Wachezaji wa Kilimanjaro stars baada
ya kuibanjua eritrea 4-0 leo na kuingia
nusu fainali za chalenji kwa kishindo
Picha na habari na
mdau Mathew Mndeme
KILIMANJARO Stars imefuzu kucheza nusu fainali kwa kishindo baada ya kuiadhiri Eritrea kwa mabao 4-0 huku Mrisho Ngassa akiibuka shujaa kwa kupachika mabao matatu peke yake (hat-trick).
Mabao hayo yanamfanya Ngasa kufikisha idadi ya mabao matano katika mechi nne alizocheza na usukani wa ufungaji wa mabao akimpiku Mzambia James Chamanga aliyefunga mabao manne katika michuano ya Kombe la Chalenji ambayo inaingia nusu fainali leo kwa mchezo wa kwanza baina ya Zanzibar Heroes na The Cranes ya Uganda.
Kilimanjaro Stars iliyouanza mchezo huo kwa kasi na kupoteza nafasi nyingi za kufunga walilazimika kusubiri hadi kipindi cha pili pale kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, John Bocco alipotumia vizuri urefu wake kwa kuruka juu na kuunganisha krosi ya beki Shadrack Nsajigwa dakika ya 61.
Winga Ngassa alifungulia karamu yake ya mabao kwa kufunga bao lake la kwanza akitokea upande wa kulia na kupiga krosi iliyokwenda moja kwa moja wavuni.
Nyota huyo wa Tanzania aliyekuwa mwiba mkali kwa ngome ya Eritrea kwa kufanya atakavyo akiwazidi mbio na chenga alifunga bao lake la pili na la tatu kwa Stars dakika 76 kwa shuti akimalizia kazi nzuri ya Bocco.
Ngassa alifunga bao lake la tatu dakika ya 84 baada ya Stars kugongea pasi nyingi kabla ya Mwaipopo kupitisha pasi ya juu iliyomkuta mfungaji huyo aliyempiga chenga kipa Yosief Zeratsion wa Eritrea na kumalizia mpira wavuni.
Hii ni mechi 32 ya kimataifa kwa Ngassa akiwa amefungaa mabao 10, huku Bocco akiwa amefunga bao lake la pili kwa Tanzania katika mechi 8 alizocheza.
Kwa ushindi huo, Kili Stars itachuana na Rwanda iliyoitoa Zimbabwe kwa mabao 4-1.
Nao Zanzibar Heroes wenye morali ya hali ya juu chini ya nahodha Abdi Kassim leo watapambana na The Cranes katika mechi ya nusu fainali ya kwanza kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
gemu ambalo amepiga bao tatu peke yake
na maafisa ubalozi nchini kenya baada ya kuwapiga
eritrea 4-0 na kusonga nusu fainali kwa kishindo
Balozi wetu nchini Kenya Mh. Nyasugara P. Kadege na afisa ubalozi wetu nchini humo Bw. Innocent Shio wakifurahia ushindi na makamu wa kwanza wa rais wa TFF Mh. Athumani Nyamlani
Kweli timu za Bara na ndugu zetu wa Z'bar Heroes wametutia moyo kwa sana. Nawakubali na mtatimiza ndoto yetu ya karibu miaka 20 ya kulisaka kombe hilo.
ReplyDeleteMichuzi inamaana huo uwanja hamna dressing rooms za wachezaji?au watu wamekojolea masinki kama taifa?
ReplyDeletemdau jibaba lenye fedha
kwa kweli nawapongezeni sana kwa sababu sisi tunaokaa huku visiwani sijui kama tungeweza kulala kama msingeshinda maana baada ya hawa wazanzibari kushinda ikawa taabu. utadhani wameshalichukua kombe tayari. nawapongeza sana vijana kwa usindi huo. Mungu ibariki Tanzania
ReplyDeletehongera sana kilimanjaro stars, lakini hawa wa ubalozi mbona sikuwaona kwa upande wa zanzibar, wawe kote bwana nje ni moja. nawategemea leo wawe mstari wa mbele zanzibar heroes pia .
ReplyDeleteInakuwaje CAF wanaitambua SIMBA kama club Bingwa ya Tanzania, wakati Yanga ndio mabingwa?
ReplyDeleteembu cheki hii CAF fixture for 2010
http://www.cafonline.com/userfiles/file/clpdf.pdf
http://www.cafonline.com/userfiles/file/ccpdf.pdf
Bwana Inocent Shio nakuona hapo. tunaku-miss sana hapa Sanaa Shekilango tunapopata moja baridi moja moto baada ya kazi. Nairobi vipi mkuu
ReplyDeleteHuyo Mama ktk picha ndiyo Mheshimiwa Balozi wetu wa Tanzania nchini Kenya H.E. Nyasugara P. Kadege.
ReplyDeleteNi jambo la faraja Kilimanjaro Stars kusonga mbele ktk mashindano haya.
Nazitakia timu zetu za Tanzania, Kilimanjaro Stars (Tanganyika) na Zanzibar Heroes zituletee kombe nyumbani Tanzania.
Hongera vijana wa Kilimanjaro Stars na kocha wao Maximo kwa kuonyesha moyo wa kutaka kufanya vizuri kadri siku ziendavyo ktk CECAFA 2009
ReplyDeleteMahojiano na Maximo na pia Mrisho Ngassa kuhusu mechi hiyo
:http://www.youtube.com/watch?v=zSFvU2ReYWw
Magoli yalivyotinga uwanjani:http://www.youtube.com/watch?v=9Ila_r3CEwg&NR=1
Naona Mrisho Ngassa anahojiwa kwa kiingereza yeye anaongea kisukuma kwenye hiyo link ya youtube.
ReplyDeletemdau Wed Dec 09, 01:51:00 PM kama ndie balozi wa tanzania kenya ok..
ReplyDeletemaana ndio nilitaka kuuliza apa nani sasa ndo balozi wetu???sasa mama mbona unaonekana uu mnyonge ivo???changamka mama japo tuone uso wa furaha za kimchezo
kilimanjaro starzz nawaombea kwa Mwenyezi Mungu tufike fainali kabisa ktk jina la Yesu..tutafika
swali wadau:
kilimanjaro starz = taifa starz?
zanzibar heroes je?