Ankal kama nilivyokuahidi hali ya barabara ya Tarakea to Marangu hivi sasa si shwari. Yaani tumelazimika kusimama masaa sita baada ya barabara kuzuiliwa na Dar Express kama unavyoona ikiwa imejikita kwenye udongo, na kidogo tu iwamwage abiria zaidi ya hamsini waliokuwemo. Kama hiyo haitoshi likaja basi dogo la fuso hapo na kuziba barabara kwa kukwama na kusababisha usumbufu wa zaidi ya magari mia.
Picha na stori na Mdau Isaya Philip
Hapa ni Rombo Mkuu kilometa tatu tu kutokea Rombo kuelekea Marangu ambapo mdau Isaya Philip alilazimika kuacha vekesheni na kushirikiana na wadau kuwatoa wajenga nchi
zege halilali hapa....
Anko naninihii jionee hapo wakati nyie mnahangaikia barabara za gorofa na kusota kwenye foleni huko kwenu wenzenu wanahangaikia huku mitaa ya Tarakea barabara ya changalawe tu ili waondokane na adha hii ya kufanya kazi ngumu ya kusukuma magari kabla ya kazi zao za msingi
kimbembe Tarakea





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Haya sasa wakati umefika kwa wale wenzetu wachaga mnaojidai kuwa nyie ndio mmnauleta maendeleo tanzania mkumbuke na barabara zenu sasa sio kushindana ni mtoto wa nani an ghorofa ngapi

    ReplyDelete
  2. Poleni sana walipakodi kwakazi ngumu mnazozipata ilatutafanya nini nawatu wanataka kuspend lots of money kujenga majumba yakifahali yenye maswimin pools,A/C,CCT camera nk nawengine tumewaamini tukawakabizi madalaka sasa wanatudidimiza kwakusign mikataba yaulaghai kwamanufaa yao nafamilia zao,itabidi tuwasubiri sana mpaka watakapotosheka labda watatuangalia na sisi walipakodi,ilatuspowashtua sidhani kama watashtuka siunajua tena mtu anayeishi kama yupo peponi!!!?

    ReplyDelete
  3. I love Rombomy home area. It looks ever green. I love it.

    Mrosso akiwa Rukwa

    ReplyDelete
  4. Vile vijisent vya 'kukarabati' nyumba ya nanihii si vingefanya kazi kubwa tu katika maeneo muhimu kama haya? Lakini nani anajali....

    ReplyDelete
  5. Mdau mkereketwa wa maendeleo...December 29, 2009

    Wadau naomba kuuliza...hivi bilioni 1.4 zilizoweka swimming pool kwa gavana zisingeweza kusaidia kurekebisha hiki kipande cha meta 200??? Watu wakasafiri kwa amani...

    ReplyDelete
  6. Du! Jana nimetoka Mashati ila nashkuru nilipofika mkuu zile Caterpillar za ujezi wa barabara zilikuwa eneo hilo kusawazisha mambo ila zege halilali wadau wako FITI kuhakikisha Rombo inaingilika na kutokeka....
    PAPAA STAN
    MOSHI. KILIMANJARO

    ReplyDelete
  7. wabongo bwana hao hawashuki hahahha likiwaka moto hilo hahaha shukeni msaidie wenzenu

    ReplyDelete
  8. hi barabara wakati mramba ni waziri wa miundombinu alitaka kuleta ubinafsi wake akaidhinisha pesa zote vijenge barabara hii,wabunge wakashtuka,sasa mdau unacholia nini hapo,barabara zote za moshi kuonganishwa na mikoa mingine na wilaya ziko tambarare,hizo ni za kuingia vijijini kabisa,wakati kuna mikoa kama manyara hawana hata barabara za kuuonganisha mkoa wao na mikoa mingine,wachaga bwana,

