Hey mzee wa libeneke na naniliiii,
hivi karibuni nataka n'tiee maguu bongoland, sasa mimi nataka niwe mjasilia-hali-na mali,nataka nifungue kiota cha kuuza softwares za computers na zile za simu,yaani nitakuwa nafanya mwenyewe zile kazi za ku-install software, na kwa wale wanaoziitaji basi nitakuwa naziuza.
Ni latest software kama vile za OS(Operating System) ikiwa ni Window 7, XP (sp1,sp2,sp3),na zile za linux(gnome na kde-environment),Mac na zile software za ofisini na kwenye ma-bussiness,,hapa naunganisha na software za aina zote za ku-mix muziki na videoz,ku-design websites, photoshop (CS3 NA CS4),3dMax, AutoCad(from 2000 to 2010),.
Kwa ufupi kila aina ya software mtu anayoitaka ataipata toka kwenye hicho kiota!! Sasa nataka nijue upepo wa bongo kwenye biashara kama hizi upoje??inalipa au bado tupo enzi zile za 47?? Na vipi wale ''mafisadi'' hawawezi kunitia kwenye mkono wa sheria,manake mimi ni Pirate mkubwa sana Online,na hapa ninazo software zaidi ya milioni 1..
Bloo mithupu hebu tupia kapuni jina na adress please!!!
Haya waosha vinywa,msaada kidogo,
hasa kwa wale waliokuwa nyumbani(tz)
Mdau wa Google
...mtu hahitaji kuwa mfanyabiashara kuelewa kwamba ni muhimu kwenda kufanya utafiti kwanza ili kujua hali ya soko na wateja. Lakini nafikiri hakuna kabisa hivyo vitu na utapata soko kweli!
ReplyDeleteKisha mwaka 47 ndio upi? Inaonekana wewe ni katika wale mnaofikiria kuwa sisi hapa nyumbani tumeota kutu vichwani na kwa maana hiyo nakukarisha na mara tu ukifika nenda kwanza ferry Magogoni moja kwa moja kabla hujazifungua hizo programu zako.
KARIBU SANA NDUGU YANGU ILA INABIDI UJIANDAE SANA NA USHINDANI MAANA MIMI NILIANZA MWAKA JANA MWANZONI USHINDANI ULIKUWA SIYO MKUBWA KAMA SASA KULIKUWA NA VIOTA KAMA HIVYO 43 TU HAPA DSM, SIJUI MIKOANI VILIKUWA VINGAPI, KWASASA SINA HESABU KAMILI SIJUI TUPO WANGAPI ILA MPAKA MWANZONI MWA MWAKA HUU KULIKUWA NA OFISI ZA HIVI KAMA 81 HAPA DSM, 29MBEYA, 18ARUSHA, 6PWANI, 9MOROGORO, 31MWANZA NAKADHALIKA .
ReplyDeletepirate mkubwa ni viuri kuwa mkweli, wewe shuka tu bongo opportunity kibao, naona bo limelipa.
ReplyDeletewii ndo kwao hapa nyumbani ukiwa na pesa mafisani watakupa heshima ao karibu.
Enzi za 47! no, hatupo enzi za 47 kwenye ICT. Sema kuna gap kubwa kati ya wanaojua ICT na wasiojua ICT. Ila wale wenye ufahamu wa ICT ni wazuri mno, na nadhani kushinda nchi nyingi zilizoendelea.
ReplyDeleteKuhusu hicho kiota chako, kibiashara utapata tabu kidogo au sana tu. Kwa maana vipo vingi sana, hapa nchini almost now kila kona. Na wateja ni wachache. Na kwa kuongeza tu, jinsi unavyozipata wewe hizo software kila mmoja huku anajua/anaweza kuzipata in the same way you use au na zaidi.
Kihusu kusumbuliwa na mafisadi, hapana, au sio sana, sheria bado hazijakaza huku.
Ni hayo yangu machache.
Ushauri wangu rethink wazo lako, au liimarishe kutokana na mawazo ya watu watakavyokupa. Ila kwa upande wa simu kidogo unaweza kufanya kajibiashara ila sio sanaaa.
