Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN); Mzalendo Sanctus Mtsimbe; akitoa maelezo ya misaada iliyokusanywa katika awamu ya pili ya Kampeni kwa ajili ya kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko inayoendeshwa na TPN, Globu ya Jamii na JamiiForums.
Pichani ni misaada mbalimbali ambayo ilikusanywa na Wadau mbalimbali. Mz. Mtsimbe alisema hadi sasa zaidi ya watu 1880 wanachangia katika kampeni ya SMS. Vitu vilivyokabidhiwa ni pamoja na ndoo; magodoro; miswaki na dawa za miswaki; sabuni; vyandarua; mablanketi; maji ya kunywa; Nguo mbalimabli za kike, kiume,watoto, Mataulo, mashati, Suruali; Viatu na Madawa ya chooni vyote vikiwa na dhamani ya TZS Million 5.
Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN); Mzalendo Sanctus Mtsimbe; akitoa maelezo ya misaada iliyokusanywa katika awamu ya pili ya Kampeni kwa ajili ya kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko

Mlezi wa TPN Mzalendo Dr. Maua Dfatari (kati) akitoa maelezo kuhusiana na kampeni kwa; Mkurugenzi wa Maafa wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo (Kulia) katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Chama Chama Msalaba Mwekundu, Masaki jijini Dar.

Alisema TPN imefurahi kuwa imetoa changamoto na sasa wadau mbalimbali wanasaidia na kuendesha kampeni kuwasaidia wahanga ingawa ilikuwa ni jambo jema kuunganisha nguvu kwani wote lengo letu ni moja. Aliasa kuwa Muhimu kuliko vyote ni kuhakikisha kuwa misaada inafika kwa walengwa. Kampeni yetu inaendelea kwa kutuma SMS yenye neon TPN kwenda namba 15522.

Mlezi wa TPN Mzalendo Dr. Maua Dfatari (kati) akitoa maelezo kuhusiana na kampeni kwa; Mkurugenzi wa Maafa wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo (Kulia) katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Chama Chama Msalaba Mwekundu. Mzalendo Daftari aliweka wazi kuwa Kampeni yetu ni ya Kukisaidia na Kukiwezesha Chama cha Msalaba Mwekundu Red Cross na haina uhusiano wowote na kampeni ya Red Alert inayoendeshwa na Vodacom.

Alisema TPN imefurahi kuwa imetoa changamoto na sasa wadau mbalimbali wanasaidia na kuendesha kampeni kuwasaidia wahanga ingawa ilikuwa ni jambo jema kuunganisha nguvu kwani wote lengo letu ni moja. Aliasa kuwa Muhimu kuliko vyote ni kuhakikisha kuwa misaada inafika kwa walengwa. Kampeni yetu inaendelea kwa kutuma SMS yenye neon TPN kwenda namba 15522.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Unajua wadau nilidhani mnatania mlipoanza hii kampeni; kumbe mko serious! Hongereni na mimi nitajiandikisha.

    ReplyDelete
  2. HAWA SI WAHANGA KWANI HAWAKUJITOLEA WAATHIRIKE NA MAFURIKO BALI NI WATHIRIKA, TUJUE KUTUMIA MANENO SAHIHI.

    ReplyDelete
  3. Asante sana mama yetu,
    maana hata sisi walala hoi umetuwezesha kwa urahisi ukilinganisha idadi ya watu wenye simu na wengi wetu uwezo wa kuchangia 4500 kwa mwezi inayokatwa 150 kwa siku ni rahisi sana ila napendekeza namba hizi ziwe za kudume na kutangazwa zaidi wakati wa maafa.
    Pamoja tunaweza mama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...