MTANGAZAJI WA TBC JERRY MURO (PICHANI) ANASHIKILIWA NA POLISI KATIKA KITUO CHA KATI JIJINI DAR KWA KILE KINACHODAIWA KUNASWA KATIKA MTEGO WA KUPOKEA RUSHWA TOKA KWA MWANANCHI MMOJA WA JIJINI.
MEDANI ZA KIPOLISI ZIMETHIBITISHA KWAMBA JERRY MURO, AMBAYE NI MTUZWA WA MWANDISHI BORA WA TV KWA MWAKA 2009, AMEKAMATWA LEO JIJINI AKIPOKEA SHILINGI MILIONI 10 KABLA MTEGO ALIOWEKEWA HAUJAFYATUKA.
KAMANDA WA POLISI WA KANDA MAALUMU YA DAR AFANDE SELEMANI KOVA ANATARAJIWA KUTOA TAARIFA KAMILI WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA NA GLOBU YA JAMII ITAWALETEA PINDI HABARI MPYA ZITAPOINGIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. Wamemtegeshea kaka wa watu kisa yeye aliwafichua.

    Polisi wa Tanzania ni MAFIA. Hawaguswi.

    Shame!!

    ReplyDelete
  2. It was about time....

    ReplyDelete
  3. hey! mr misupu what is conspirancy?

    NONDO

    ReplyDelete
  4. Hii ni kutaka kumnyamazisha maana uozo polisi walioufikia hautamkiki, telling u na sisi hatunyamazi hata kama nusu yetu hatutafika lakini uozo wa polis lazima uanikwe hadharani! Wantanzania tusikae tu tukaangalia jambo hili lets fight for justice!

    ReplyDelete
  5. huyo ni mtu mdogo tu.kama kweli tunapiga vita rushwa basi tuanze na Tibaigana na kadhalika

    ReplyDelete
  6. Huu ni mchezo wa kitoto, Jerry ameonewa na ametegeshewa,hakuna aliye msafi! polisi wameungana na kuufanya huu mchezo, tulisikia vijiweni wakizungumza. tena trafiki wamepanga kufungua kesi mahakamani, habari tunazo. Mwacheni Jerry Muro mchimchafue!

    ReplyDelete
  7. Polisi acheni hizo! huu ni mtego, tena mnafanya ujinga! kwanini asingekamatwa siku za nyuma? kijana ni mwadilifu, acheni afanye kazi.

    ReplyDelete
  8. Polisi wanachemsha. huo ni mchongo, dogo baada ya kuwaumbua trafick. hebu wamwache afanye kazi, Kaka Tido, hebu msaidie dogo aendelee kutupasha habari.

    Hivi polisi hamwoni aibu? tunajua mipango yote hadi ya kuchangishana pesa kutaka kuishitaki TBC.

    ReplyDelete
  9. Duh it is very sad kwa kweli LAKINI hiyo lazima ni FIX. Katika Nchi hii Kushinda vita dhidi ya Rushwa ni ndoto kwasababu

    1. Watu kama Jery Muro ambae amekuwa mstari wa mbele kutokomeza swala la rushwa dhidi ya polisi wanakuwa wanahatarisha maisha yao na walarushwa ndio mbinu zao kuwakamatisha na kuwafix watu hao . Mimi siamini kama kilochotokea ni kweli kuhusu Muro it must have been cooked. Ni Mbaya sana.

    2. Rushwa ni Mtaji wa wantu wengine sana wenyewe pesa kwahiyo kushinda vita hii labda mpaka YESU arudi tena.

    Inasikitisha sana, inauma sana, kuona mambo kama haya yakitokea.

    ReplyDelete
  10. bongo burudani.!

    ReplyDelete
  11. walimfumnga musendo miaka kadhaa naona na sasa wanataka kushikisha adabu dogo.

