Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo wa Serikali ya Mapunduzi Zanzibar, Mh. Juma Shamhuna akizungumza kwenye hafla ya Easy Finance kutoa Shilingi Milioni 12.5 kusaidia ZFA kufanikisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Shoto ni Naibu Waziri wa Habari na Michezo ZNZ, Mh. Mohamed Thabit Kombo. Hafla hii imefanyika visiwani wikiendi hii.
Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo wa SMZ, Mh. Juma Shamhuna akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Easy Finance Bw. Isaack Kasanga baada ya Taasisi hiyo ya mikopo, kuichangia ZFA Shilingi Milioni 12.5 kufanikisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Mtendaji Mkuu wa Easy Finance Bw. Isaack Kasanga akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo wa SMZ Mh. Juma Shamhuna mara baada ya Easy Finance kuichangia ZFA Shilingi Milioni 12.5 kufanikisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Naibu Waziri wa Habari na Michezo wa Zanzibar Mh. Mohamed Thabit Kombo, akizungumzia ufadhili wa Easy Finance kwa ZFA mara baada ya Taasisi hiyo ya mikopo, kuichangia ZFA Shilingi Milioni 12.5 kufanikisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Taasisi ya Mikopo ya Easy Finance, imetoa mchango wa Shilingi Milioni 12.5 kukisaidia Chama cha Soka cha Zanzibar, ZFA, kufanikisha mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kurindima huko Zanzibar hivi karibuni.
Hafla fupi ya makabidhiano, imefanyika jana mjini Zanzibar ambapo Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo wa SMZ, Juma Shamhuna alipokea hundi hiyo kwa niaba ya ZFA, na kuipongeza Easy Finance kufafadhili Kombe la Mapinduzi, pia alitoa wito kwa wafadhili wengi zaidi kuzidi kujitokeza kufadhili michezo visiwani humo.

Akikabidhi hundi hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Easy Finance, Isaack Kasanga, amesema Easy Finance, imetoa mchango huo kwa ZFA, ili kuonyesha inathamini juhudi za ZFA, kuboresha mchezo wa soka Visiwani Zanzibar.

Bwana Kasanga amesema pia mchango huo ni namna ya kurudisha fadhila kwa jamii wa Wazanzibari kwa jinsi wanavyoiunga mkono taasisi ya Easy Finance ambayo inalo tawi wisiwani Zanzibar.

Hii ni mara ya pili kwa Easy Finance kufadhili michezo Zanzibar ambapo mara ya kwanza, ilitoa ufadhili wa shilling milioni 5 katikati ya mwaka huu.

Easy Finance, ni taasisi ya mikopo inayotoa mikopo ndani ya muda mfupi na masharti rahisi, ina makao makuu mjini Dar es Salaam na matawi Zanzibar , Mwanza na Mbeya litafunguliwa hivi karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. ...his name is Mahmoud (rather than Mohamed) Thabit Kombo, unless he has changed it in the last few days.

    ReplyDelete
  2. Kama pesa hizi zingekuwa zinasaidia elimu ingekuwa kitu kizuri sana.Shule nyingi hazina madawati wakati tunasika makampuni yanatoa mamilioni kwenye soka.

    ReplyDelete
  3. ZENJI RAHA SANA,UKIWA NA 5000 POUND UNAKUTANA NA MAWAZIRI NA MAKAMERA,HEBU JULY NIENDE NA MIMI NIKASAIDIE JAPO SHULE SIO.

    ReplyDelete
  4. Jamani safari moja huzaa nyengine, hapa jamaa wanaanzia tu na si km hawajui kwamba zanzibar tuna uhaba wa vitendea kazi kwa idara ya elimu, nawapongenza kwa mchango wenu ili kukuza mashindano yetu ili kuyaenzi Mapinduzi.....
    Junior Hyderabad.

    ReplyDelete
  5. Jamani huu ukumbi gani yaani huyu waziri was nini sijui amelowana na jasho utafikiri hapo ni Gym. A/C ipo wapi?

    ReplyDelete
  6. Jamani why mtu anaenda kukutana na Waziri, tena ktk shughuli za kikazi, halafu anavaa T-shirt? Na huyu naibu waziri vp? au walikuwa ktk sports day ya Easy finance? maana nisije nikawa nashangaa kumbe ni sports day

    ReplyDelete
  7. Huyo ni Mahmoud Thabit Kombo tuliyesoma nae Arusha School au? lazima nirudi bongo [Tambararez].

    ReplyDelete
  8. Jamani kule kwetu visiwani, kiongozi huwa karibu na wananchi so we respect them as normal person si unaona hta naibu waziri hana suti? Hakuna kujikweza kule sote ni maskini ww vp? Kuhusu kurowa jasho naibu waziri hamjui km hakuna umeme kule kwa siku kadhaa.
    Junior Hyderabad.

    ReplyDelete
  9. Huyu bwana anatoa mchango, angevaa hata kaptula ni sawa tu, anayepokea mchango ndio lazima aje amevaa suti, kuheshimu shughuli..... ni jeuri ya pesa

    ReplyDelete
  10. Mbona nilisikia Zanzibar wamegundua mafuta na wameanza kuyachimba imekuaje tena?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...