Mh_Balozi Mhandisi John Kijazi akifurahia kombe la ushindi ambalo timu ya Ubalozi wa Tanzania India ulishinda kabla hajalikabidhi kwa timu captain. Katika kusherehekea Uhuru wa Tanzania Jumuiya ya wanafunzi wanaosoma India na Ubalozi wa Tanzania nchini humo uliandaa bonanza la michezo nyumbani kwa balozi ambalo lilifana sana.
mbio za 'vipofu' zikikaribia kuanza
mashindano ya kula maandazi yanayoning'inia
shindano la kuvuta kamba kati ya timu ya
wanafunzi na wafanyakazi wa ubalozi. ngoma ilikuwa droo
kukimbia na ndimu
balozi akitoa mawili matatu kwa timu ya ubalozi kabla ya gemu

Mh Balozi Mhandisi John Kijazi akiwa Mwenyekiti wa Tasa Bi. Jennifer Sumi (kulia) na Makamu wa Rais Jane Balama wakishuhudia mchezo wa soka.
Timu kabambe ya wanafunzi kabla ya gemu
umoja na upendo kati ya wanafunzi na wafanyakazi wa ubalozi









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hongereni sana kwa kufanikisha shughuli hii naomba mwakani mh balozi kwenye mashindano haya tushirikishwe na miji mingine ya hapa india kama vile hyderabad hili litatusaidia kujua na kujenga ushirikiano mzuri baina ya wanafunzi na kuimarisha jumuiya zetu kwa kubadilisha mawazo
    pia naomba nniulize kwa wanatechnohama hivi hiyo kamera ilikuwa na makosa ya tarehe maana naona kama tukio lilifanyika 26/03/2009 na sio uhuru day yaani tarehe 9/12/2009 naomba kueleweshwa

    ReplyDelete
  2. Naona utakuwa umekosea, Michuzi. Mwezi wa 3 huwa ni uhuru wa Zimbabwe. Wa Tanganyika huwa ni mwezi wa 12!

    ReplyDelete
  3. Hongereni sana kwa kuazimisha uhuru day ni utamaduni unaopaswa kuendelezwa,nimefurahishwa sana na ushirikiano unaoonekana hapo na pia wanajamii walivyowakilisha kwa pamba za kisport zenye heshima mbele ya balozi.kuhusu state nyingine kushirikishwa,,jamani hao wamefanya kwa niaba yetu tuwapongeze aidha gharama za kuwashirikishwa wt ubalozi wautaweza kuzibeba,

    ReplyDelete
  4. michuzi acha usanii mwezi wa 3 sio uhuru wa TZ umechomekea picha za zamani za sherehe nyingine sio uhuru

    ReplyDelete
  5. Hapo wadau sio kosa la michuzi kuhusu tarehe. Ni kosa la mwenye kamera hakuseti tarehe ipasavyo. Otherwise nawapongeza sana ndugu zangu kwa kuadhimisha uhuru day kwa bonanza la michezo kati ya Wanaubalozi na Wanafunzi. Dada Fadhila uko juu, hongera sana Mhe. Balozi na wengine wote hapo.

    ReplyDelete
  6. mweee tarhe ya uhuru iyo jamani???

    ReplyDelete
  7. 42 naona unauza sura wa ukweli wangu

    ReplyDelete
  8. Annon wa Sun Dec 13, 04:57:00 PM,
    uhuru wa Zimbabwe ni tarehe 18 mwezi April na sio mwezi wa 3

    ReplyDelete
  9. hongereni sana nadhani miji mingine muige mfano hawa wanaonyesha umoja wa nguvu ndio maana sura zao zimejaa furaha tele
    hongereni ubalozi pamoja na viongozi wa wanafunzi wa delhi

    ReplyDelete
  10. mimi kwnza nawapongeza ubalozi na waandaaji wa shughuli kama hii.uongozi wa wanafunzi pia na wanafunzi wote.badala ya kukosoa kosoa wacha tufirie ni jinsi gani wakati ujao tunaweza tukawa na bonanza la india nzima.kama TASA ya delhi iwasiliane na TASA za sehemu nyingine ili kuwezesha swala kama hilo.kwa ujumla hongereni TASA-DELHI na ubalozi na msisikilize watu wasio na akili kwani watawarudisha nyuma.One love

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...