
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh.Dr.Ibrahim Msengi akipokea msaada wa vifaa vya afya kutoka kwa mkurugenzi wa Vodacom Foundation Bi Mwamvita Makamba.Vifaa mbalimbali vya afya vyenye thamani ya Milioni 20 vilitolewa kwa hospitali ya Bombo Mkoani Tanga.Sherehe hizo za makabidhiano zilifanyika mwanzoni mwa wiki hospitalini hapo.

Mkuu wa wilaya ya Tanga mjini Mh Dr.Ibrahim Msengi akikabidhi msaada wa vifaa vya afya kwa mganga mkuu wa hospitali ya Bombo Dr.Adam Mtatifikolo.Msaada huo ulitoloewa hospitalini hapo na kitengo cha misaada cha kampuni ya simu ya Vodacom.Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Bi Mwamvita Makamba.

Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya Bombo mkoani Tanga wakifurahia msaada wa vifaa vya afya vilivyotolewa na Vodacom foundatuion hospitalini hapo.Wanaoshuhudia ni mkurugenzi wa Vodacom Foundation Bi Mwamvita Makamba (kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh.Dr.Ibrahim Msengi (katikati). Sherehe hizo za makabidhiano zilifanyika mwanzoni mwa wiki hospitalini hapo.
Mwamvita Makamba!
ReplyDeleteTanga Tanga Kunaniiii? inamaana unawamba ngoma na kuvutia kwenu? Msambaa wewee!
haya Hongereni sana Vodacom muwakumbuke na Tumbi. ama upishe atokee mkurugenzi mwingine anatokea maeneo hayo nasi tufaidiiiii
Tunaomba picha za msiba wa Mzee wetu Kusaga mbn hamna
ReplyDeletemdau Sauz
mcheza kwao hutwanzwa yaghe hongea
ReplyDeleteHuu ni ukabila, kila kitu huyu mwanamke anapeleka kwao. Kama si hivyo basi ni siasa za kijinga. Ukoo wa Makamba unakera sasa.
ReplyDeleteacheni hizo mwamvita anamwaga misaada minono karibu kona zote za tz na si tanga tu nilijua tu mtasema kweli midomo hailipiwi VAT
ReplyDeleteVoda lipeni kwanza kodi mnayopaswa kisha ndio mtoe misaada.
ReplyDeleteMichuzi siamini kama kweli unaminya au unachelewesha kupost comments kama hizi?
Sasa huyu mkuu wa wilaya anafanya nini hapo? Serikali sio iliyotoa msaada huo, ni Vodacom. For members of an under-performing government such as this to try to win publicity using such occasions and gifts from the private sector is really disappointing.
ReplyDeleteTunashukuru TZ tunajitahidi misaada muhimu lakini pia tungefuatilia utumiajiau utelekezaji wa hiyo misaada.Na kitu kingine hospitali zetu ziko nyuma sana na usafi kwa kweli unaenda hospitali hali inasikitisha wewe mgonjwa unaumwa hiki na unaenda kuambukizwa kingine.Tunahitaji misaada ya vifaa vya kufanyia usafi ni muhimu sana
ReplyDeleteHaya waosha vinywa!
ReplyDeleteIs VODA SOCIAL RESPONSIBILITIES paying them off??? Nahitaji hard data......
Mwamvita hizo nywele na hiyo miwani imekufanya uonekane mkubwa, kama maza fii vile.
ReplyDelete