Jerry Muro akiingia sentro leo
Akiwa amezingirwa na makachero wa polisi, mwandishi wa TBC Jerry Muro akiwasiliana na ndugu na jamaa baada ya kufikishwa kituo cha kati jijini Dar leo akituhumiwa kupokewa rushwa toka kwa mhasibu mkuu wa zamani wa wilaya ya Bagamoyo, Bw. Michael Wage

Jerry Muro akihojiwa na waandishi wenzie kituo kikuu cha polisi jijini Dar leo ambako anashikiliwa kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi milioni 10. Jerry Muro akijiandaa kukabidhi vitu vyake
kwa makachero wa polisi baada ya kufikishwa sentro leo
JERRY MURO MATATANI

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Jerry Muro (pichani juu kulia) kwa tuhuma za kudai fedha kwa njia ya vitisho.

Muro anadaiwa kumtisha aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo Michael Wage ambaye hivi karibuni alisimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa tuhuma za ubadhilifu pamoja na viongozi wengine wa Halmahauri ya Wilaya Bagamoyo.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Suleimani Kova alikiri jeshi lake kumshikilia Muro na kuwa alimtishia Wage kuwa yeye ni Ofisa wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kumtaka atoe fedha Sh milioni 10.

“Polisi inamhoji Muro dhidi ya tuhuma hizo na mahojiano yakikamilika taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na maelezo zaidi nitayatoa kesho wakati wa mazungumzo yangu na waandishi wa habari” Kova alisema.

Bingwa huyo wa Tuzo za Uandishi wa Habari 2009 Tanzania alionekana akiwa sentro na mkononi ameshikilia bahasha tatu pamoja na kamera ya Video.

Alipohojiwa na wenzie juu ya kuhusika na tuhuma hizo alikana na kudai kushangazwa kuwekwa chini ya ulinzi kwa madai kuwa alipigiwa simu na mtu kupewa taarifa kuwa kuna kazi katika Hoteli ya City Garden.

“Kaka nilitaarifiwa tu kama ujuavyo kazi zetu kuwa kuna kazi City Garden niakaamua kwenda. Lakini baada ya kufika tu nilishangaa nawekwa chini ya ulinzi na askari kanzu ambao ndiyo walionifikisha kituoni hapa bila ya kunitajia kosa lanmgu. ” alilonga Muro.

Kwa upande wake Wage alidai kuwa mtuhumiwa anatumiwa na watu wengine ambapo juzi alimpandisha katika gari lake na kumfunga pingu kisha kumtaka atoe Sh milioni 10 na kwa kuthibitisha kuwa alikuwa ndani ya gari hilo alidai kuacha miwani yake yenye mikanda myeusi.

Polisi ilipomhoji Muro kama anazo pingu alikiri kumiliki pingu pamoja na bastola ambapo baada upekuzi katika gari lake lenye namba za usajili T 545 BEH polisi walikuta pingu hizo pamoja miwani iliyosemwa na mlalamikaji.

Muro alishinda tuzo ya Mwandishi bora wa mwaka kupitia vipindi vyake vya Televisheni vya "Usiku wa Habari" vinavyorushwa katika kituo cha TBC1 kila siku na kabla ya kuhamia hapo alikuwa kituo cha ITV na aliendesha kipindi cha "Ripoti Maalum".

Miongoni mwa mambo aliyokuwa akirusha katika vipindi hivyo ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na ukiukwaji wa sheria.

Polisi wamekuwa ni waathirika wakuu katika vipindi hivyo kwani mara mbili amewatoa Polisi Usalama barabarani wakiomba na kupokea rushwa hadharani kutoka kwa madereva wa malori na mabasi ya mikoani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 70 mpaka sasa

  1. Watanzania mnaoishi nje, hasa vijana bado mnaendekeza fikra za kurudi Bongo? Ni Swali tu.

    ReplyDelete
  2. jamani hiyo sababu ya jery kukamatwa mbona bado haijaniingia akilini?..kwa uelewa wangu c rahis jery kujibadilishia kazi na kujipa madaraka ya takukuru...hasa ikizingatiwa kwamba yeye ni maarufu na watu wengi wanamfahamu hasa kupitia televisheni...kama ni kweli jery umechemsha but it seems imepikwa!!hebu wahusika waifuatilie kwa karibu bana maana jamaa wanataka kumlipizia..