KWA MAANA HIYO UNATAKA KUJA NYUMBANI KUTUUZIA SOFTWARE ZA WIZI????KWELI WEWE HAUNA AKILI
ReplyDeleteMdau wa google huoni haya kujisifia wizi? Unajua nilipoanza kusoma hii post nilikuona mtu wa maana sana ila nilipofika hiyo paragraph unayojitapa kwa software piracy ndio nikashangaa. Ni jambo zuri kufikiria kuanzisha biashara kama hiyo nyumbani ila unapaswa kuwa na softwares halali sio hizo za kuiba.
ReplyDeleteKujielezea kwako hapa wazi wazi kuna ashiria kwamba wewe unajiona mjanja kwa vile unajua kutumia torrents na P2P networks kuiba software. Ndugu yangu wizi ni wizi tu anaevunja nyumba mwizi na wewe utakuwa mwizi. Dhana kama hii ya kwamba kuibia microsoft au autodesk sio wizi ndio inayowafanya viongozi wetu wafanye ufisadi serikalini na kujiona wajanja.
Mie nakushauri huo mchezo achana nao, siku hizi kuna open source softwares chungunzima ambazo ziko capable kukaribiana na hiyo zinazouzwa. Kwa mfano hizo OS za linux ulizozitaja au kwenye motion graphic softwares kama Blender badala hiyo 3dmax au maya, au GIMP badala ya photoshop, pia kutumia openoffice.org badala ya microsoft office.
Kwanza uelewe uwezekano wa kushikwa na pirated copy huku ughaibuni mkubwa sana, wewe bila shaka una internet yako nyumbani ambapo IP yako inajuilikana. Hayo ndio yaliyomkuta mzee wa theutamu. Penalty yake ni kubwa sana ukishikwa. Pia mara hiyo misoftware sio bure inakuwa na adwares kibao ambayo hata ukiscan huioni.
Nawasilisha
HI MKUU,
ReplyDeleteMI NAITWA MUDDY NI MTU WA IT NA NIMESOMEA NJE YA NCHI NA NIKO KWENYE FANI HII KWA MUDA SASA TOKEA 2003 NILIPOTUA TZ, ILA MIMI NIMEAJILIWA LKN NIMEPITIA KTK MAKAMPUNI MENGI KIASI HIVYO NAJUA TOKEA ISSUE ZA TENDA MPAKA MTU ANAPATA DEAL LA KUUZA. E MAIL ADDRESS YANGU NI muddynice20@gmail.com HIVYO KAMA UTATAKA MAWASILIANO ZAIDI NA USHAURI ZAIDI NADHANI NI VYEMA TUKIWASILIANA KWA E MAIL YANGU, KWANI LICHA YA KUAJILIWA MIMI PIA NI MFANYABIASHARA (MJASILIAMALI) HAPA BONGO JAPOKUWA SIYO ZA IT KWANI HIZO ZILISHANITOA NOCK OUT KITAMBO TU KUTOKANA NA KUWA KWANGU NA MTAJI KIDOGO NA KUKOSA EXPOSURE. SO KWA UPANDE WANGU NAKUKARIBISHA UJE UPATE CHALLENGE ZA NYUMBANI NA NINAFURAHA SANA KUSIKIA MMBONGO ANATAKA KURUSHA TEAM NYUMBANI KUJA KUPAMBANA, KWANI SIO SIRI NI VYEMA KUPAMBANA ILI KUWAONDOA HAWA WAGENI WANAOCHUKUA UTAJIRI WETU NA KUTUWACHA MASIKINI, HIVYO NASHAURI WATANZANIA WENGINE WENYE UWEZO WA KUMSHAURI HUYU MDAU WAFANYE HIVYO ILI KUONGEZA AJIRA KWA NDUGU ZETU WENGINE WASIO NA AJIRA, MANAKE NAJUA MUUNGWANA AKIFUNGUA KIOTA, ATAHITAJI MLINZI, SECRETARY, WASAIDIZI NA KIKIFANIKIWA ATAHITAJI KUFUNGUA NA MATAWI SEHEMU NYINGINE ZA HAPA BONGO, SO WABONGO WATAKULA AJIRA.
