meneja wa uwanja!!ushenzy sana huu

    ngoja nisafiri nione wa kunibughudhi na izo makaratasi

    ReplyDelete
  16. Mimi msafiri wa siku nyingi. nchi nyingi sasa hazihitaji hizo kadi za manjano. Kama wewe umetoka nchi tajiri, kuonyesha kadi ya manjano ni ujinga wa hali ya juu. wananchi wao wanapata tiba bora, maji safi na wanategemea kuishi miaka 75 na zaidi. Kama matatizo ya H1N1, Korea ya Kusini, China, Indonesia, Singapore na Japan wana TV zao pembeni, kama mwili ukiwa moto kupita kawaida, unaitwa pembeni na kuchekiwa papo hapo. Kama unaumwa, unawekwa hospitali kama wili moja hivi. Kama huna, unapita zako. Hamna kuangaishwa.

    Ni ujinga wa hali ya juu wakati unawakera wageni na sheria zisizo na kichwa wala miguu na papo hapo unatumia fedha chungumzima kuwavutia waje kutembea Tanzania. Sheria za chanjo zitumiwe tu endapo abiria ametoka katika baadhi za nchi ambazo zimedhurika na magonjwa sio abiria wote wasumbuliwe.

    ReplyDelete
  17. Kama hivyo ndivyo basi ni kweli utaratibu unaotumika uko kinyume na haki za binadamu.Kuna wengine tumeondoka nyumbani siku nyingi kidogo ha ktk nchi ambayo nipo hakuna utaratibu huo wa kuwa na kadi ya chanjo hivyo kunisumbua kwa hilo swala sidhani kama ni sahihi.Inaweza ikawa serikali ilikuwa na maana nzuri ILA imetumia wrong"approach ".

    ReplyDelete
  18. Serikali ishukuru kuwa watu bado wanakuja Tanzania kutembea. Ukiangalia gharama za maisha Bongo, ni kubwa na mtu anafikiria mara mbili kuja kuangalia mbuga za wanyama. Rafiki zangu wengi ulaya wanakwenda Afrika Kusini kwa kuwa ni rahisi kuliko Tanzania na wameridhishwa sana. Kama uko Asia au Ulaya, ni rahisi kwenda nchi jirani kwa likizo na matumizi yote ni sawa sawa na bei ya tiketi ya kwenda Bongo. Ukijumlisha na usumbufu na mahitaji makubwa ya fedha kuja kutembea, watu wengi wanasita kuja Bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...