    ReplyDelete
  12. Nchi hii wachapakazi hawatakiwi hata kigogo,watu kama jerry walikuwa wanahitajika enzi ya nyerere na sio sasa,polisi wameamua kumfanyizia tu kulipiza kisasi cha kuanikwa wakipokea rushwa katika magari,ukiwa mchapa kazi,muwazi na mkweli nchi hii uwe na ulinzi wa kutosha la sivo unaweza hata uwawa.tizama mkurugenzi wa mwanahalisi yaliyo mkuta!!!!.inasikitisha sana kama police inakuwa hivi.polisi kuna uozo wa kufa mtu wakubali wasikubali,wewe hapa jijini unaombwa rushwa barabarani waziwazi!leseni unaweza kupata hata kama hujui kuendesha gari so ukishapata leseni unaingia barabarani kujifunza!na ndo maana hata watu hawaendi driving school coz leseni utazungushwa mwaka mzima lakini ukiwa na hela hata mtoto anapata!yuko wapi zombe aliyeuwa na kupora/kura rushwa!yaani mimi inaniuma hadi basi!!!!!!!!!!!!,kama ni umamuzi wangu jeshi la polisi ningelifuta na kubakiza JKT na JWTZ japo wanauwa wananchi.

    ReplyDelete
  13. Teheheheh!
    Tulitegemea alivyokuwa akiwafichua wala rushwa yeye ni malaika, kumbe loooo, walewale!!

    ReplyDelete
  14. Nafikiri polisi wanataka kutuonyesha kwamba hata wapiga vita rushwa nao si wasafi. Swali ni kwamba kwa nini mtangazaji alikubali kupokea pesa bila sababu ya msingi? Anapokea 10m kwa biashara gani? Kama polisi walienda na gia hiyo ya pesa bila shaka walijua kwamba huyo mtangazaji huwa anatabia hiyo.
    Waandishi wengi wa Tanzania huweka pesa mbele, ndiyo maana tunaona wakitumika kuwachafua viongozi na watu wengine hapa Tanzania.
    My take: Kitendo cha Jerry Muro kuingia mtegoni kirahisi kiasi hicho ni ishara tosha kwamba naye si msafi.

    ReplyDelete
  15. Nayeye alikuwa mpuuzi...utapigaje vita Rushwa wakati wewe mwenyewe sio msafi? Mnawalaumu tu watu bure...ninyi wenyewe majaribu ya Million 10 yanawashinda itakuwa waliokula za EPA ambazo ni mabillioni? Haya sasa yamekukuta...!!

    ReplyDelete
  16. in the US polisi walikuwa wanaitwa "PIGS" kwa kipindi fulani kutokana na tabia hizi hizi za uonevu. Itabidi polisi wetu nao waitwe "Nguruwe"

    ReplyDelete
  17. that is police game, shame on them,
    Let the guy out.
    Always in this country strong people are being weaken when fighting for corruption.

    ReplyDelete
  18. AMELIKOROGA, Kama kweli aliwekewa mtego akaingia kichwakichwa na kuzitia ndani milioni 10, mandata na TAKUKURU wakamnasa hana ujanja mashirika, atanyia debe.

    ReplyDelete
  19. Pamoja na utendaji wa kazi wake mzuri lakini waandishi wa habari wana mchezo mbaya wa kupokea rushwa, tena nikisema rushwa nitakuwa nakosea, ni blackmail hasa wanayofanya. Maana watamwambia mtu tuna ishu yako ukitaka tusiitoe tupatie kiasi kadhaa cha pesa.

    Sasa kama huyu Jerry Muro alikamatwa nyumbani kwake amekaa tu yeye na familia yake wakambambikia hizo pesa, nitasema wamemuonea. Lakini kama aliwekewa mtego akanasa, ina maana ni kweli alikuwa mpokeaji wa rushwa ila hicho kiwango kwa kweli kinatisha, milioni kumi? Basi hiyo habari au hiyo ishu itakuwa nyeti sana, ngoja tusikie na tuone.

    Nakumbuka nilikuwa na mwandisi fulani wa ITV kwenye msafara mmoja hivi alikuwa anafanya coverage ya ziara ya kiongozi mmoja mkubwa tu. Basi huyo Mwandishi alidai nimpe pesa kwanza ndio apige picha za hilo tukio na kama sikumpa pesa hafanyi kazi. Nikamwambia sikupi senti tano hiyo ni news kwa station yako na wewe hapa unafanya coverage, basi huyo mwandishi akagoma kabisa kufanya kazi. Sie tukafanya kilicotupeleka news zikatoka kwenye vyombo vingine vya serikali. Nimeishakutana na waandishi pia ambao wanakuja na news za uwongo na kuanza kublackmail kuwa usiponipa pesa nitatoa hii news kwenye vyombo vya habari. Nilikuwa nawaambia nenda katoe kama una hakika na ukweli wa habari uliyonayo. Nikiwaanika hapa hao waandishi ni aibu tupu, watu wazima na tena wenye majina makubwa!

