Bondia Rogers Mtagwa (kati) Steven Luevano (kulia) ambaye ndio bingwa wa Bantam (WBO) na wa kushoto ni Juan Lopez aliyempiga Mtagwa mara ya mwisho ndio bingwa wa WBO Feather mpinzani wake toka Cuba Yuriokis Gamboa hakuwepo kwenye press conference hiyo.
Bondi Mtanzania anayepigana akiwa Marekani, Rodgers Mtagwa, ataingia ulingoni tena hapo kesho Jumamosi katika ukumbi wa Madison Square Garden jijini New York.

Mtagwa anaingia kwa mara nyingine tena kutafuta nafasi nyingine ya kutwaa taji la WBA dhidi ya bondia hatari kutoka Cuba Yuriokis Gamboa ambaye nduye bingwa mtetezi wa taji hili la uzito wa unyoya (WBA).

Akizungumza na sauti ya America Mtagwa amesema yuko tayari na amejiandaa mno hivi sasa kuliko hata lile pambano lake lililopita na Juan Lopez ambalo liliacha gumzo kubwa mjini New York ambapo Mtagwa alishindwa kwa utatanishi.

Aliongeza kwamba anakimbia kila amekuwa akipiga begi kila siku na yuko kwenye uzito unaotakiwa na amejiandaa kwa raundi zote 12.

Mpinzani wa Mtagwa kwa upande wake ni bondia hatari lakini kama alivyokuwa Lopez yeye pia hajawahi kupigana zaidi ya raundi sita kwa muda mrefu sana mapambano yake mengi yanaisha kwa KO ikiwa ni chini ya raundi 6.

Usiku huo pia Juan Lopez ambaye ndiye bingwa wa WBO (Feather) na hivi sasa ameongeza uzito kutafuta kuchukua mkanda wa pili katika uzito wa Bantam na bingwa wa uzito huo wa (WBO) Steven Luevano.
Kwa habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...