KARIBU SANA MKUU.
Muddy Nice
Utamu wa ngoma uicheze na sio kusikilizia mlio wake.
ReplyDeleteKuwa na moyo wa kijasiria mali na kama hiyo ndo field yako anzisha tu kiota chako na mambo utayaona hapa hapa.
Halafu mnalalamika Wachina wakiwaletea bidhaa feki. Katika hizo zaidi ya mil.ulizonazo zaidi ya laki tisa ni feki. Bora ubaki huko huko kuliko kuja kuwaibia watu pesa yao wanayoipata kwa kusota.
ReplyDeleteAsante kwa kuwa mkweli na kweli sasa itakuweka huru!
ReplyDeleteKweli unatafuta ushauri wa kuendeleza biashara ya wizi wa kazi za wenzako?
Kwa jina la kuheshimu IPR za wenyewe nazifunga nira za Torrent zote,share.com na vitendea kazi fanana vyote na kuvitupa jehanam.
Nakuokoa sasa kijamii, ubadilike kabisa maana hata Europe na US sasa sheria kali na msako wa kufa mtu uko mbioni kuwashughulikia waliokuwa wezi kama wewe.
Karibu nyumbani ukiwa umezaliwa upya kiteknolojia na kimatendo.
Karibu sana mjasiria-hali. Nadhani COSOTA wa wadau mbali mbali wa hati miliki wangependa sana kukupokea, labda tu ungetoa full address yako hapa jamvini pindi ikiwa tayari ili iwe rahisi kwao kukupata.
ReplyDeleteKaribu sana daslama.
sidhani kama waafrika siku hizi tumeanza utamaduni wa kununua original software,
ReplyDeletewengi wetu ni kama anasa
mdau, ughaibuni
Njoo mkubwa usijali hata kama ni pirate wa carribean au wa wapi we njoo tu upige kazi kwani faida ya kazi zako itawasaidia watu wengi tu, ila vizuri kama walivyokushauri wadau wa hapo juu biashara ni sayansi, hivyo kabla hujaamua kuifanya lazima ufikirie na kuhakikisha umejiridhisha na utafiti utakaoufanya, lazima ujue baada ya kutafiti soko vizuri na kufanya ulinganifu vizuri wa gharama za uendeshaji pindi utakapoamua kuifanya biashara yako,ili biashara yako useme inakulipa kwa mazingira yetu ya kitanzania ni lazima iwe na uwezo wa kukupa faida si pungufu ya 30% kwani hii ndio interest tunayolipa kwenye benki zetu tukichukua mikopo!, hivyo jiandae na ujipange mkubwa
ReplyDeleteMimi nipo ughaibuni lakini kunasoftware moja umeitaja hapo, ninaitaka nitakuapataje...Achana na hao wasiojua hizi software zilivyo na bei na wengine (mafisadi) si ajabu wanazo kibao lakini hata hawajui kuzitumia.
ReplyDeleteKama unaweza kumumunya sio mbaya. Unanunua copy moja unafunga kwenye computer 20.
Nikupataje
NINAKUSHAURI NA PIA NINAWAOMBA WANAOSIMAMIA HAKIMILIKI WAZIONE LESENI ZAKO ZINAZOKURUHUSU KUUZA HIZO SOFTWARE VINGINEVYO SISI TUKINUNUA TOKA KWAKO TUTAKUWA TUNASHIRIKI KATIKA WIZI ENDAPO WEWE HAUNA LESENI INAYOKURUHUSU KUUZA MALI ZA WATU BILA IDHINI YAO. WIZI HUU UMESHAMIRI TANZANIA KIASI SASA WATU WANAJITANGAZA BILA UOGA. KPSA HILI ADHABU YAKE NI KIFUNGO.
