Rome: Jana tarehe 30 Januari, Mjini Rome, Italy, kulikuwa na mkutano mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Roma. Mkutano huu ulikuwa na agenda mbili, kwanza ni Kupitisha Katiba ya Jumuiya ya Watanzania Roma, pili kuchagua Viongozi.
Mgeni rasmi kati mkutano huo alikuwa Mh. Salvator Mbilinyi, ofisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italy ambaye alimuwakilisha Mh. Abeid Aman Karume, balozi wa Tanzania nchini Italia.
Waliochaguliwa kuwa Viongozi ni ndugu Leonce Uwandameno kama mwenyekiti wa Jumuiya, ndugu Erasmus Luhoyo Pindu, kama mwenyekiti Msaidizi, Diana Olotu kama Katibu msaidizi. Katibu na Mweka hazina wamebaki wale wale yaani Katibu Ndugu Andrew Chole Mhella na Mweka Hazina ndugu Awadhi.
Kwa picha na habari zaidi tutembeleeni hapa
ondoeni hiyo miziki kwenye blog yenu...inakera, sisi tunataka kusoma information na siyo kusikiliza muziki, Also too much stuff..ondoeni weather, messenger pingbox, exchange rate, and currency converter....zinaifanya blog yenu inakuwa slow and congested...sisi tunaochajiwa kwa bandwith inakuwa soo... JUST MY OBSERVATIONS!!
ReplyDeleteni vizuri ndugu zetu Italy mnaonyesha umoja.
ReplyDeleteMdau
Duniayetukubwa.blogspot.com
Mbona wakristo watupu, hakuna watanzania waislam hapo roma. Nauliza tu!!!
ReplyDeletewakristu au waislam wote ni watanzania hatuna ubaguzi angalia vizuri we mdau uliyeulizia khsu suala la muislam au ukristu yupo mweka hazina ni muislamu na muwakirishi wa wajumbe pia ni muislamu. asante sana michuzi umeitoa watanzania wote ni ndugu hatuna udini wala ukabila.asante mi mdau.
ReplyDeleteOngeleni sana kwa umoja wenu ndugu zangu Watanzania wa Roma. Watanzania wengine waishio nchi za nje wanashindwa kuwa na umoja kama nyie, wanatawaliwa na chuki na matatizo ya kila aina. Mungu Ibariki Africa mungu Ibariki Tanzania!
ReplyDeleteMbona London wote ni waisilamu na hakuna anayelalamika? Na huku Bongo wote ni waisilamu na hakuna anayelalamika. Nilikuwa nashangaa tu.
ReplyDeleteWatu wengine sijui mtakuwa lini. Karne ya 21, na bado mawazoni mmekalia mambo ya UDINI tu badala ua kufikiria mambo muhimi ya kuendeleza nchi yetu na jamii zenu hapo ulipo.
ReplyDeleteDini yako inakusaidia nini wewe hapo ugenini ? Watu kama nyie ndio mnawarudisha wenzenu nyuma, kwa kung'ang'ania mambo yasiyo na msingi.
Community nyingi za waTZ ZINAKWAMA kwa sababu watu kama nyinyi. Huyu dini hii, na yule dini ile. Grow up people!!
Muhimu sana, sasa tujiulize nchi nyingine mbona hatusikii? balozi zinashindwa kuwahamasisha watanzania kuanzinsha umoja, kila mtu anajifcha kama panya buku... umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, penye wengi hapa haribiki jambo!
ReplyDeletetuige mfano huuu
sishangai hasilani,kuna imani/dini tu wakiwaona WAKRISTO basi damu zinawachemka na roho ya kuua inawaingia ghafla...wao ni ruksa na kheri kuchukia wakristo.msipate shida kumlinganishia mahali kwingine kwenye dominant religion/pple
ReplyDeletedini zenyewe zililetwa tu afrika
ila ivi vyama mh!!!aya
Hongera sana.
ReplyDeletekama Mhella ninayemfahamu ni Deo je umeshamaliza shahada yako ya uzamivu? Tulikutana Torino. Kweli nawapongeza sana kwa umoja wenu.
nduguyo
Mzalendo kutoka Tabora
Mzalendo toka Tabora hapo juu, Deo Mhella ni kaka yake Andrew Mhella.
ReplyDelete