    ReplyDelete
  9. Huu ndio umuhimu wakupiga kura. Umempa mbunge miaka mitano hajafanya kazi ondoa chagua mpiga kazi regardless ya chama chake. Kuweka changarawe barabarani sio pesa nyingi. Watu wanaangalia tu barabara za mijini wanasahau vijijini/mikoani. Kama hamna vitu muhimu kama barabara tunategemea vijana waendelee kukaa maeneo kama haya. Ndio maana wanakimbilia mijini. Nasisitiza hili linalojionyesha hapa ni ufinyu wa mawazo, viongozi kukosa mwelekeo na uhamasishaji.(motivation). Wananchi wanaweza kufanya kitu chamaana sana kama wakihamasishwa. Hela za walipa kodi zinakwenda wapi jamani??? Tunahitaji leadership, pesa za walipa kodi zitumike vizuri, nguvu kazi yakujitolea ipo kama inavyoonekana kwenye picha.Shame on us!

    ReplyDelete
  10. Tues 29 Dec, 05:47:00 PM

    Hiyo ni barabara inayounganisha nchi na sio ya kijiji! Ni internations Highway!

    ReplyDelete
  11. nyinyi hapo juu msianze upuuzi wenu sio kila kijiji kina lami na sio kama watu hawawezi tukijipinda weweeee lami hadi mlangoni kwa taarifa yenu serikali ya tz haikubali mtu binafsi kujiwekea lami yule mzungu wa slip way angeshaweka kile kipande cha barabara yake lami zamaniiii lakini kapigwa stop so msilete vimbelembele front humu ndani katizeni machame kwetu kwa wapalestina utalia full lamiiiiiiiiiii hadi canada nilipo
    manka wa canada

    ReplyDelete
  12. kila siku tunasikia katika vyombo vya habari kuwa utengenezaji wa barabara ni mojawapo ya mafanikio makubwa ya serikali ya ccm (awamu ya 3 na 4) - ningeshauri tuwe wa kweli tuwe tunasema mafanikio ya serikali hizi ni matengenezo ya barabara za dar na sio barabara za tanzania!
    ukishangaa wanakushangaa kwa nini unashangaa!

    ReplyDelete
  13. hizo picha ni za zamani siku hizi bongo barabara ni safi kushinda hata huko marekani na ulaya

    ReplyDelete
  14. jamani kaka michuzi acha kutoa hizi picha za ajabu kwenye blog wabeba box wataogopa kurudi tanzania wakati huku maisha ni safi kuliko huko ughaibuni

    ReplyDelete
  15. lssa michuzi mwenyewe ndio mgomvi ana penda watu wa gombane umu ndani,
    yeye mwenyewe kimya!uafikiri katiwa barafu kwenye nye.. zake

    ukabila na majungu umundani atutatki kawachonga nishe wakenya na c wa bongo

    ReplyDelete
  16. manka wa canada,serikali haikatazi watu kujiwekea lami,kuna watu wamejiwekea lami kutoka main road hadi kwenye nyumba zao,hivyo kama famlia yenu ina uwezo wa kujenga lami kijijini kwenu jengeni tu,ombeni kibali serikalini mtapewa,huo ni kama msaada wowote kwa jamii,ila lami lazima ifikie kiwango fulani,kwahio unaweza kukataliwa kama hutaonyesha funds na kiwango kinachotakiwa,wasalimie huko canada

    ReplyDelete
  17. poa mdau hapo juu ntawapa hi ila nachojua yule mzungu alinyimwa aliambiwa serikali ina uwezo wa kuweka lami ati hawataki watu wajiwekee ni kuidhalilisha sirikali
    manka wa canada

    ReplyDelete
  18. manka ningekutajia watu waliojiwekea lami kuondoa vumbi lakini si vizuri kutaja majina ya watu sehemu kama hizi,ila wapo na inaruhusiwa,changishaneni wachagga muweke lami kama mna uwezo, sio lazima serikali ifanye kila kitu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...