ReplyDeleteMdau
ReplyDeleteKaribu bongo kusema ukweli asilimia kubwa ya wabongo wanajua mambo ya technolojia sasa hivi kila mtu anajitahidi kua na japo PC nyumbani kwake. Ukitaka kuuza pirated software ujue kuzitumia ikiwa pamoja na kuzi install. Watu mtabakia kumkandia jamaa lakini ukweli ni kwamba legal software wenye uwezo wa kuzinunua ni Serikali makampuni na Wazungu au watuwenye uwezo mkubwa. Kwamfano utakuta mtu amenunua PC yake ya mtumba kwa laki 2 then unamwambia aweke genuine Window na Office kwa laki tatu hata kwa dawa hata kubali. Hizi kazi za kuweka software zipo sana especially ukiweza kuwa guarantee customer kua zitakaa muda murefu bila kuwa detected na wenye hizo software. kwa mfano ishu ya antivirus ni kubwa sana na inalipa ile mbaya bongo, kwasababu ma technician wengi huwa wana weka hizi ambazo ni free copy ambazo ailimia kubwa ya virus haviwi detected utakuta mtu kila siku analalamika. Ukiwa na hizo utauza sana.Na jinsi ya ku clean virus. Ma technician wengi wa bongo wanajua ku format Pc kila kitu wanakuambia inabidi u format. Sababu hawana wanalolijua zaidi ya hilo. Kitu kingine Ninge penda kukupa worning hizo kazi za kudeal na user zinasumbua na zina consume time sana. Kwa hiyo Ujiandae maana kwa ulivyo jieleza utakua unadeal na individual customers only hamna kampuni itakayokubali issue za pirate.
Mdau Katika IT
Mimi ni Graphic Designer, kwa hiyo naijua vizuri mienendo ya maendeleo ya ICT hapa nyumbani. Sikushauri kuja kwa ajili ya biashara hiyo peke yake manake kama sisi ma-designer ambao softwares zetu ni one of the most expensive softwares mfano package ya Adobe CS inauzwa more than USD 500 lakini kwa hapa kwetu nikikutajia bei unaweza ukalia mi nimenunua ghali sana basi ni TShs 50,000 hata kampuni kubwa hazinunui original copies hiyo ni East Africa yote. Na kwa sababu hii ni fani yangu siwezi nikawahi kupata software latest nimuuzie designer mwenzangu ntampa buureee kwa nini? ili na yeye akipata anipe bure pia. Hivyo ndivyo watu wengi kwenye field hii ya mambo ya ICT tunavyoishi Bongo mpaka ma-architecture japokuwa wanapata hela ndefu for one job lakini they play the same game. Enewei usiogope njoo ufanye research mwenyewe, Bongo ni land of opportnities ndio maana wageni hawaishi kuja kila siku! Hapa ma-opportunities ni mengi kuliko Ulaya na Amerika wewe tu kukuna kichwa chako vizuri
ReplyDeletendugu yangu kweli unaishi kwenye karne ya ishirini..WEWE UNATAKA KUFANYA BIASHARA NENDA KAFANYE RESEARCH..KWANINI MMETOLEWA NJE NA WAZEE WENU MKAFUTE MATONGOTONGO HALAFU BADO TU MNAISHI KWENYE MAZINGIRA YA KIZA?!!! WEWE KAMA MFANYA BAISHARA WA KWELI FANYA RESEARCH NA ACHA KUULIZA WATU..HUJUI KAMA UNA WASHINDANI, AU HAO WASHINDANI WATAKUPA POSITIVE REPSPONDS??MIMI NAISHI UGHAIBUNI LAKINI NACHOKUFAHAMISHA KUWA WABONGO WAMEAMKA KWA NGUVU KALI..WEWE UMESHAONA MTU ANATENGENEZA SIMU KWA KUTUMIA NAZI?????SASA KAZI KWAKO.
ReplyDeletehuyo jamaa anayeuliza atanipaje, hembu tumia hii id, mgazimazi@yahoo.com,na kwa ufahamu tu hizi software,hasa zile za microsoft,zina-update kama kawa from genuine,ukibisha nakupa gurantee ya miezi 6.