    ReplyDelete
  3. POLE SANA KAKA TUNAKUOMBEA KWA MUNGU!

    ReplyDelete
  4. kaka michuzi habari hii inashangaza sana sana, yani nakuwa kama siaminiamini vile. Hebu tunaomba utusaidie sie tulioko huku mbali kupata ukweli wa mambo. Ni kweli huyu Jelly Mulo alikwenda bagamoyo na Pingu na Bastola, na kudanganya kuwa yeye ni afisa wa PCCB, na kutishia kwa kutoa pingu ,na kwamba hivyo vitu vimekutwa kwenye gari lake?? hii habari inashangaza kwa kweli. Ina maana jelly muro ni mtu wa aina hiyo kweli au amefikia huko au kachezewa mchezo gani?? kwa maana kama ni kweli yeye mwenyewe alitoa pingu basi inashangaza sana. hebu tusaidie mzeee aminia mwana najua kesho utatuijia na Ukweli kamili wa mambo. very anxious to know about this n can't wait
    ahsante
    Mdau wa P&T

    ReplyDelete
  5. Mkata issueJanuary 31, 2010

    Kabla jogoo hajawika yaliyofikirika yanatokea!

    Sasa ukute hiyo bastola haikusajiriwa wala hana nyaraka za kuimiliki; muziki wa hapo haujulikani!!

    Halafu tena na pingu za Polisi au za bandia za watoto kuchezea?, mmh!! jamani kwani Takukuru huwa nao wana pingu?

    Jamani hivi kweli Jerry alifanya hayo?
    Ngoja tusubiri kupata ukweli maana hapo tatuhumiwa makosa ya jinai yasiyopungua manne kama ni kweli.

    1. Kujipachika utumishi wa TAKUKURU
    2. kuomba rushwa
    3. Kumtishia raia kwa pingu na bastora (kama maelezo ya huyo Mhasibu yatakuwa hivyo)
    4. Kumiliki pingu na bastora (kama hana kibali cha kuwa nayo)
    5. Kubeba bastora na kuitumia kutishia raia (kama maelezo ya huyo Mhaasibu yatakuwa hivyo)

    Halafu huko TBC itaonekana kama ametumia kazi yake ya Utangazaji kujificha kama mpiganaji dhidi ya rushwa ili yeye aendeleze kuomba rushwa. Hivyo atakuwa amekiuka maadili ya kazi yake na hivyo kibarua kuota mizizi.

    Jamani nauliza tena maana sijaamini kama ni kweli hayo yamefanywa na Jerry Muro tuliyesema apewe tuzo kwa kazi yake ya kishujaa ya kuumbua waomba rushwa!

    ReplyDelete
  6. Kwani hapa Dar Pingu zinauzwa wapi?

    ReplyDelete
  7. Gari ya huyu Jerry ni Vitara ama? maana zinafunguliwa bila tatizo hapa mjini. Afteral, almost all cars wakiamua kufungua wanafungua tu. They are in the bussiness with catching the thiefs....they must know better.

    Somebody has planted evidence to this guy. And wasamaria wema you must do something to deal with ths otherwise what he was trying to change 'behavioural change will be dumped in vain!'
    otherwise watu tunaowaona ni ndivyo sivyo vibaya kiasi hiki?

    Jerry find yourself a gud lawyer.
    Pitty!!
    And you shouldnt doubt him a bit. With his kind of reporting he cant be that stupid to act as a PCCB agent!.
    Bad move for the these guys; they were to be better in that otherwise, hu! hawa wezi hawataisha maana mmh they might be smarter than planting such not even close unbeliavable evidence.

    ReplyDelete
  8. Cha msingi kila kilichokuwep kitajitokeza tu kama wamegnayia mchongo au kama jamaa kachemshwa mwenyewe kwa kujiona alipowaumbua wale askari akaona atumie advantage hii kwa kuwatisha watu kama atawauumbua au wampe rusha.....hayao yote yarajitokeza na ukwlei tutauona.

    nimefurahishwa na mfau hapo juu wa 11:30 eti kwani hapa Dar pingu zinauzwa wapi? hii kali inamaana kama anazo basi kazipata huko huko kwa hao maaskari duh ebana eee!!!

