President Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a debate on improving agriculture production to boost food Security during the World Economic forum in last night in Davos . Left is Ms. Ellen Kullman Chair and CEO of of the US based DuPont company and right is Microsoft Founder and Chairman Bill Gates.

President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the the Microsoft founder and Chaiman of the Bill and Melinda Gates Foundation, Bill Gates shortly after participating in a debate on improving Food Security held in at Davos Congress Hall on the last day of the session. Microsoft supports the ICT college of the Dodoma University among other projects
President Jakaya Mrisho Kikwete(right) in conmversation with Vietnam Prime Minister Nguyen Tan Dung(centre) and the chariman of the New Delhi Television Roy Prannoy(left) who was also the moderator during the debate on Global Food Security held at Davos Congress Hall.
President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with World Trade Organisation WTO Director General Pascal Lammy at the Davos Congress hall in Davos last night during the last session of the World Economic Forum held in Davos Switzerland. Photo by Freddy Maro.

Na Mwandishi Maalum, Davos, Uswisi

ILO YAISIFU TANZANIA
KWA UONGOZI BORA NA IMARA
Shirika la Kazi Duniani (ILO) limesema kuwa Tanzania ni mfano mzuri wa nchi yenye uongozi bora na imara, hali iliyoiwezesha nchi hiyo kutoyumbishwa kupita kiasi na msukosuko wa karibuni wa uchumi duniani.

Aidha, Shirika hilo limeipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufanikiwa kutengenezaji ajira zaidi ya milioni katika miaka minne ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Bwana Juan Somavia amesema kuwa ukweli kwamba Tanzania haikuyumba kupita kiasi kutokana na msukosuko wa uchumi dunia ni ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa nchi inasonga mbele kwenye mikono salama.

Bwana Somavia ametoa sifa hizo kwa Tanzania wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Jumamosi, Januari 30, 2010, kwenye Hoteli ya Arabella Sheraton Woodhuus, Davos, Uswisi, ambako Rais Kikwete amefikia.

Rais Kikwete pamoja na Bwana Somavia, walikuwa mjini Davos kuhudhuria Mkutano wa 40 wa Taasisi ya Uchumi Duniani ya World Economic Forum (WEF), ambao unamalizika kesho, Jumapili, Januari 31, 2010. Mkutano huo umehudhuriwa na mamia kwa mamia ya wajumbe kutoka sehemu mbali mbali duniani wakiwamo viongozi kutoka zaidi ya nchi 30.

Bwana Somavia amemwambia Rais Kikwete kwenye mazungumzo hayo: “Yako, Mheshimiwa Rais, ni nchi inayosonga mbele, ikiwa haina jambo la kuiyumbisha. Ni nchi iliko kwenye mikono iliyotulia, yenye uongozi bora na imara, ukweli ambao ulijidhihirisha wakati wa msukosuko wa uchumi duniani.”
Viongozi hao wawili wamejadili msukosuko wa uchumi duniani na athari za msukosuko huo kwa nchi mbali mbali na hasa zile zinazoendelea. Msukosuko huo ulilipuka kati ya Oktoba na Novemba, mwaka juzi, 2008, na athari zake zinaendelea kuisumbua dunia hadi leo.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa mfumo wa uchumi wa soko, pamoja na manufaa yake makubwa duniani, bado unahitaji aina nzuri ya kuudhibiti mfumo huo, ili kuzuia dunia isiweze kuingia katika matatizo makubwa zaidi ya uchumi.

Kuhusu ajira katika Tanzania, Bwana Somavia ameipongeza Serikali ya Rais Kikwete kwa kuweza kutengeneza ajira zaidi ya milioni moja, kama Chama cha Mapinduzi (CCM) kilivyoahidi katika Ilani ya Uchaguzi wa 2005.

Hata hivyo, Rais Kikwete amemwambia Bwana Somavia kuwa ni bahati mbaya kuwa msukosuko wa uchumi duniani umeifanya Tanzania kupoteza nafasi 47,000 za ajira, lakini akaongeza kuwa ni dhahiri kuwa zipo ajira zaidi zilizojitokeza hasa katika sekta isiyokuwa rasmi katika kipindi hicho cha msukosuko duniani.

