Mkuu wa Wilaya ya nanihiii, aksante kwa kuendeleza libeneke kwenye globu yako hii ya jamii. Twafurahi sana kwa updates zako za kila dakika, kazi yako inaonekana kaka. Mie nna jambo linanitatiza sana kwenye hii nchi yetu yenye maendeleo ya kasi; naomba niwakilishe kwako kaka.

Unajua siku hizi familia kibao zina usafiri binafsi. Ila nadhani wengine ni limbukeni hasa ukitegemea anataka mwanae apate starehe ambazo yeye hakuzipata wakati anakua. Matokeo yake ni maafa kwa hawa viumbe wasio na hatia. Utaona mzazi akiwa na mwanae kwenye gari halafu hajali kama mtoto amekaa kwa usalama wakati yeye amepiga belt.

Mara nyingi huwa naona watoto wakicheza cheza na kuruka ruka kwenye gari wakati watu wote wazima wakiwa wamefunga mikanda na kuhakikisha usalama wao. Sioni busara iko wapi hapa. Tena utakuta gari inaendeshwa kwa kasi ya ajabu na brake zisizo na mpangilio, sasa yakitokea tusiyoyaombea huyu mtoto anakuwa na hali gani? Nani wa kulaumiwa?

Kwa umakini sana nimefuatilia hawa watu hawazuiwi na traffic na kupigwa faini. Sijui hapa kwetu huku hili ni swala la kawaida? Nadhani umefika wakati tuanze kuliangalia hili jambo upya, maana hivi vigari vyetu visiwe chanzo cha kuwapa wengine majanga, maana mtoto akiwa loose kwenye gari anaweza akaanza kufanya fujo na kumfanya mzazi kusababisha ajali, kitu ambazo kitakuwa ni uzembe wa hali ya juu.
Mie nilikuwa naomba Traffic badala ya kuona ni jambo la kawaida wawapige bao hawa watu tena bila huruma, maana leo asubuhi nimekutana na familia zaidi ya tano zikiwa zinafanya mchezo huo huo. Jamani huu ni ulimbukeni, fikiria kwanza usalama wa watoto kabla ya kufanya mambo haya, au michuzi hawa wameletewa leseni nyumbani nini? Maana sidhani kama kuna shule ambayo haina mkazo kwenye usalama wa abiria na wapita njia.

Hivi Michuzi, Imagine baba au mama amefunga brake ya ghafla, mtoto atakuwa na hali gani? Mie niliyoyaona yanatosha ila naomba wafikishie wadau wapate kuelewa kuwa kama mtu mzima anafunga mkanda kwenye gari iweje mtoto aachwe arukeruke na kutembea kama vile gari imekuwa uwanja wa soka na vilevile gari iko kasi?

Mie noana si ustaarabu. Mkuu wa Wilaya, Mifano iko mingi sana kwa wenzetu wa dunia ya kwanza, traffic akiona mtu anaendesha gari na mtoto hajafungwa mkanda vizuri hilo ni kosa kubwa sana, na adhabu ni kali lakini kwetu wanaangalia na kucheka tu. Mie naomba niwakilishie hili maana inaudhi kwa watu wazima kukosa kufikiria jambo la hatari kama hili especially kwenye mji wenye ajali kila dakika kama daslama.

Nawakilisha

Mdau wa River Between
Mbezi kwa Komba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. HAWAJUI UDEREVA NI KZI SIO FANI. WANAFIKIRIA SIFA ZA KUMULIKI GARI NA SIO USALAMA BARABARANI . NI USHAMBA TUU WENGINE UTAWAONA HUKO UGHAIBUNI WAKISHAENDESHA MAGARI BASI NDIO WANAONA WAMEUKATA. JAMANI ENDESHENI VICHWA SIO MAGARI. DADA ZETU PIA KAMA HAUNDESHI WANAKUTOLEA NJE????

    ReplyDelete
  2. tzforchange naona una ka roho ka kwanini.....ni vipi ushamba mtu kuendesha gari???Raha jipe mwenyewe banaaah kama vijisenti vipo kwanini mtu asiwe na miguu minne????kula kitu roho inapenda "we r only live once".
    mdau wa Bahi

    ReplyDelete
  3. kamaua mama/baba but be careful we need u drive safely.

    tzforchnge

    ReplyDelete
  4. ebwaneee..kuna siku niko barabarani nikamuona jamaa anaendesha gari huku amempakata mwane kwenye mskano...duh ilinibidi kwanza nijiiulize niko wapi..labda nilikuwa naota....lakini nkaambiwa hii ni bongo...mdau umesema ukweli...wengi hawajui umuimu wa ufungaji mikanda...

    ReplyDelete
  5. heee mtoa mada kuna leseni za kuletewa nyumbani???

    .....................?

    ReplyDelete
  6. Ni kweli kabisa mdau,nadhani uzembe mkubwa upo Traffic police wanatakiwa watoe elimu kwa mtu anayepatiwa lisence,,hasa madereva wa kike

    ReplyDelete
  7. Sasa wewe mdau unataka kuleta mambo ya wazungu kwa wabongo hapa! Tangu lini wabongo wakawa na viti vya watoto kwenye magari? Ikitokea ajali si mipango ya Mungu?

    ReplyDelete
  8. ANON 10 09 UMEENDA SHULE MPAKA MWISHO MUNGU NDIO MLIZI WA WATU WOTE SASA HAO WADHUNGU WASIOMUAMINI MUNGU WAAAMINI UTAALAMU WAO WAKO GIZANI USHAMBA WETU TUNABAKIA KUIGIZA.

    tanzania for change dot gov

    ReplyDelete
  9. ASANTE SANA MDAU KWA KULETA HILI SWALA NASHAURIANA NA WEWE MIMI MDAU NAISHI HUKU KUSIKOISHA MABARAFU NILIKUWA HOME HATA KUPANDA TAKSI MIKANDA HAKUNA NA HATA HAO WATU WA SHERIA ZA BARABARA HAWAJUI HATA WALA MAANA YA SHERIA YA BARABARA WAO SHIDA YAO NI PESA HATA MKIJAZANA KAMA NDIZI SHAURI ZENU NA MAAJALI YAKITOKEA POLISI NI WAKUMTAFUTA NDIO HAPO NILIPO ZIDI KUCHUKIA KUWA BONGO HAKUNA MABADILIKO MAGARI MENGI MIBOVU MABARABARA MABOVU NA WATANZANIA SERIKALI SASA IYANZE KUFIKIRIA KUONGEZA MABARABARA MJINI DAR MJI WA DAR UNACHAFULIWA NA GASI YA MAGARI YAANI MOSHI WA MAGARI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...