    ReplyDelete
  9. HIVI SHERIA ZA POLICE NI LINI ZITABADILISHWA?
    KWA KWELI SIYO HAKI UNAMKAMATA MTU BILA YA KUMWAMBIA KWANINI YUPO CHINI YA ULINZI!!!!!!!!????
    NI HAKI YA MTU KUAMBIWA KILICHO MKAMATISHA THEN MAELEZO ZAIDI ATAYAPATA KITUONI LAKINI.
    TAFADHALI POLICE WEKENI MAMBO YENU WAZI KWA FAIDA YA MLIPA KODI bytheway yeye ndo anayewalipa mshahara.
    thanx

    ReplyDelete
  10. mada ya ziada :WANAHABARI NA RUSHWA!!!!
    mimi ninachojuwa bongo wanahabari ni watu wanaodai rushwa kuliko mtu yeyote , haya ninayoyasema ni kweli kabisa, ukiwaita kwenye press conferance yoyote lazima uwalipe au habari yako haitatolewa kwenye vyombo vya habari , kuanzia wanndishi hadi hao tv & radio prensenter ,kwenye redio ndiyo usiseme kama huna laki 2 kwa kila mtangazaji wa redio nyimbo yako haitasikika redioni , tena walivyokuwa hawana maadili hudai kama vile haki yao.
    siwezi kusema kitu kuhusu bw jerry inawezekana kuwa ni fitina au naye yumo :bongo kila kitu inawezekana

    ReplyDelete
  11. Utata mtupu wala haimake sense.wamempakazia tu

    ReplyDelete
  12. Wausika wa usalama,jamani kwakweli inabidi tuwe makini sana hasa kwa swala la haki, mambo aya ndiyo yanafanya vijana washindwe kurudi nyumbani TZ, tunacho taka ni aki itendeke kwa kijana uyu(Jerry)

    ReplyDelete
  13. Elimu ni kitu muhimu. Huu mpango wa ku "kumframe" Jerry Haukwenda shule. Unaonekana wazi ni mpango wa polisi wetu wenye darasa dogo! Lakini Saidi Mwema kasoma, yeye kweli anakubali kuhusishwa na "cheap games" please give us a break!!! Mmetundaganye kwa mengi mno sasa mnatudanganya kama watoto wa shule za vidudu

    ReplyDelete
  14. mbona kuna utata kwenye maelezo ya polisi? taarifa za mwanzo zinasema kwamba amekamatwa akipokea sh mill. 10 kabla ya mtego aliowekewa haujafyatuka, na sasa tunaambiwa kuwa ni yeye binafsi aliekwenda kwa kwa huyo Wage under false pretences! kwa madhumuni ya kupata pesa. sasa hii mbona haiendani na mtu aliyewekewa mtego? au kwa mtego wanamaanisha survaillance?... au vitu vilivyokutwa kwenye gari lake?

    ReplyDelete
  15. MICHUZIIIIIIIIII TUWEKEE MANUUU TULIVYOFANYA KWELI EMIRATE WEWEEEEE MAN FOREVER HE HEE HEEE MAN UUUU OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!

    ReplyDelete
  16. eh! eh! eh! we mkata issue hapo juu sio BASTORA!! ni bastola

    ReplyDelete
  17. Jinsi ninavyofahamu

    Vijana wengi wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari vya serikali ni Intellegence Agent. Hawa wanafanya kazi na vyombo vya usalama ambavyo polisi hawavijui. Kwahiyo Jerry anaweza kuwa na kofia mbili kazini. Anaweza kuwa Mtangazaji na Intelligent.
    Kwahiyo inawezekana alikuwa na story ya Bagamoyo na akawakazini kwa kutumia Kofia nyingine huyu Mhasibu akajua anamdanganya, akamwitia Polisi. Kuna kitu kilichowaunganisha hawa watu wawili. Tuangalie simu na mawasiliano yao..Kabla ya yote!

    Assumption ya pili...
    Huyu Jamaaa ametegeshewa na kukamatwa kwa mtego ambao yeye hakuujua na hivi vi-evidence wanavyokuja navyo ni danganya toto.

    Backfire!!!......
    Hawa waliotega huu mtego kama hawakuuweka vizuri, unaweza kubackfire na watu wakapoteza kazi kama hawana akili nzuri.

