Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia utekelezaji wa Majukumu ya Mpango wa Tasnia ya Uziduaji (EITI -Extractive Industries Transparency Initiative ) Jaji Mstaafu Mark Bomani (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Kamati yake ya EITI baada ya kutambulishwa na Naibu Waziri wa Nashati na Madini Adam Malima (kulia) kwa wajumbe wa kamati hiyo jijini leo.. Picha na Mwanakombo Jumaa, habari na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Raisi Jakaya Kikwete amemteua Jaji Mstaafu Mark Bomani kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya kusimamia Utekelezaji wa Majukumu ya Mpango wa Tasnia ya Uziduaji (Executive Industries Transparency Initiative – EITI).

Akimtambulisha Mwenyekiti huyo kwa wajumbe katika kikao cha pili cha Kamati hiyo, kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Adam Malima amesema, Jaji mstaafu Mark Bomani ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na mchapa kazi hivyo uteuzi wa Rais umemfaa na utaleta tija katika utendaji kazi hasa katika usimamizi na matumizi mazuri ya madini.

“Hapa Tanzania karibu kila mtu anamfahamu Jaji mstaafu Mark Bomani. Hii imetokana ufanyaji kazi wake ulio makini ulionmfanya Mhe. Rais kumteua, kwani anajua ni mtu anayejituma katika kazi,” Amesisitiza Waziri Malima.

Wakati huo huo, Jaji Bomani amesema, ameupokea uteuzi huo kwa furaha na ameahidi kufanya kazi kwa bidii katika kuishauri serikali juu ya matumizi mazuri ya madini ili kila mwananchi anufaike na rasilimali hiyo.

Kamati ya uziduaji ilianzishwa rasmi mwaka 2008 na kuzinduliwa mwaka jana mwishoni ikiwa na majukumu ya kusimamia na kutoa ushauri kwa serikali namna ya kutumia vizuri madini hayo ili yaweze kumnufaisha Mtanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Rais Mh. Kikwete, safi sana kwa hili na penye kupongezwa tunahitaji kukupongeza.
    Sasa basi katika mfuatano huo huo. Tafuta Katibu mkuu na au kamishina wa madini mtu strong asiye na mawaa na mzamivu katika eneo la madini.

    Ili kamati hii ifanye kazi nzuri, LAZIMA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA WAWE WENYE UWEZO NA WASIO WABADHILIFU

    ReplyDelete
  2. Mwenyekiti tumemjua, wajumbe vipi? Tuambiwe wajumbe wa hiyo kamati ni akina nani, na nani amewateua au wamepatikana vipi?????

    ReplyDelete
  3. Huh?

    Ni nini hii tume? What does this mean "Kamati ya kusimamia Utekelezaji wa Majukumu ya Mpango wa Tasnia ya Uziduaji (Executive Industries Transparency Initiative – EITI)"??????

    ReplyDelete
  4. Mtu aliyechaguliwa ana records nzuri kiutendaji na hilo linaeleweka...lakini hamuoni kwamba umri wake umekwenda sana? Mbona wapo vijana wengi wenye shule nzuri na wenye kuchapa kazi?? Hata ankal hapo anaweza....with light touch!

    ReplyDelete
  5. Michuzi hivi kwanini unanibani comments zangu kila siku unaniboa sana.

    Mimi nashungaaaaa mbona viongozi kila siku ni wale wale kundi hilo hilo la watu????? akitoka hapa anapelekwa hapa vipi jamani, kwani hakuna watu wenye akili zaidi ya hao hao, huyu baba ni mzee, ni tajiri, hana watu tegemezi, amechokaa, mnampaje tena uongozi yeye?? apewe mwenngine bwana.
    Vijana watapata wapi experience kama hawapewi nafasi nashangaa.
    Siufagilii kabisa uchaguzi huu, hapana sikubali.

    Mtoto wa Mkulima

    ReplyDelete
  6. you know sometimes hata nachoka kuongea haya maswala vijana tupo wapi? au mheshimiwa hatuoni labda tupeleke majina yetu ikulu atujue.

    ReplyDelete
  7. Kila siku ni wastaafu wanaoteuliwa.....watastaafu lini kama mnaendelea kuwapa majukumu?

    ReplyDelete
  8. Tanzania kwa tume, tumejaariwa. Huyu mzee si alikuwa mwenyekiti wa kamati ya madini ya kurekebisha na kupitia mikataba pamoja na akina Zitto. Cha kushangaza hata ile ripoti waliyoiandaa haijatekelezwa wala kujadiliwa amepewa tena ulaji mwingine. Tunatumia hela nyingi sn kuunda hizi tume lakini matokeo yake inayeyuka na unamwona mwenyekiti wa kamati amepewa kamati ingine. Huo ufanisi utatoka wapi? Na huyu mzee jamani amechoka toka enzi zile mpk leo ni yeye, hakuna watu wengine? na mbali na hilo yupo kwenye kamati kibao. Cha kushangaza na yeye hatakai anasema ameupokea uteuzi huo kwa mikono miwili. Sisi vijana tutajifunza lini hizo kazi? Ukienda kuomba kazi unaambiwa huna exeperience jamani experience itatoka wapi kama wastaafu wanakaba kila kona?

    Kaka Michuzi, hivi ile ripoti ya madini iliyotakana na kamati ya akina Bomani, Zitto na wajumbe wengine ya kumshauri rahisi kuhusu masuala ya madini inapatikana wapi? au nini kimetekelezwa kutokana na hilo? Nimeona juzi mheshimiwa alikuwa na wakuu wa Barrick, kaazi kweli kweli na tume zisizoisha.

    Mdau Brussels- Belgium

    ReplyDelete
  9. we anko sijui ankal hii tabia yako ya kubanabana msg za watu ukome watu tunalipia hela ma cafe na tunalipia bill za internet unaboa sana au kwa vile blog ya jamii iko juu ndo unandengua??? acha hizo kama comment haina matusi iache iende hewani hata mange u turn anakushinda ukome kubana meseji zetu na hatuami ng'oo tutakabana humuhumu
    mkereketwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...