Mpiganaji Rachel Obadia Lugoe (shoto) akifurahia nondozzz yake ya Masters in International Communication Management katika chuo kikuu cha The Hague University cha Uholanzi na Course Manager wake, Ms Maggie O'Neill. Rachel ni mwandishi wa habari mwandamizi ambaye amefanya kazi vyombo mbalimbali

Rachel akipongezwa na course na Manager wake Ms Maggie O'Neill mara baada ya kula nondozzz yake.
Baadaye kulifanyika tafrija fupi ya kujumuika na baadhi ya Watanzania kwa msosi.
Mpiganaji Rachel akigonga glass(cheers) na watanzania wenzake ikiwa ni ishara ya kumpongeza, kumtakia kheri, furaha na mafanikio zaidi kwa kupata Masters in International Communication Management.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. ..I was wondering where you were....Kumbe ulipotelea Uholanzi....Hongera sana Rachel kwa kuhitimisha masomo salama! Nakutakia kila la heri katika pilika za maisha baada ya masomo yako.

    Faustine
    drfaustine.blogspot.com

    ReplyDelete
  2. umemaliza skuli rudi hm utuletee ujuzi,achana na mabox kama watu wa Uk wanamaliza skuli bado wanamg'aninia mabox ukiwauliza wanakwambia wanarekebisha kwanza ndio warud. teh! teh!

    ReplyDelete
  3. Kumbe hata waholanzi wanavaa majoho wanapopata nondo?

    ReplyDelete
  4. Dada Rachael ongera sana,
    nimefurahi sana kuona kwamba umefanikisha masomo yako, nakutakia kila la kheri na Mungu akutangulie katika maisha yako.

    ReplyDelete
  5. kwa nini watu wakiona mssosi uwa wanacheka sana?

    ReplyDelete
  6. hongera sanaaaaaana kwa kula nondo elimu haina mwisho

    ReplyDelete
  7. Kumradhi nielekezeni sijui.

    Hivi vyuo vingine uko ulaya cheti huwa wanakabidhiwa ofisini/chumbani na mwalimu wako maana hapa sioni kama kuna dalili za mkusanyiko wa sherehe kama inavyokuwaga hapa. Sina maana kwa picha hii tu nilishaonaga na nyingine nyingi, leo sasa imebidi niulize.
    Nasema tena kumradhi

    ReplyDelete
  8. Hongera mno jirani....bora watakuheshimu sasa na kukutunzia ardhi yako,welcome home again.....

    ReplyDelete
  9. Hongera Dada Rachel kwa kupata Masters! Najumuika na family yangu kukupongeza na kukutakia afya njema. Najua unazoa picha nyingi na slides hivyo naomba ukifika Bongo nijulishe nikutembelee ili nizifurahie. Au hurudi??!!!!!. Picha zako ni nzuri mno dada!

    ReplyDelete
  10. Hey Rachel, HONGERA! Habari njema!

    - Chemi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...