    Kwanza rushwa unakamatwa na polisi au Taasisi ya kuzuia rushwa?

    Mbona kizungumkuti?

    ReplyDelete
  20. hatutaki longolongo tuwekeeni video tuone mchezo wote ulivyokuwa mpaka mkamkamata na hiyo rushwa kama mlivyopatikana nyie Askari.

    Vinginevyo itakuwa mme mset huyu Muro.

    ReplyDelete
  21. AMa kweli rushwa haiwezi kuzimwa. Polisi wa Tanzania hawakosolewi. Si hata ile ya
    Mwanza,aliyewataja polisi kwamba walishiriki kwenye ujambazi, saa
    chache baadaye alikamatwa akihusishwa kuwa na yeye ni jambazi. Bongo tambarare kweli kweli.

    ReplyDelete
  22. hii inachekesha kweli,ndio kusema
    kweli huyu mtangazaji alichukua rushwa ya milioni kumi?kwa kutangaza biashara gani? au kuuza kiwanja gani? kama si fitina tupu za polisi zidi ya wanahabari wanaoyaanika hadharani maovu ya polisi.

    ReplyDelete
  23. wanaokwapua mamilioni ya dola hawaguswi na wanaitwa waheshimiwa vijisenti.

    ReplyDelete
  24. PESA BWANA! WEE ACHA TU! SASA KIJANA NAYE KATUANGUSHA KWAWELI. ILIBIDI AJITAHIDI KWA KADRI YA UWEZO WAKE KATIKA KIPINDI HIKI AMBACHO KALIANZISHA TAFRANI KUKWEPA MITEGO YA JINSI HII KWA GHARAMA YOYOTE ILI ASHINDE MAJARIBU. KWANINI KAAMUA KUINGIA MKENGE HUU HATA KAMA ALITEGESHEWA? WASOMI WA BIBLIA WANAELEWA NIKISEMA UKITAKA KUTOA KIBANZI KWENYE JICHO LA MWINGINE, TOA KWANZA BORITI KWENYE JICHO LAKO. IKITHIBITIKA KWELI ALITAKA KULA MLUNGULA, KAZI YAKE YOTE ITAKUWA IMEFITINISHWA. NAJUA NI UMAFIA KAMA MWINGINE ALIVYOSEMA HAPO JUU, LAKINI ALITAKIWA KUWA SMART ENOUGH KUKWEPA MTEGO. HATARI NYINGINE NI YEYE KUJIEXPOSE KUWA HABARI HIZO ZA UCHUNGUZI NIZA KWAKE BADALA YA KITUO CHA TBC. YEYE ANGECHUNGUZA HALAFU ISOMWE TU STUDIO ILI KUFICHA ID YAKE, LAKINI MCHEZO ANAOUFANYA BONGO KUTAKA SIFA! UTAMPONZA YEYE NA WANAOMTEGEMEA. USICHEZE NA MWENYE PESA BWANA, UTAKWISHA! NAWASILISHA WADAU

    ReplyDelete
  25. INANIUMA SANA NIKIFIKIRIA NALIAAAA....! hivi nchi yetu inaelekea wapi yani hii hata kwa mtu ambaye hajasoma sana atajua ni mpango mzima wa polisi kulipiza kisasi kwa huyu mwandishi kwa kuandika kwake ukweli kuhusu kukithiri kwa rushwa kwa jesi la polisi...

    Hivi hii ni rushwa gani ya milion 10 kwa mwandishi wa habari au kuna mgodi unataka kubinafsishwa kimagendo(sidhani)... Haki ya 'free speech' sasa Tanzania inaonekana kumilikiwa na watu wachache.

    Sasa ni wakati wa waandishi wa habari kuwa pamoja katika ishu kama hizi... anyways tungojee maamuzi na ushahidi wa mahakama.... ingawa walarushwa 'mapapa' wanadunda tu kama kawa.