    Confusion....
    Bado sijaona wala kuelewa ipasavyo ni kwanini huyu jamaa alikamatwa. Kamanda wa polisi hawezi kukaa na habari 24hrs juu ya mtuhumiwa, kwasababu ili mtuhumiwa akamatwe lazima tuwe na sababu za kutosha kusema kwa public juu ya makosa ya mtuhumiwa,kama kamanda hana cha kusema sasa hivi, basi Jerry hakutakiwa kuwa kituo cha polisi. Uchunguzi hauwezi kufanya wakati mtuhumiwa amekatwa bila ya kuwa na strong evidence za kumkata.

    Kamanda wa Polisi Mkoa!
    Huu mtego mchafu unaweza kuwa ni kitu ambacho wewe hakuujui, fuata sheri na ukweli juu ya swala bila kuogopa mkubwa ndio itakuwa usalama wako. Kama wanayoandika wanahabari kuhusu jinsi huyu jamaa alivyokamatwa ni kweli, basi kuwa mwangalifu sana ndg yangu.

    ReplyDelete
  18. Nakubaliana na aliyepost Mon Feb 01, 01:23:00 AM kuwa bongo kila kitu kinawezekana, if you know what s/he meant. Yasije yakawa yale yale ya Adam Mwaibabile?

    ReplyDelete
  19. There is a big man behind this.Muro is just a minor in the "RUSHWA" field. If We are real against "RUSHWA". lets start with the big fish.Fellow TZN lets wake up.

    ReplyDelete
  20. Jamani pingu na bastola vinazwa pale Tanganyika Arms. Kwa bastola baada ya kununua utatakiwa kupata kibali kabla ya kukabidhiwa lakini pingu nenda hata wewe leo utauziwa, hazihitaji kibali.
    Suala la miwani kukutwa katika gari siyo issue kwa vile police can get into your car if they want to. Ila nafikiri kuna mtu yuko karibu na Jerry akawatonya polisi kuwa jamaa anatembea na pingu na bastola ktk gari; au walifngua gari lake (kwa kutumia police master key) wakitaka kumsakizia kitu kingine (kama bangi au bunduki ya wizi) wakauta pingu then waka-change plan baada ya kukuta pingu na hivyo wakaweka miwani na zua walilolizua.
    Binafsi siamini kwa umaarufu wa Jerry (kwa sababu ya kuonekana ktk TV) anaweza kuthubutu kumdanganya mtu kuwa yeye ni ofisa wa TAKUKURU. Na kama Jerry angekuwa mjinga kwa kiasi hicho,nafikiri asingefika hapo alipo. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  21. CENTRAL POLICE STATION = KITUO CHA POLISI CHA KATI

    CENTRAL BANK = BENKI YA KATI?

    ReplyDelete
  22. "Polisi ilipomhoji Muro kama anazo pingu alikiri kumiliki pingu pamoja na bastola ambapo baada upekuzi katika gari lake lenye namba za usajili T 545 BEH polisi walikuta pingu hizo pamoja miwani iliyosemwa na mlalamikaji."

    Haya ndio mambo ya bongo!! Anamiliki pingu yeye kama nani?? Waandishi wa habari tz njaa tupu, wengi wao wamenunuliwa, na wanazalilisha kazi ya uandishi wa habari..

    ReplyDelete
  23. za mwizi ni arobaini

    ReplyDelete
  24. SOMENI VIZURI MAELEZO, JERRY ANAKIRI YEYE MWENYEWE KUMILIKI PINGU NA BASTOLA BADO BAADHI YENU MNADAI KAWEKEWA! DARASA BOVU SHULE MBOVU.

    ReplyDelete
  25. JERRY ANASTAHILI KUNYANG'ANYWA TUZO, TUJIFUNZE TOKA NJE.

    ReplyDelete
  26. Jerry should find a good lawyer, but certain things are so doubtful, why should he own handcuffs ? he admitted they are his? what are they for? the person who accused him, is not one of our millitia but rather a tossed public servant..i smell something, newsmen likes bribe more that anything that walks faster, if you want them to come and cover your event, which is news anyways and its their job, they will demand 'nauli' this is not receipted and no one condems it..we are all human beings subject to corruption and living in a corrupt country where even when you get excellent service you deserve you always feel bad if you leave without 'thanking' the provider who is just doing his job; i think the problem is deeper than that, if a traffic police demands rushwa; you have 2 options, pay a small amount and get away with it..or pay full amount for the misdeed at the traffic police and get a receipt..good law abiding citizens always do this....so ahem..rushwa stops when we want it to stop..

