
Mkuu wa wilaya ya Ilala Evance Balama na Mbunge wa viti maalum kwa upande wa walemavu Margreth Mkanga wakiwa wameshilia kitabu cha "The Forgotten" HIV and disability in Tanzania ambacho kimefanyiwa tafiti na TACAIDS kuhusiana na jinsi walemavu walivyosahaulika kwenye masuala ya ugonjwa wa UKIMWI wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar

Kamishna wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI (TACAIDS) Fatma Mrisho akiangalia batiki zilizotengenezwa na wanawake wajasiliamali wenye ulemavu wa aina zote wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar

Mkuu wa wilaya ya Ilala Evance Balama akimuangalia Abdala Nyangala ambaye ni mlemavu wa macho kutoka Mbagala Kibondemaji jinsi anavyochomeka uzi wa sherehani kwenye cherehani yake ambayo anaitumia kushona nguo za aina mbalimbali za jinsia ya kike na kiume. Mkuu wa wilaya huyo alikuwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar

Wasanii wa kikundi cha The Seven Blind Beats kilichopo mkoani Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar

Wasanii wa kikundi cha sanaa cha walemavu wa aina zote cha Upendo kilichopo mkoani Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...