Wachezaji wa Kilimanjaro stars baada
ya kuibanjua eritrea 4-0 leo na kuingia
nusu fainali za chalenji kwa kishindo
Picha na habari na
mdau Mathew Mndeme
KILIMANJARO Stars imefuzu kucheza nusu fainali kwa kishindo baada ya kuiadhiri Eritrea kwa mabao 4-0 huku Mrisho Ngassa akiibuka shujaa kwa kupachika mabao matatu peke yake (hat-trick).

Mabao hayo yanamfanya Ngasa kufikisha idadi ya mabao matano katika mechi nne alizocheza na usukani wa ufungaji wa mabao akimpiku Mzambia James Chamanga aliyefunga mabao manne katika michuano ya Kombe la Chalenji ambayo inaingia nusu fainali leo kwa mchezo wa kwanza baina ya Zanzibar Heroes na The Cranes ya Uganda.

Kilimanjaro Stars iliyouanza mchezo huo kwa kasi na kupoteza nafasi nyingi za kufunga walilazimika kusubiri hadi kipindi cha pili pale kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, John Bocco alipotumia vizuri urefu wake kwa kuruka juu na kuunganisha krosi ya beki Shadrack Nsajigwa dakika ya 61.

Winga Ngassa alifungulia karamu yake ya mabao kwa kufunga bao lake la kwanza akitokea upande wa kulia na kupiga krosi iliyokwenda moja kwa moja wavuni.

Nyota huyo wa Tanzania aliyekuwa mwiba mkali kwa ngome ya Eritrea kwa kufanya atakavyo akiwazidi mbio na chenga alifunga bao lake la pili na la tatu kwa Stars dakika 76 kwa shuti akimalizia kazi nzuri ya Bocco.

Ngassa alifunga bao lake la tatu dakika ya 84 baada ya Stars kugongea pasi nyingi kabla ya Mwaipopo kupitisha pasi ya juu iliyomkuta mfungaji huyo aliyempiga chenga kipa Yosief Zeratsion wa Eritrea na kumalizia mpira wavuni.

Hii ni mechi 32 ya kimataifa kwa Ngassa akiwa amefungaa mabao 10, huku Bocco akiwa amefunga bao lake la pili kwa Tanzania katika mechi 8 alizocheza.
Kwa ushindi huo, Kili Stars itachuana na Rwanda iliyoitoa Zimbabwe kwa mabao 4-1.
Nao Zanzibar Heroes wenye morali ya hali ya juu chini ya nahodha Abdi Kassim leo watapambana na The Cranes katika mechi ya nusu fainali ya kwanza kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.


Mrisho ngassa na wanahabari baada ya
gemu ambalo amepiga bao tatu peke yake
kocha marcio maximo wa kilimanjaro stars akipongezwa
na maafisa ubalozi nchini kenya baada ya kuwapiga
eritrea 4-0 na kusonga nusu fainali kwa kishindo

Balozi wetu nchini Kenya Mh. Nyasugara P. Kadege na afisa ubalozi wetu nchini humo Bw. Innocent Shio wakifurahia ushindi na makamu wa kwanza wa rais wa TFF Mh. Athumani Nyamlani

Balozi wetu nchini kenya Mh. Nyasugara P. Kadege na maofisa wa ubalozi ambao wako bega kwa bega na Kilimanjaro stars wakiwapongeza wachezaji kwa ushindi mnono wa bao 4-0 dhidi ya eritrea



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kweli timu za Bara na ndugu zetu wa Z'bar Heroes wametutia moyo kwa sana. Nawakubali na mtatimiza ndoto yetu ya karibu miaka 20 ya kulisaka kombe hilo.

    ReplyDelete
  2. Michuzi inamaana huo uwanja hamna dressing rooms za wachezaji?au watu wamekojolea masinki kama taifa?
    mdau jibaba lenye fedha

    ReplyDelete
  3. kwa kweli nawapongezeni sana kwa sababu sisi tunaokaa huku visiwani sijui kama tungeweza kulala kama msingeshinda maana baada ya hawa wazanzibari kushinda ikawa taabu. utadhani wameshalichukua kombe tayari. nawapongeza sana vijana kwa usindi huo. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  4. hongera sana kilimanjaro stars, lakini hawa wa ubalozi mbona sikuwaona kwa upande wa zanzibar, wawe kote bwana nje ni moja. nawategemea leo wawe mstari wa mbele zanzibar heroes pia .

    ReplyDelete
  5. Inakuwaje CAF wanaitambua SIMBA kama club Bingwa ya Tanzania, wakati Yanga ndio mabingwa?
    embu cheki hii CAF fixture for 2010
    http://www.cafonline.com/userfiles/file/clpdf.pdf

    http://www.cafonline.com/userfiles/file/ccpdf.pdf

    ReplyDelete
  6. Bwana Inocent Shio nakuona hapo. tunaku-miss sana hapa Sanaa Shekilango tunapopata moja baridi moja moto baada ya kazi. Nairobi vipi mkuu

    ReplyDelete
  7. Huyo Mama ktk picha ndiyo Mheshimiwa Balozi wetu wa Tanzania nchini Kenya H.E. Nyasugara P. Kadege.

    Ni jambo la faraja Kilimanjaro Stars kusonga mbele ktk mashindano haya.

    Nazitakia timu zetu za Tanzania, Kilimanjaro Stars (Tanganyika) na Zanzibar Heroes zituletee kombe nyumbani Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Hongera vijana wa Kilimanjaro Stars na kocha wao Maximo kwa kuonyesha moyo wa kutaka kufanya vizuri kadri siku ziendavyo ktk CECAFA 2009

    Mahojiano na Maximo na pia Mrisho Ngassa kuhusu mechi hiyo
    :http://www.youtube.com/watch?v=zSFvU2ReYWw

    Magoli yalivyotinga uwanjani:http://www.youtube.com/watch?v=9Ila_r3CEwg&NR=1

    ReplyDelete
  9. Naona Mrisho Ngassa anahojiwa kwa kiingereza yeye anaongea kisukuma kwenye hiyo link ya youtube.

    ReplyDelete
  10. mdau Wed Dec 09, 01:51:00 PM kama ndie balozi wa tanzania kenya ok..

    maana ndio nilitaka kuuliza apa nani sasa ndo balozi wetu???sasa mama mbona unaonekana uu mnyonge ivo???changamka mama japo tuone uso wa furaha za kimchezo

    kilimanjaro starzz nawaombea kwa Mwenyezi Mungu tufike fainali kabisa ktk jina la Yesu..tutafika

    swali wadau:
    kilimanjaro starz = taifa starz?
    zanzibar heroes je?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...