    ReplyDelete
  26. Eleweni kuwa, wale Police wadogo humo barabarani wamewekewa hesabu ya kupeleka kwa mabosi wao kama vile daladala zinavyofanya kazi.

    Kwa ufupi ni kuwa, trafiki anapukukamata na kudai mshiko, anaukusanya mpaka kufikia hesabu ya bosi wake na cha juu ni chake, bosi naye anakata mshiko mpaka kwa Tibaigana au sijui nani mkubwa huko.
    Kwa ufupi ni mtandao ambapo wote wanahusika.

    Hii ndiyo sababu huwezi kumshitaki police yeyote kwa rushwa kwa kuwa katumwa na bosi huyo huyo unakomshitakia, sasa kwa akili zako unadhani bosi wake atamtamtia matatani? Ni lazima watatafuta stori ya kufanya isiwe ishu na kuwaacha huru hao trafiki au police yeyote. Yaani umshitaki mafia kwa mafia sijui utapata nini zaidi ya kukutwa umekufa msituni.

    Dogo Muro alitakiwa ajue hilo. Tanzania waachieni watanzania wenyewe, rushwa ni sehemu ya maisha ya watanzania hasa viongozi wakuu serikalini, hivyo hawaoni sababu ni kwa nini muipigie kelele wakati inawanufaisha zaidi ya kuwakera, wao hawatoi wanapokea tu, kwa hiyo kwao si kikwazo ni muziki mzuri wa injili.

    Sijui mtaelewa nini wabongo wenzangu, nchi hii si yenu, toeni tu rushwa, laleni tu na njaa, ugueni tu bila kutibiwa, mjifie.
    Fungeni midomo yenu, vinginevyo ya Jerry Muro na waliomtangulia yatawakuta pia.

    Waachieni Kikwete na washikaji zake wale life.

    ReplyDelete
  27. Vendetta au kweli?

    ReplyDelete
  28. Unasema "AMEKAMATWA LEO JIJINI AKIPOKEA SHILINGI MILIONI 10 KABLA MTEGO ALIOWEKEWA HAUJAFYATUKA"....


    Kama mtego haukufyatuka wamemkamataje na kwa nini Polisi ndo wahusike kufuatilia na kufyatua mitego ya Rushwa na sio PCCB??? au hii ilikuwa na maslahi ya JESHI LA POLISI ZAIDI?

    ReplyDelete
  29. Sijaelewa hapo juu, pameandikwa kakamatwa akipokea shilingi milioni 10 kabla ya mtego aliowekewa haujafyatuka, sasa hii ina maanisha kwamba alishtukizia kwamba ni set up so hakuchukuwa hizo hela ama?

    Mwandishi naona umetuchanganya kidogo, anyways kama walivyotangulia wachangiaji wa hapo juu hii bila shaka itakuwa ni kama kisasi cha hawa polisi baada ya yeye kujaribu kuwafichua, but still kama kapokea kweli hizo hela that doesn't make him less guilty.

    Watanzania tuache hizi tabia za kupokea bahashishi, kuna mshirika yana policy kabisa ukifanya kazi na client akafurahi akakutunukia hata kazawadi kadogo basi unatakiwa umwambie kwamba its against work policy. Ila njaa ndio inayotuponza wengi wetu ndio maana tunakuwa blinded.

    Karibu kila mtu anaepokea rushwa binafsi yake huwa haiiti rushwa yani anakuwa na definition yake kwamba ni shukrani/ takrima na kadhalika. Kwa hiyo huenda na bwana Muro na yeye aliona hiyo ni takrima tu hivyo hakuna ubaya kupokea.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  30. kwanza polisi kama walipokea hiyo taarifa ya rushwa kwanini wasiwaambie TAKUKURU? Maana wao watakuwa walalamikaji na waashitaki?Ingekuwa heri ingekuwa TAKUKURU wamemkataka,Polisi wananlipiza kisasi.Very bad.