ReplyDeletekwenye ishu nzima ya virus and malware,nafikiria,licha ya kutumia strong virus like kaspersky au bitdefender,kwa watakaohitaji basi naweza kuwawekea virus free OS kama hii ya Mac(kumbuka hii OS inaoperate kwenye machine yoyote hata ile isiyokuwa ya Apple) au hii za Linux Ultimate(like ubuntu ultimate v.2.4), ni free of commands na inaoperate like xp,ni more juicer kuliko hata hii ya new window 7..nawakilisha..(mgazimazi@yahoo.com)
ReplyDeleteHere in Tanzania.we need people like you to develop our county not to steal from us.Ipende inchi yangu iendeleze usije kuinyonya kwa kuleta bidhaa feki zisizo na mpango.
ReplyDeleteHuyu Jamaaa atakuwa na skills Ndogo sana ya Computer.Software zote hizo free online.kwanini ununue software wakati zote hizo unaweza pata bure just ni kugoogle online.It sounds anafikiri wabongo hawajui tumia INTERNET..Yeye mwenyewe ni wa mwaka 47....Kutokana na uwezo mdogo wa kuwaza....
ReplyDeleteUnajua Ms anatoa bure software kwa Nchi za dunia ya tatu.Mtu yeyote aende tu center za Microsoft(Ms) utapata kila aina ya software
ReplyDeletemdau izo soft mazee tunazio bongo kinoma tena genuine win 7, kaspersky anti-virus 2010, quickbook 2008. pastel,office 2007,tasbook,photoshop,micromedia dreamwever,firework,flash,swish,photostudio, cooledit, visualDJ,BPM Studio,adome in design,adobe premier,vista,xp, yan kibaooooooo ni wewe mwenyewe tu ukizita tena mimi nakupa hii ishuuu nimo kilimnajaro na wala si ugaibuni IT haina enzi za 47 hata kinachotoka saa hiii mimi kesho asubuhi ninacho tena genuine...
ReplyDeleteMdau Moshi.
Klimnajaro.Tanzania
Jipange sawa sawa! This is bongoland for you...we need brains and not fakes......
ReplyDeleteAisee mbona wewe mzushi namna hii? Windows 7 tangu lini ina service pack 1, 2 na 3... ama kweli wewe ni mwizi. KAribu DSM tukuingize mjini.
ReplyDeletenijuavyo software zinapatikana online nyingi ni TRIAL VERSION,siku 30 au 15 then zina-expire,sasa hapo zinapatikana bure kwenye net??how could we then support software developers team? tusidanganyane banaaaa!!mwache dogo akafanye dili bongo..ebooo
ReplyDeleteMdau ameomba kujua mazingira ya biashara hiyo yalivyo. Hajasema anazileta kwa sababu ninyi bongo hamnazo.
ReplyDeletePili kuwa enzi za mwaka 47 ni nadharia, maendeleo uliyonayo sasa yanakuwa ya mwaka 47 ukishayapita. Na unaweza kujua hivyo tu baada ya kupita ulipo. miaka si mingi tulikuwa tunajitamba Tv zipo mpaka kariakoo.
Tatu, karibu nchi zote duniani zina wataalam ktk fani mbalimbali. Tatizo ni avarage wananchi wangapi wanajua mambo(elimu/knowledge). Hiyo ndio inayofanya uitwe naive.
Wewe Anonymous wa Tarehe Wed Nov 04, 07:31:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous inaonyesha unaskills Ndogo pia omba msaada kuna ambao wanaojua tumia "Crake" badala ya Trial inakuwa unatumia milele omba msaasa utaelkezwa nini maaana ya Crake.any software mahackers wanacrake....Ombaa msaada utaelimishwa....Kwanini ununue wakati kila kitu ni bure nitacrake anysoftware for you from trial
ReplyDeleteKWA KWELI BONGO WEZI NI WENGI!! NO MATTER HATA WABUNGE WETU WANONA NI UJANJA KUCHUKUA POSHO MBILI MBILI NA KULUMBANA NA TAKUKURU. TUTAFIKA TU.
ReplyDeleteK.O.R.
...crake! What type of an animal is this? My goodness me!
ReplyDeletehahahha 'crake'...ni mjusi!ha ha haaaaaa
ReplyDeleteney-bham.