Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais (Mazingira) Mhe.Batilda Burian akiingia kwenye Ukumbi wa Mkutano wa Bella Centre mjini Copenhagen kuhudhuria Mkutano wa Tabia Nchi unaoendelea Nchini Denmark Copenhagen, Kulia ni Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Ruth Molel na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira ndugu Richard Muyungi . PICHA NA ANNA ITENDA -MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Viongozi wengi namna hii wanaenda kufanya nini kwenye huu mkutano?

    Hivi kuna haja ya kupeleka ujumbe wa watu wengi kwenye mkutano huu?

    Tumieni pesa za walipa kodi vizuri ninye viongozi wa serikali ya Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Per diem zinacost sana walipa kodi Tanzania.

    ReplyDelete
  3. jamani watz kwa kusindikizana hamjambo, yaani ni ujinga mtupu!

    ReplyDelete
  4. JAMANI SENGINE WAPO WACHACHE LAKINI PICHA INAONEKANA WAPO WENGI...CHAMSINGI WAZINGATIA LEONGO WALILOPELEKEWA PALE SIO KURUDI MIKONO NA KCHWA KITUPU...SIJUI HATA KAMA WANACHANGIA HOJA WAKIWEPO KWENYE MIKOTANO YA KIMATAIFA.

    ReplyDelete
  5. Nawaunga mkono anonymous wote hapo juu......hii nchi kwa kweli tunasikitisha sana, YAAANI NI UJINGA MTUPU HASAA, LAKINI HAWA WATAKUJA KUTUFAHAMU VIZURI muda si mrefu....wanatuchezea sana hawa !!!

    ReplyDelete
  6. WAWAKILISHI WA TANZANIA WAMECHANGIA

    Msafara wa wawakilishi wa Tanzania si mkubwa kupita misafara wa nchi zingene kwa wale ambao mpo mbali na hapa Denmark.

    Nikiwa mtanzania ninayeishi hapa,ningependa kuwafahamisha wawakilishi wetu kuwepo hapa haswa wakati huu wa mkutano mkuu wa COP15
    ni muhimu saana kwa mtazamo wa mbali kwa Tanzania na bara zima la Africa.
    Wawakilishi wetu wamepiga hatua kubwa saana kwa sauti ya umoja kulipigania Tanzania na bara zima la Afrika,kwa mtazamo wa karibu kunaweza kuwepo na maswali mengi yasiyo na majibu,lakini kwa mtazamo wa mbali Tanzania na bara zima la Africa tutafanikiwa mengi.

    Safari hii kwa mara ya kwanza wawakilishi wetu Tanzania hawakuja kwa kukubali mipangilio isiyo na uhakika wa kudumu kwa Tanzania na bara zima la Africa,wamesimama imara na kushilikiana kwa sauti moja.

    Mickey Jones-Denmark

    ReplyDelete
  7. Afrika tulikubaliana cha kusema na kufanya.

    Umoja wa Madola ulikubaliana cha kusema na kufanya mjini Port of Spain, (T&T).

    Kuna maana gani ya kupeleka ujumbe mkubwa huko Kopenihageni?

    ReplyDelete
  8. wee Mickey Jones ukumbuke sio wewe tu mtz anaeishi hapa DK tupo wengi watz hapa tunaoishi DK,EBU WAFAFANULIE VIZURI WADAU NI KIPI ULICHOTAKA KUWAELEWESHA INAWEZEKANA UKAWA NA JAMBO LA MAANA ILA MAELEZO YAKO YAKO DUNI SANA.MDAU NORREPORT STATION COPENHAGEN DK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...