Mbali na kukutana na Bwana Somavia, Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa WEF, Profesa Schwab.

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Davos cha Congress Centre ambako shughuli za WEF zinaendelea, viongozi hao wamejadili, miongoni mwa mambo mengine, maandalizi ya Mkutano wa WEF-Africa ulipangwa kufanyika mjini Dar Es Salaam mwanzoni mwa Mei, mwaka huu, 2010.

Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa mkutano huo wa WEF-Africa kufanyika nje ya Jiji la Cape Town la Afrika Kusini ambako miaka yote mkutano huo umefanyika.

Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani la World Trade Organisation (WTO) kwenye Congress Centre.

Wakati huo huo, Rais Kikwete anatarajiwa kuondoka mjini Davos asubuhi mapema ya leo, Jumapili, Januari 31, 2010, kwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Mwaka huu wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo, Jumamosi, Januari 30, 2010 mjini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. natumaini kikwete hukutuangusha uliweza kutoa hoja zenye nguvu. Kiingereza siyo issue unaweza kutumia kiswahili pia mkuu.

    ReplyDelete
  2. Nimeangalia moja ya mjadala na nimeona wengi wanaongea kuhusu infrastructures, energy, nafikiri wote wanaona vitu vya kupewa kipaumbele lakini Tanzania ni tofauti vipaumbele viko kwenye magari ya viongozi na nyumba za viongozi.

    ReplyDelete
  3. Hawa jamaa wakishake hands na leader from a poor country wanapata credit uko kwao.... for reference lakini after that hakuna kinachofanyika believew me, toka viongozi wetu waanze kutembeza bakuli takribani miaka imesha fika 47 lakini njaa iko pale pale...



    mdau ujerumani

    ReplyDelete
  4. mimi namkubali JK kwa kazi kubwa anayofanya angalia watu anaokutana nawo katika mkutano huo... ni watu wazito wa dunia hii, baba wa watu kweli anafanya kazi sasa kazi ipo hapa sasa waziri wa miundo mbinu yuko wapi kwnye mkutano kama huo? anaenda na waziri wa ulizi wakati ulinzi tunao safi kabisa, anglia waziri wa kilimo yupo tu anapiga mahesabu yake. JK ana hitaji vijana wa uchumi kwenda nao watu ambao wataongea kama yeye. kweli bado ana kazi kubwa kuchagua watu kama mawaziri

    ReplyDelete
  5. Huu ujinga wa kufikiria Kikwete hazungumzi kiingereza kizuri ni upumbavu usio kifani. Jamaa anazungumza vizuri na ana sense of humor. Nilikuwa natazama TV program ya Balozi Andrew Young hapa Marekani ambapo alikuwa akimuhoji Kikwete huko Tanzania kwenye mbuga za wanyama Kikwete alikuwa akieleza hali ya utalii na jinsi Kenya wanavyotumia ujanja kujitangaza kwa kutumia rasilimali za Tanzania. Pia Raisi wa zamani wa Marekani Jimmy Carter pia alichangia kwa hilo la Kenya kutupiga chenga. Lakini akaongezea kuwa Tanzania ndio nchi yenye potential kubwa sana ya maendeleo. Kwa ufupi Kikwete ni Raisi aliyetulia anazungumza vizuri hicho kiingereza mnacho fikiri ndiyo kitu kikubwa. Mimi hapa kiingereza ndiyo maisha yangu ya kila siku kuanzia asubuhi mpaka nalala, nakuhakikishie Kikwete hana tatizo na lugha na ndiyo maan a anakutana na viongozi wengi kwani anajua mbinu za mawasiliano ya lugha.

    Mdau USA.

    ReplyDelete
  6. Looking so good for a poor country leader..its sad that magufuli and kawambwa could not make it..but why include them while we can have masha to speak smoothly and make us look and sound good...i guess u gotta speak in american accent to impress the bigwigs.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...