Na: EDWARD BALANDYA & SIMON KIMARO
(Wadau wa idara ya Fedha-Stanbic Bank)

Wafanyakazi wa idara ya fedha kutoka Stanbic bank (T) Ltd wiki hii waliwakilisha
wafanyakazi wenzao wa benki katika majukumu ya kijamii pale walipowatembelea marafiki wenzao wa kituo cha FRIENDS OF DON BOSCO kilichopo Dar es salaam maeneo ya Kimara -Suka. Kituo cha DON BOSCO kina idadi ya watoto 70 wa rika mbalimbali, kuanzia umri wa miaka 4 mpaka 20, wanaosoma katika shule ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya juu.

Idara ya fedha ya Stanbic Bank (T) Ltd huwa inajinyima kwa kukatana sehemu fulani ya mishahara kwa kila mwana idara, na makusanyo hayo hutolewa mara mbili kwa mwaka kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii.

Makusanyo pia hupokewa kutoka kwa wafanyakazi wengine wa Stanbic Bank (T) Ltd ambao hujitolea chochote, ambavyo vyote hukusanywa na kuwakilishwa kwa wahusika kwa niaba yao.


Juu na chini ni Wadau wa Stanbic Bank (T) Ltd wakiwa na marafiki zao wa friends of Don- Bosco.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mzee Simon safi sana hivyo ndivyo inavyotakiwa mana hata kwenye vitabu vya dini imeandikwa tuwasaidie wenzetu

    ReplyDelete
  2. MANENO UMENENEPA HIVYO NA MAMA SWEKE. MANENO BWANA MDOGO MAMA SWEKE TULIKUWA PAMOJA NBC, MIMI SIPO TENA HUKO.

    ReplyDelete
  3. Frenu Decoration Training CentreJune 08, 2012

    Helo, this is Nuru Isango from Tanzania in East Africa writing as a Principal at Frenu Decoration Training Centre hereby, informing you that i would love to volunteer my College to support five children/youth from your foundation to join our centre that provide three main course include Decoration, Computer and English of which we believe these children will have the best opportunity to use their skills and ability from the knowledge they acquire and end the poverty by become a self employed in the market of Decoration.
    If you found it applicable and helpful to these children then we can sit down to have a discussion to the rest of the number remain/interested as we are very open and flexible to discuss any potential opportunity that might arise with you.
    Our centre is located at Chang'ombe -keko Toroli in Temeke District
    p.o.box 42870, Dar es salaam,
    Mob: +255652 831 421/+255712 590469
    Email:frenu2012@gmail.com
    i have mentioned the above contact should you require further information

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...