    ReplyDelete
  27. ...tunaweza kujenga theory nyingi kuhusu hili lakini pamoja na yote miwani,pingu na bastola vilivyoelezwa na mlalamikaji vimekutwa kwenye gari yake.kama walaipigiana simu basi makampuni ya simu yatasaidia kutoa ufafanuzi pia kwa nambari alaiyotumia.

    Na kama vitu hivyo vimepandikzwa katika gari yake muro atajua ni wakati gani.

    pamoja na yote ni jambo la kusubiri tu ndio hali ilivyo.ushahidi huo upo.
    Pamoja na y

    ReplyDelete
  28. wewe mzungu unayesema eti wamepandikiza pingu hizo kwa sababu eti gari lolote linaweza kufunguliwa soma habari yote. Aliukizwa kama anapingu akasema ndio na wakazikuta sasa hii yako wewe umeitoa wapi?

    ReplyDelete
  29. Ohhhhhh My Goddddd!!!!!!! yaani sipati picha.
    Jamani hivi nchi ina matatizo gani??? ila sitaki kuamini kuwa Jerry alikuwa anaomba rushwa, of course najuwa kuwa waandishi wa habari bila rushwa hawafanyi kazi yako. Yaani tumekwisha majaji wapokea rushwa, mapolisi wapokea rushwa, madakitari wapokea rushwa, manesi wapokea rushwa, waandishi wa habari wapokea rushwa haya Watanzania wenzangu niambieni tukimbilie wapi??!!!!

    Tumekwishaaaa!!!!

    ReplyDelete
  30. Jamani nina ndugu yangu wa damu ni mwandishi lakini watu walikuwa wanasema sema nje kuwa ni afisa wa usalama na ss tukawa tunawashangaa coz tunamjua vema ndugu yetu. lakini siku ya siku binafsi nilithibitisha kuwa ni afisa wa usalama kwa mambo yake pia anamiliki silaha ambayo anaificha sanaa na anaweza kukurupuka akapotea kama mwezi msiwe na uhakika alipo na akiongea na simu maongezi yake ni ya kiusalama kabisa pia mnaweza kwenda sehemu akatoa ishara fulani na kusema tuondoke hapa sio salama kwa kweli maisha yake ni utata na hapendi watu wajue anapoishi wala namba yake na nahamahama mno. inawezekana kwa asilimia 90 (maoni yangu) Jerry ni afisa usalama hawezi kukubali haraka kwamba ana silaha endapo anajua haimiliki kihalali lets wait and see.

    ReplyDelete
  31. Bwana Yesu namuombea huyu kijana na umsaidie aweze shinda yote yalomzunguka maana ni binadamu na pia hii VITA aloiazisha ambayo ni "ulaji"wa watu...amen

    niko nyuma siku nikikuona naomba nikusalimie japo kw amkono tu.hope hauna mapozi

    Tz kuna visa mara muafaka,mara meremeta,EPA,richmond,zombe,babu seya,per diems nk nk

    ReplyDelete
  32. Jamani msisahau kuwa huyu ni MEKU ati mchana fundi viatu usiku 'somebody else'
    Kwa wanaopinga kuwa hawezi kufanya hivyo kwa umaarufu wake nawashangaa hawajui kwamba watu bongo wanatumia umaarufu kujinufaisha, who is he by the way, he is just a human being, hebu rejeeni kwa watu kama Alhaj Mintanga aliyekuwa rais wa ngumi na mabondia wake,somebody Masanja aliyewahi kuwa katibu mkuu simba ambaye sasa anachezea kifungo kirefu china kwa kukutwa na madawa ya kulevya,aliyekuwa mmiliki wa bendi ya extra bongo ambaye alikufa kwenye tukio la ujambazi akiwa ni mmoja wa majambazi. Hiyo ndiyo stahili ya bongo ili utoke bongo lazima u-take risk na inakuwa rahisi zaidi unapokuwa maarufu,msione watu wanamaisha mazuri bongo wana mambo yao,iisue ya Bagamoyo inajulikana ni rahisi kwa mwandishi kama jerry kuitumia kwa lengo la kujinufaisha. Mkurugenzi aliyefukuzwa alikuwa anawatumia waandishi kumchafua Mkuu wake wa wilaya matokeo yake yeye na timu yake ndio wameumbuka wakiwa bado na machungu dogo anataka kwenda kuvuta kitu kidogo noma.