    ReplyDelete
  31. Tanzania bwana,vyombo vya sheria haswa polisi wamekuwa wananiacha hoi kwa jinsi wananvyofanya mambo yao kwa miaka mingi tu.Pole sana bwana Muro mungu atakusaidia manake inaonekana wanakulipiza kisasi kwa kuwa uliwaumbua.
    mdau
    duniayetukubwa.blogspot.com

    ReplyDelete
  32. linapokuja kuwa ni polisi kala rushwa hiyo ni kweli au mtu mwingine lakini ikiwa kwa mwandishi wa habari huyo kabambikiwa au kategewa.

    sijui ukweli uko wapi lakini hata wewe hujui. ukweli utajulikana baadaye.

    ReplyDelete
  33. Wadau nashindwa kuwaelewa, rushwa ni rushwa kama kweli kachua rushwa shame on him, wacha sheria imuukumu maana kama ni kweli alikuwa anatufool tumuone yeye ni msafi kumbe si kweli na wapo wengi wa namna hiyo! Ni upuuzi kukemea wala rushwa kama wewe ni mmoja wao!

    ReplyDelete
  34. jamani jamani police achen dhambi nzito kama hiyo kama kuwafukuzisha kazi vibaraka wenu ndo mmeamua kumtenda hivyo mtoto wa watu yatawarudia hata dini zetu zote mbili haziruhusu mnadhambi nzito kama kweli mmemsingizia mkatubu kabisa! NATOA WITO KWA WANAHABARI WOTE UNGANENI MARUFUKU KUANDIKA HABARI ZA POLICE KAMA KWELI MNAMPENDA MWENZENU.

    ReplyDelete
  35. Every promising Star in Africa is damned! This is the curse of Africa!

    ReplyDelete
  36. TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO!

    ReplyDelete
  37. Du Hii kweli TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO....YANI KAMA KUSOMA HUJUI HATA PICHA UTAONA...POLISI SHAME ON YOU,HUU NI MCHEZO MMEMFANYIA JERRY MURRO KWA KUWAUMBUA MKILA RUSHWA NA NYIE MMEUNDA GENGE ILI KUMUINGIZA MTEGONI...NAYE KOVA ALIHAJI LKN HATA PICHA HAIONI? KESHO HATA MKITANGAZA HATUTOAMINI HIYO HABARI,KWANIN BAADA YA KUWAUMBUA NA NYIE MMEAMUA KUMUANGUSHIA JUMBA BOVU,SASA WANAOKAMA RUSHWA NI PCCB AU POLISI?

    NI MIMI MDANGANYIKA.

    ReplyDelete
  38. Pole sana ndugu Muro.Kama wamekuonea ukweli utaonekana na ninahakika utatoka salama na kuendeleza mapambano.Ninachotaka kukumbushia kwa wanamapambano wote wa rushwa ni kwamba ni lazima kuikwepa mitego yote inayowekwa.Kwani ukikubali kuingia kwenye mtego,utakuwa unausaliti upambanaji wako.Au kama ukitaka kuuteguwa mtego uliotegewa; wewe toa taarifa TAKUKURU kuwa kuna mtu au watu wanataka kukupa rushwa; TAKUKURU ipo kwa wapokea rushwa na watowa rushwa pia.Kwakuwa wewe utakuwa tayari umetowa taarifa hiyo TAKUKURU wataweka mtego wa kumnasa mtoaji na si wewe tena.Polisi wetu wanachezo mbaya ndiyo maana wahenga walisema usifanye urafiki na polisi,kwani hawachelewi kukugeuzia. Hivyo wapambanaji wote wa haki bini haki mlijuwe hilo.

    ReplyDelete
  39. walikuwapo wengi wakapita.. nadhani it is high time kwa Jelly kupita. hakuna marefu yasiyo na mwisho.. wamelewa amani ya nchi ndiyo maana wanafanya mchezo mchafu kama huo.. kijana anafanya kazi sasa wameona kumnyamazisha waendelee na ufisadi wao ni kumtengenezea bomu... amani ya nchi itavunkika kwa upumbavu wa watu wachache... wamfunge basi huyo kijana waone jinsi watu wanavyosema inatosha... ipo siku kama siyo leo inakuja karibuni watanzania watasema inatosha.. hapo hata bunduki huwezi warudisha nyuma...

