

SOTE (kama) FAMILIA (kwa) PAMOJA KUAFIKIA AZIMIO ndio kirefu cha SOFAPAKA, klabu ya soka iliyoanzishwa kutoka na timu ndogo ya kanisa la M.A.O.S Ministries jijini Nairobi chini ya usimamizi wa Pastor Jimmy Carter Ambajo mwaka 2002.
Klabu hii, ambayo pia ina timu ya wanawake SOFAPAKA QUEENS, imekuwa ikishiriki katika michuano ya kanisa hadi mwaka 2004 wakati mfadhili mkuu ambaye sasa ndiye Rais wao Elly Mboni Kalekwa, mfanyabiashara tajiri mzaliwa wa Congo Kinshasa.
SOFAPAKA, maarufu kama Watoto wa Mungu, iliundwa na timu ya vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu, kabla ya kuanza kununua wachezaji nyota kutoka vilabu vingine vikubwa.
Mwaka huu wamenyakua ubingwa wa Kenya na kuwa timu ya mfano sio kwa Kenya tu bali Afrika Mashariki kwa ujumla, hususan Tanzania kwani ni klabu changa lakini imefanya makubwa na kuna kila dalili itafika mbali.
Pamoja na kuukosa ubingwa wa Tusker 2009, Globu ya Jamii inaipongeza SOFAPAKA kwa kuwa timu ya mfano. Ukiangalia tovuti yao tu utajua hilo, jambo ambalo achilia mbali wakongwe Simba na Yanga, yaani hata TFF hawana tovuti na habari zao zinapatikana kwa mbinde kama enzi za ujima. Hadi sasa ni African Lyon FC, Azam FC na Mtibwa Sukari FC pekee zenye tovuti (japo na wao ku-update kila siku ni mgogoro kiasi). Yaani aibu tupu!
Watembelee SOFAPAKA
HAKUNA NIZAMU SI KILABU YA KUIGWA KAMA IMEMPIGA MPIGA PICHA WETU NCHINI. SI YAKUIGWA FULLSTOP. JAMES.
ReplyDeleteWAKENYA HOIIIIIIIIIIIII MPIRA WA KILABU HAWATUWEZI SIMBA NA YANGA WAMEWAPIGA ILA NAWAPA HONGERA WATANI WETU YANGA KWA KUCHUKUWA UBINGWA WA KOMBE LA MBUZI.
ReplyDeleteAhsante kwa info, mie nilidhani ni timu ya kampuni ya kutengeneza sofa itumiayo nembo ya paka anayependa kushinda ktk sofa.
ReplyDeleteHongereni SOFAPAKA kwa kuonyesha njia jinsi ya kuendesha klabu ya mpira kwa mafanikio.
Ni mategemeo yangu klabu zenye wafadhili tajiri na mpya Tanzania kama AficanLyon(tizama webusaiti) na Azam (tizama webusaiti)zinazoongozwa na vijana watafanya mapinduzi ya kuendeleza vilabu vyao viwe vikubwa kamaklabu za Ahly na National za Misri.
Mdau
Mbagala DSM
sasa wewe unazungumzia simba, yanga na tff kukosa tovuti, hivi zile za ikulu, bot, serikali, mashirika, nk nazo unaziita tovuti?
ReplyDeleteJamani huyo Rais wa SOFAPAKA...
ReplyDeletesi tutakwisha sote kwa magonjwa jamani...
http://www.yangatz.blogspot.com/
ReplyDeletekaka michuzi umetaja Azam na Mtibwa pekee kuwa ndio timu zenye website lakini African Lyon nao wanyo hii hapa. http://www.africanlyonfc.com/
ReplyDeleteAsante
Maendeleo ni hatua muhimu....hapa bado ni yanga..simba..manji...friends of simba...Maendeleo ya soka ya kweli ni ndoto...Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Mozambique zote zilikuwa nyuma ya Tanzania kimpira miaka ya '70.
ReplyDeleteHONGERA SOFAPAKA NAWATAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAENDELEO YA SOKA LA KWELI....
Soka inatushinda Tanzania...hata kiwango cha maamuzi pia ni tatizo? kuna Nchi hazina timu nzuri lakini angalau wana waamuzi, vyama, wawekezaji, washabiki.. na wadau wa soka kwa ujumla wenye upeo wa kutosha kuelewa soka inaelekea wapi kwa sasa.
HAWA WANATUMIA MIGONGO YA DINI KULAGHAI
ReplyDelete1.HAWANA NIDHAMU [wametaka kumpiga refa baada ya kufungwa]
2. Wanaamini uchawi [wamegoma kuingia kwa rooms half time
3. Wachafu na adabu mbaya [wamekojoa uwanjani mbele ya fans woote]
4. Hawakubali kushindwa [wameanzisha fujo baada ya kuchinjwa]
5. Wanashangiliaje goal vile wakati ndio kwanza 1st half as if ndio penalty ya mwisho alafu wanachukua kombe IoI
Wataisoma DAR YOUNG AFRICANS sasa