    ReplyDelete
  33. MIE SIAMINI KABISAAAAAA, HAO MAPOLISI WAMEONA SASA WANAMULIKWA SANA NA JERRY MAANA HATA KUOMBA RUSHWA WANASHINDWA KAMA ALIVYOWARUSHA MATRAFIK WA NJOMBE/IRINGA/MBEYA KWENYE TBC... JAMANI WAANDISHI WA HABARI JITOKEZENI KUFANYA KAZI KAMA JERRY ILI MUTUOKOE JAMANI RUSHWA INANUKA BONGO. JERRY DONT WORRY YOU WILL BE OKAY SOON GOD IS WITH YOU.

    ReplyDelete
  34. Amezidi umbea na yeye...eeeh!!

    ReplyDelete
  35. i think its a publicity stunt on jerry muro's side..this kind of publicty will make heads turn and him more popular as reporter..check out the distinguished reporters around the world they always have cases.

    on the second side might be someone out to get him as in Tz there is nothing as freedom of speech or exposure of the wrong doers so you should have laid low mr reporter.

    ReplyDelete
  36. Duh! polisi mmekwisha kama ni mchongo mmeingia choo cha kike kama wanavyosema huko mtaani.jerry mmemkamata na rushwa je tangu lini Kova kaanzisha kitengo cha kupambana na rushwa? pili mbona watu wa pcb hawakuwepo mlipomkamata? polisi acheni uendawazimu. kukamatwa kwa jerry siyo rushwa wala nini hii ni chuki binafsi ya wapokea rushwa na mafisadi ila najua ukweli utajulikana tu kwani kila kinachofanyika gizani kitajulikana kwenye mwanga .kaka yangu jerry tuko pamoja wapokea rushwa lazima tuzaae nao hata kama mtatutisha hatishiwii mtu hapa kazi mtindo mmoja .hongera kova kwa kuanzisha kitengo cha kupambana na rushwa

    ReplyDelete
  37. Waandishi wa habari wamezidi kwa kuomba rushwa. Ukitaka kujua ni kwa kiasi gani huomba rushwa waulize wabunge na wagombea ubunge.
    Wengi wa waandishi wa habari ni wanafiki, wailani rushwa huku wakiwa ndiyo vinara.

    ReplyDelete
  38. WADAU...jerry kuown pingu au bastola wala sishangai kwanza kwa level ya ujambazi bongo sasa hivi i should say it is essential mtu kuown bastola for their own safety! kumbuka jerry baada ya kuwa mfichua uovu lazima kuna watu wanamtafuta sana wammalize so mie sishangai...i dont think jerry angefanya kitu cha kijinga namna hii kujifanya ofisa wa TAKUKURU ilhali kila mtu anajua ni mwandishi wa habari..huyo mzee wa bagamoyo naona mambo yake yalivodunda akatafuta mtu wa kumtolea tu mistressi yake..

    ReplyDelete
  39. FREE JERRY MUROOOOOOOO!

    ReplyDelete
  40. Duh!!its very sad to hear that,kwani labda polisi wanafanyaje kazi?kwasababu kwa jinsi ilivyo inaoanekan kama polisi walikuwa wanajua kinachoendelea kuhusu huyu Jerry na huyo mhasibu sasa cha kujiuliza hapo je ni nani aliwaambia au ndio walikuwa wanamfuatilia kwa kila jambo kuanzia simu zake na kila aina ya mawasiliano yake ne je kwanini jeshi la polisi limfuatilie Jerry tuwakati kuna matukio kibao ya uhalifu hayajapatiwa majibu watu kibao wameuwawa huko ukerewe watuhumiwa hawajapatikana, pesa nyingi zimeibiwa kwenye mabenki watuhumiwa hawajapatikana, majambazi yameuwa juzi juzi tu kule kimara lakini watuhumiwa hawajapatikana lakini maskini Jerry Muro kalipoti tu uhalifu wa polisi hazijapita hata wiki tatu leo hii kijana kakutwa akipokea rushwa!!!!Jeshi la polisi letu lingekuwa linafanya kazi na kutoa majibu ya haraka namna hii basi nafikiri nchi yetu isingekuwa na tishio kubwa la uhalifu mpaka kukosa imani kwa wawekezaji wetu!!
    Ni imani yangu kuwa haki itatendeka kwa Jerry na ukweli bila kutokea mtu wa kumfunga paka kengele basi Jerry na wanaopigania haki za wanyonge kama Jerry watapotea na kila mtu atajipigania mwenyewe, pole Jerry amini mungu yupo na atakusaidia inshalllah utashinda vita