    ReplyDelete
  40. 1. Jamani si rahisi kufikiri kuwa Jerry aliyejitokeza kwa ushujaa hivi karibuni kuwaumbua Polisi wala rushwa halafu naye anapatikana na kosa hilo hilo kabla jogoo hajawika.
    Ukweli utajulikana hata kama ni baada ya karne!

    2. Ni vema tuseme kuwa wapokea rushwa tz si maaskari wa barabarabi tu. Yaani kuna waandishi wengi tu wa habari kama walivyosema wengine hapo juu ambao bila kumpa fedha eti hatoi habari. Au anakuja na kukutishia kuwa kuna habari mbaya inayokuhusu hivyo anataka fedha ili asikuandike vibaya. Huu ni ukiukaji wa maadili ya kazi yao na naomba WaTz tukatae kabisa kuhonga waandishi wa habari au watangazaji kwa namna yeyote ile kama ambavyo tunapaswa kuwakatalia Polisi wa Trafiki n.k

    3. Ufisadi wa Waandishi si kuwa unafanyika kwa fedha tu bali pia ni kwa kuwazuia watoa comments zao kinyume na matakwa yao na rafiki zao wanaowalinda. Nadhani hii haihusiani na blogu hii, maana kama inahusika basi naye awe macho na mitego ya namna hii.
    Yaani nitaweza kwenda TAKUKURU na kuandika mbele yao comments ambazo hazichafui hali ya hewa, ukiziminya tu tunajua kuwa kweli unayemlinda mnakula naye!

    Na waandishi hawawezi kususia kuandika habari toka Polisi eti kwa sababu Jerry kakamatwa. Habari ni haki yetu wananchi na si marupurupu ya Polisi!

    ReplyDelete
  41. KAMA NI KWELI KAPOKEA RUSHWA, ANATAKIWA AFUNGWA ZAIDI YA WENGINE. KWA SABABU YEYE ALIKUWA ANAFICHUA MAOVU AMBAYO YEYE MWENYEWE ANAYAFANYA.

    DAWA NZURI KWA WANAFIKI,WANAO ICHEZEA JAMII .

    ReplyDelete
  42. Mama hellenasraFebruary 01, 2010

    Jerry usipokuwa makini watakuua kabisaaa..
    Nchi hii sio ya kutafuta sifa,waachie nchi yao,hawapendi kuchokonolewa

    ReplyDelete
  43. Kaka misupu,hii too mucha sasa.
    Na amini usiamini, polisi ya Bongo imekuwa kama ni genge la wahuni flani ambao wao wana uwezo wa kukufanya chochote na wewe unatakiwa kunyamaza kimya..

    Hivi rushwa ya 10 m, huyu mhasibu wa bagamoyo,amazitoa wapi 10m. Kwa kipato gani cha kumuwezesha kutoa rushwa ya 10 m. Mhasibu wa bagamoyo acha kutumiwa na polisi, ndio hao wanaokula rushwa za kijingajinga, tunajua wanatuwa na maboss wao, kwa nini wakutumie na wewe? Hebu kuwa jasiri, tunajua kabisa wewe uwezo wa kutoa rushwa ya 10 huna. Vinginevyo wewe ni mla rushwa mkubwa na wa kutupwa. Waziri mkuu tu ana shi 25 m bank, wewe umezitoa wapi, acha wizi na wewe jinga mkubwa wewe....

    ReplyDelete
  44. JERRY POLE SANA. WEWE NI COLLEGE MATE WANGU PALE MLIMANI.NAKUKUMBUKA SANA MISIMAMO YAKO. NA UNAYOYAFANYA NI MATUNDA YA AKINA PROF. BAREGU, LWAITAMA, MUKANDALA, MUKANGARA NA WENGINEO. HII NCHI AJABU SANA. WAMEANZA NA WALIMU WETU KUWANYIMA MIKATABA, SASA WMEKUJA KWA SISI WANAFUNZI WAO, LAKINI HATUACHI KUSEMA. WATANZANIA FANYENI KITU KIMOJA SEMENI LOLOTE MNALOLIONA HALIFAI MPAKA WENYEWE WATAONA AINBU. NA MIMI NAANDAA BOMU HUKU NILIKO MAANA NI JIMBONI KWA MZINDAKAYA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...