PICHA ZA WASHIRIKI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI KATIKA KONGAMANO LA KUMBUKUMBU YA MIAKA 10 YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE KATIKA CHUO KIKUU CHA UNIVERSITY CHA EDINBURGH, SCOTLAND, WAKIWA KATIKA PICHA ZA PAMOJA BAADA TU YA KUFUNGUA CHAPISHO LA MWALIMU NYERERE (PICHANI JUU) CHAPISHO HILO LILIFUNGULIWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MH. BERNAND MEMBE.
wadau wa scotland wakiwa na Mama Sitti Mwinyi kwenye hafla hiyo
Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Mh. Bernad Membe na Balozi Mwanadai Maajar wakipozi na wadau wanaoshiriki kongamano hilo la Mwalimu

wadau wana furaha kukutana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mama Sitti

Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mama Sitti na wadau














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. BARIDI HAIJAWA KALI HIVYO MZEE!

    ReplyDelete
  2. Kwanini wasifanyie BONGO?

    ReplyDelete
  3. picha imetoka bomba ila kuna mheshimiwa mmoja hapo kwenye picha ya mwisho naona alikuwa anashangaaaa sana. au ndio mara ua kwanza kutua mamtoni...tititi

    ReplyDelete
  4. Kwanza pongezi kwa kuadhimisha kumbukumbu ya maisha ya Mwl. Nyerere.

    Pili itakuwa vizuri kama tulivyosikia ktk taarifa ya kumbukumbu ya maisha ya Nyerere iliyofanyika Edinburgh kuwa kuna filamu iliyotengenezwa na Ole Oki kuhusu maisha ya Mwalimu.

    Filamu hiyo ikiwekwa ktk www.youtube.com basi itakuwa jambo jema kwa wa-Tanzania na wa-Afrika hata walimwengu kupata kufuatilia aliyifanya Mwalimu ktk uhai wake.

    Maana sasa hivi, hakuna kumbukumbu ktk filamu inayoendana na umaarufu wa Mwalimu duniani.

    Mdau
    Baku, Azerbaijani.

    ReplyDelete
  5. hivi London sijui Scoatland kumeshakuwa baridi kiasi hicho? naona wametiliza makoti ya winter na winter navyojua bado kiduchu...

    ReplyDelete
  6. Eti hajawahi kufika mamtoni?
    jamani wabongo sijui ni lini tutakuwa wakubwa wa Akili,
    Mamtoni kituagani,
    Life bomba home asikuambie mtu.
    MTONI KUFULIA
    2 . Kuhusiana na kiwango cha baridi,kama leo hii umetoka Dar na ukaenda London Kesho am telling you itasikia baridi ya kufa mtu,so acheni ufinyu wa mawazo ndugu zangu,endeleenikubeba Bixinyo kama kawa

    ReplyDelete
  7. Kunda mbishiii!! haukukubali mpaka ukatokeza mbele kuliko wengine tukuone!! Nzuri hiyo kaka.

    Edwin

    ReplyDelete
  8. wee unaesema, London sijui Scotland! kwa hiyo unajua london iko scotland!? ashame on you! unavyosikia kwamba winter haijaanza, lakin hujui unasikia tu! kwa taarifa yako Scotland is very cold, hata summer watu wanavaa makoti. Acheni ku judge vitu visivyo kuwa na msingi, badala ya kupongeza mnaponda, wabongo bwana! mtabakiaga hivo hivo nyuma kila siku.

    ReplyDelete
  9. We Anon wa Tue Nov 10, 06:20:00 PM

    Unaijua Scotland?. Kwa taarifa yako wiki hii huku tunacheza +7 to -3, Sasa kwa mtu aliyetokea bongo +7 tu ni baridi kali sana kwake. Unataka kujifanya wewe umezaliwa nchi zenye baridi. Mwache mzee ajikinge, unajua madaktari walivyo mshauri?, Wazee kibao huku sometimes wanazidiwa barabarani kwa baridi na ndiyo wamezaliwa na kuzeekea huku.

    ReplyDelete
  10. wadau mtu kama hauishi sehemu ya baridi na umeenda kutembea mara moja mwili wako utakuwa hujazoea na lazima utavaa makoti mazito kuliko wenyeji. Sio lazima iwe nje, hata ukienda Arusha; wanaotokea Dar utakuta wamajitwika masweta kuliko wenyeji. Mwili lazima u-acclimatize (kuzoea hali ya hewa)

    Hata kwa wale wanaoishi nje utakuta wakati wa demani (fall/autumn) mwili unahisi baridi zaidi kuliko wakati wa "spring" ingawaa kiwango cha jotoridi ni kilekile.

    Isitoshe, mzee Ruksa umri umeenda sasa (84). Lazima atahisi baridi kuliko vijana; pia inabidi alinde afya kwa kuvaa makoti.

    Ye alikuwa rais wa Zanzibar mwaka kwa mmoja na wa Tanzania kwa miaka 10, unafikiri hakupata nafasi ya kutembea nje jamani?

    ReplyDelete
  11. annoy 11:44 am acha kuwa na mawazo finyu..labda hujajuwa nini watu wanachozungumza hapa.
    pili kubeba bixinyo sio tatizo..ndio maana nchi zikaendela kwa kujali kila kazi..kwakufahamisha tu ujue ulimwengu mwanamee hachanui kazi, watu ulaya huacha kazi za ofisini kwa kuingia fani ya mabomba ya maji machafu...unasemaje kwa hilo???...au uzushi??? kwa hiyo usidharau kazi za watu....au ndio nyinyi wale...mnaoshndwa hata kujisugua wakati wakuoga mnatafuta wafanyakazi wa ndani afanye kazi hiyoo??? mwanamme hachagui kazi ndio maana wenzetu wanaendela...tuendele kusubiri vilivyotafunwa..mwishowe tutameza makombooo.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...