    ReplyDelete
  41. Msikurupuke kuchangia mada kabla hamjasoma..Jerry mwenyewe kakiri kumiliki bastola na pingu na sio ajabu anaweza kuwa ni Usalama wa Taifa au PCCB sio.Kwa vyovyote vile ana kibali cha kumilika vitu hivyo.issue hapa ni swala la kuomba rushwa,ni vigumu kujua ukweli huenda ni mtego kawekea..Na hiyo 10m alikua kisha pewa au kaomba? huyo kategwa na yeye kaingia kichwa kichwa..

    ReplyDelete
  42. Green Eyed BFebruary 01, 2010

    kwa mtu anaependa kufanya "concrete reasoning" ya maoni ya watu kuhusu hili swala na story yenyewe utapata jibu moja kuwa hii ni set up ya Police Force. Mi nipo inquisitive sana na jamaa aliejiita "Mkata issue" ambaye ukimchunguza flow yake ya kuandika ni definitely Njagu. Nae amekuwa planted atoe maelezo ya "kipolisi polisi" yanayotoa picha nini kitakachofuata akidhani watu humu kwenye blogu hatujasoma au hatujui sheria. Ingekuwa vizuri manjagu wasituingilie huku kwenye blog kwa kutuma some immature comments, wao waendelee kufanya yale walio na uwezo nayo -kama kufanya izi set up, kula rushwa, kuiba, kuazimisha zana za wizi. Aluta Continua.

    ReplyDelete
  43. "Amezidi umbea na yeye...eeeh!!"
    Hii inasikitisha sana,mtu mzima na akili zako kumuuita "mmbea" mtu anayeanika madudu yanayofanya na watu ambao kazi yao ni kuhakikisha madudu hayafanyika.shame on u cabron!
    For sure hili ni toto la fisadi au nilifisadi.

    ReplyDelete
  44. makini jerry namuonea huduma, kweli hili ni vigumu kuujua ukweli ingawa inaonekana kama wamemtegeshea kwani jerry ana tabia pia ya kupenda pesa na kutishia mtu ampe mara nyingi tumekuwa tukimuonyesha hasikii, sifa zilimlevya kijana huyu, mungu amsaidie

    ReplyDelete
  45. HISIA YANGU NI KUWA HII HABARI HAZIJAWA ZA KWELI HADI HAPO SERIKALI ITAKAPOWASILISHA KESUI MAHAKAMANI. NASHAURI TUSUBIRI.

    ReplyDelete
  46. Jamani hii ndo TANZANIA bwanaa. Mtaumiza vichwa vyenu bure lakini this is Tanzania. Ukionekana unataka kuweka mambo ktk mstari uliosawa watu wanakutengenezea nawewe deal ili wakuogopeshe na kukunyamazisha. Nchi yenye kupenda rushwa watu wake utaijua tu. Kaka Jety hizo ni mbinu za kukutisha uache kufichua maovu yao...tupo pamoja, M.Mungu ndo mtenda haki..Aluta continyua....usife moyo mpaka wajirekebishe..

    ReplyDelete
  47. Jerry Muro anamiliki bastola kihalali, tokea akiwa ITV. Hili nina hakika nalo. Hilo la pingu sifahamu.

    ReplyDelete
  48. Hivi jamani kama sio akili nafikiri mwanadam hana kitu kingine cha kutambua mambo. Huyu Wage akamatwe na Jerry Muro mtangazaji maarufu asimtambue? Wage mpaka leo hana Television. Nina wasi wasi na uhalisia wa jambo hili. Pole Jerry, ukweli utajulikana. Watanzania wanaoumizwa na rushwa tunakuombea. Hiyo ni njia ya kublock mbio zako.

