Basi la Kampuni ya Mohamed Trans lenye namba za usajili T810 BCB likiwa limeharibika vibaya baada ya kugogana na gari dogo aina ya Toyota Coaster katika Kijiji cha Kandoto wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro, juzi na kusababiha vifo vya watu 19 papo hapo na wengine 40 kujeruhiwa. Picha na Grace Macha wa Same.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. UNAJUA MTU ANAWEZA KUPATA AJALI HATA UKIPANDA BUS GANI ILA MOHAMED TRANS IMEZIDI.KATIKA KIPINDI CHA MIEZI MINNE INAWEZEKANA YAMEPATA AJALI ZAIDI YA MARA TANO.SASA WIZARA YA USAFIRISHAJI NA USALAMA BARABARANI WANAVIGEZO GANI KUIACHIA HII COMPANY IENDELEE KUTOA ROHO ZA WATU?.MOHAMED TRANS NI TERROLIST BUS KWANI THIS IS ENOUGH NOW.KILA SIKU LINAUWA JE HADI LINI?.

    ReplyDelete
  2. Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu 19 waliopoteza uhai wao kwa ajali hii.

    Haya mabasi yataendelea kutumaliza tu na watu hawasemi chochote, hivi kwanini? Mbona nchi za wenzetu hazitokei ajali za ovyo kama hizi? Kwanini Serikali isichunguze vizuri kuhusu jambo hili. Kila mara ajali ajali, na watu wanaendelea kufa tu, mabasi yanaendelea kukimbia ovyo bila hata sababu.

    ReplyDelete
  3. Kaka michuzi hii tuangalie tunaongea point japokuwa unanibania sana lkn ujumbe umefika hata kwako ila ninachosema hii wizara inayoshughulika na mambo haya ipo wapi jamani tunapoteza ndugu zetu wengi sana kwenye ajali hizi za barabra mie ni mdau wa blog yako nipo ughaibuni kwa hili miaka yote hii kama ingekuwa ulaya mawaziri wangekuwa walishajiuuzulu sana lkn bongo wa2 wanakufa hata waziri anayeshughululikia na haya mabo wala hana hata habari jamani plz serikili tunaomba muwe na huruma ya wananchi walio waweka madarakani jamani muungu atawaulizi kama viongozi wetu kuweni na imani au mapaka watoto wenu wapte na ajali za vx zenu ndio mchukulie atua tuangalie kila siku watu wanakufa mie nilpo ulaya nchiliyokaa sijawa wahikusikia ajali kama za bongo na viongozi wamekaa kimya kama nchi yetu tuwe na huruma michuzi hata ukibania lkn hata wewe ujembe umeusoma kaka mithupu massage sent ........mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  4. SAMAHANI KWANZA BWANA MICHUZI HIZO NAMBA ZA USAJILI ZIKO WAPI HAPO?,PILI MBONA HAYA MABASI YA BONGO YAKIPATA AJALI KIDOGO NI WATU 19? NA PIA LIMEGONGANA NA GARI DOGO JE LINGEGONGANA BA FUSO?au NDIO YANABADIKWA BANDIKWA TU MABATI,AU ITAKUA MICHUZI AMEKOSEA LITAKUA LIMEUNGUA MOTO,bYE THE WAY-HIVI MBONA AJALI ZA KIJINGA JINGA KILA SIKU,KWANINI KUSIWEPO NA ALAMA ZA BARABARANI NA NATIONAL SPEED LIMIT?AU KUNA KAMPENI YAKUMALIZA NDUGU ZETU HUKO BONGO,SERIKALI NDIO CHANZO KAMA KUNGEKUA NA ALAMA ZA BARABARNI NA KISHA MADEREVA WAKAKAA SHULE KAMA ULAYA VILE BASI 79% AJALI ZINGEPUNGUA.mDAU nuramo

    ReplyDelete
  5. Maisha ya Mtanzania hayana thamani - Jadili

    ReplyDelete
  6. JAMANI, NINYI WATANZANIA(VIONGOZI] WENYE MAMLAKA YA KUWEZA KUANGALIA USALAMA WA MABASI HAYA YA MOHAMED JUENI KUWA MNASHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA KUWAUA WATU NA MNA LA KUJIBU MBELE YA MUUMBA.FUNGIENI MABASI ILI AKIFILISIKA ATAJUA UCHUNGU WA ROHO ZA WATU HUYO MOHAMED.HUU NI UZEMBE TENA USIO NA KIFANI NA MOHAMED UJIANDAE KUJIBU MASHTAKA YA KUUA WATU MBELE YA MUNGU SIKU YA KIAMA

    ReplyDelete
  7. mtanzania amepikiga kila kona. akibaki kijijini anakufa kwa njaa! akipanda basi kwenda kutafuta riziki mjini (kwa wajanja), basi linamnyonga! akifanikiwa kufika huko anafisadiwa. watawala wanataka tuwaimbie nyimbo za misifa, tusiwakosoe! ukiwakosoa eti chuki. laana.

    ReplyDelete
  8. Hizi ajali kama wanavyosema wadau sijui hadi afe nani ndo mamlaka zistuke. ajali kama hizo ni mtaji mkubwa hapa ulaya hiyo kampuni ingeshafilisiwa siku nyingi kwa ajali kama ile ya singida iliyouwa watu zaidi ya 20. Mawakili wetu uchwala wanasubiri kesi za ufisadi tu hawajui kama mchango wao unaweza kusaidia kupunguza ajali hizi endapo wangewasaidia waathirika kuzishitaki kampuni husika a kudai fidia. kampuni zisizokuwa makini na kujali viwango zingeshaisha zenyewe, kalagabaho.

    ReplyDelete
  9. kwa miezi hii ya karibia na sikuku ni kawaida,kuna garage moja nilikuwa ninabishana na fund alikua ananiambia miez ya december ni miez ya biashara kubwa kwao mim nikambishia sana sasa siku moja kwenye january 2009 nilienda kufanya service gar yangu kwake nikakuta yard yote imejaa magar yaliyopata ajali mpaka nje ya gate aliponiona mara moja akaniambia angalia niliyoyasema.
    Kwa maoni yangu Inawezekana hizi ajali zinatokea kwenye miez hii kwa sababu kunakua na movement nyingi za magar na barabara zenyewe zimechoka na ni finyu watu wengi wanakua wanaenda mikoani na pia ulev wa madereva weng,kuna watu wengine siku za kawaida wanakunywa pombe kidogo au hawanywi kabisa lakin ikifikia sikukuu wanakunywa kupita kiasi.Halaf pia abiria wanachangia sana mim nilishashuudia kwenye bas abiria wakimgombeza dereva kwa nin anaendesha gar polepole sana wakatishia kabisa kuwa next time hawatalipanda manake linawachelewesha kufika na kwa sababu ya mwendo mdogo linawachosha,kwa hiyo wakat mwingine tusiwalaumu sana madereva.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...