Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana akifafanua jambo kuhusu matumizi ya Tovuti ya Wananchi katika kujibu hoja za wananchi wakati wa mafunzo ya tovuti kwenye kikao kazi cha makatibu wakuu wa wizara leo jijini Dar Meneja Mradi wa Tovuti ya Wananchi Bw.Finehasi Lema akitoa ufafanuzi wa namna ya kupokea na kujibu hoja za wananchi zinazowasilishwa serikalini kupitia Tovuti ya Wananchi wakati wa mafunzo ya tovuti kwenye kikao kazi cha makatibu wakuu wa wizara leo jijini Dar
Baadhi ya makatibu wakuu wa wizara mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo juu ya Tovuti ya Wananchi katika kujibu hoja mbalimbali za wananchi zinazowasilishwa serikalini wakati wa mafunzo ya tovuti kwenye kikao kazi cha makatibu wakuu wa wizara leo jijini Dar



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. kumbe ni kamradi kamtu

    ReplyDelete
  2. mzee michuzi hawa watu wanapoteza hela zetu bure tu,inasikitisha sana nimewaandikia wizara ya miundo mbinu tangu mwezi wa nane mwaka huu mpaka leo sijajibiwa,naona hawana cha kufanya ushaidi upo kwenye website yao kama hawataufuta naweza ni kucopy na kupaste,kwa kweli inasikitisha mno hata email address zao hazifanyika kweli

    ReplyDelete
  3. tovuti gani hizo za wananchi? naomba nielimishwe jamani mdau mwenzenu

    ReplyDelete
  4. Advocate JashaDecember 15, 2009

    Kweli nakubariana na wachangiaji waliotangulia huu ni ufujaji wa fedha nikihesanbu hizi semina chini ya jina kupigana misasa kuhusu tovuti ktk kipindi cha miezi 4 ni ya 3 kwanza Morogoro,Arusha na sasa Dar.Wakati ukiziangalia hizo tovuti za serikali na mashirika mengi , serikali hata ya Ikulu balozi,mikoa karibu zote ni tovuti ambazo hazifanyiwi uptodate hivi kuna anefahamu tovuti ya maelezo au ya TBC iliyjitokeza kwa siku moja na kutoweka vyombo vinavyopashwa kua mfano.Vinginevyo hizo semina zinasomeka kama JIA YA UFUJAJI WA PESA ZA WALALAHOI Anko MICHUZI WASAHIDIE MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  5. Viongozi wengi wa Serikali wana phobia ya kompyuta, hawapo ofisini kutwa wako safari. Lema hii tovuti iwe iinteractive kama jamii forums tuone nani hajibu na aliyejibu kajibu nini!
    Or else shutdown the website. Haina kazi!!! Tumepeleka maoni mwaka sasa hamna hata jibu tumetoa hata namba zzetu za simu.
    Huu ni uzembe!

    ReplyDelete
  6. ive wanalielewa somo lakini?

    ReplyDelete
  7. Per diem tu hapa, si unaona walivyonona!

    ReplyDelete
  8. Jamani hao makatibu wakuu kwanza watapata mda wapi wa kujibu hoja za watu tena toka kwenye internet??
    Mi ningeshauri, kwasababu kila wizara ina kitengo cha habari, Information officer wangehusika zaidi na hao ndio wangepata majibu toka kwa katibu mkuu, iwe moja ya majikumu yao!! makatibu wakuu kutwa vikao, safari pia si wazuri sana katika matumizi ya computer, email zenyewe kama wanazo hawazitumii.....MI NILISHATUMA MASWALI YANGU KUPITIA TOVITI HIYO TOKA MWEZI WA SABA HADI LEO SIJAJIBIWA!!!! Naungana na mchangiaje hapo juu kuwa tovuti iwe interactive!

    ReplyDelete
  9. Maswali yangu yanapigwa dana dana mara Ikulu mara Utumishi mara fedha na sasa imechukua mwaka mmoja hivi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. kwanza hamuoni wanavotisha kama masimba vile...watajibu saa ngapi mambo ya akili ya wanainchi???

    yani mnanikera nyie viongozi hamjui tu

    izi kodi zetu zinatoa machozi siku

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...