    ReplyDelete
  49. Nakujibu anony wa kwanza kabisa:

    Sina hamu wana nia ya kuja nyumbani. Nimeondoka kihalali kwa kutumia elimu yangu na pesa yangu.

    Nilirudi kusaidia taifa lakini nikakuta upuuzi uko pale pale, hamna la maana kimaendeleo katika miaka mitano niliyokuwa naishi nje. Matatizo kufungua biashara, matatizo kulipa kodi, matatizo maji an umeme, matatizo barabara na ufisadi, matatizo wizi na ubakaji, serikali haina nia ya kuleta maendeleo leo wala kesho.

    Nikaamua kuikana uraia wa Tanzania kihalali ili nisivinje sheria, na kuchukua uraia wa Marekani. Sababu ni nyingi, lakini moja ni ya uonevu wa sheria kwa mwananchi. Sasa nastarehe na nalala vizuri pamoja na umeme, mahi safi, na kazi yangu binafsi. Tanzania inakosa wasomi wengi kama mimi (nina MBA Finance kutoka UNiversity of Chicago,Marekani) kutokana na uzembe wa serikali inayokimbilia awamu ya tano bila kuonyesha dalili zozote za maendeleo kwa wananchi wa hali ya chini.


    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  50. utata mtupu!

    ReplyDelete
  51. TZ umaarufu ni business
    Alitumia umaarufu wake kuwa mtaji
    Hakuna mfichua rushwa Tanzania kwakuwa tumezaliwa nayo na tutakufa nayo.
    Namjua Wage hata nilipokuwa nasumbuliwa na wajinga wa namna hiyo Mr Wage alinambia tuwawekee mtego.
    Wage is the honest man i know him

    ReplyDelete
  52. Theory inayotela mantiki ni hii hapa. Polisi na Jerry walikuwa upande mmoja. Polisi walimdanganya Muro akamchunguze wage kuwa ni mtoa rushwa. Tunaambiwa Wage amesimamishwa kazi. Polisi wakampa Pingu Muro na mpango mzima wa kudai rushwa ili wathibitishe tuhuma dhidhi ya Wage. Bila ya kufahamu Jerry alikuwa anafanyiwa set up kwa ushirikiano kati ya Wage na Polisi ambao Jerry kwa sababu ambazo Jerry alifikiri wako na polisi katika uchunguzi. Dili ilipokaa sawa ya kumkamata Wage na Rushwa, Polisi wakamgeuka Jerry na kumkamata yeye Jerry. Ndio maana inaonekana Jerry akabaki kupigwa Butwaa. Wage alikuwa mkuu wa wilaya asingeweza kudanganywa kijinga na mwandishi ambaye kila mtu anamjua. Ukweli utajulikana tu.Polisi wanachekesha

    ReplyDelete
  53. Wage alishawahi kumfanyia mkuu wa TAKUKURU Iringa the same thing. Walimuomba rushwa akawapa. Wakamrudia tena kwa the same matter. Akamlipua jamaa akawa demoted.

    Tanzania woote wala rushwa. Na umaarufu means pesa.

    Hata Mrema alikemea huku akiomba rushwa kubwa sana.

    Pingu alitoa wapi na ana mamlaka gani kumfunga mtu?

    Wabongo acheni kupenda mtu. Kama kafanya atalipa costs zake

    ReplyDelete
  54. Kaka Wage hongera sana
    Hawata kuchezea tena

    ReplyDelete
  55. No set up no majungu. Naamini amefanya. Wage si mtoto wa kutumika na jeshi wala mjinga yeyote.

    Weka ndani

    ReplyDelete
  56. Chokochoko mchokoe pweza binadamu hutomwezaa - ama kweli waswanili walisema. Hata kama huyo mwema kasoma ndo unafikiri atakubali watoto wake wachafuliwe ki-hivyo ili aonekane kuwa hajui kulea!!!?? Mh

    ReplyDelete
  57. Siri kali iko kimya mambo kibao ya ovyo ovyo yanafanyika, ndiyo maana Mwalimu baba wa taifa alisema Askari asitembee ha hela alijua haya. angalia wananchi wa mbezi, kimara, na kibaha mail moja ijumaa hadi leo wamelala rumande eti kuvamia shamba la mitamba, je siri kali inajua hilo RPC anajua, OCD anajua OCCID anajua OSS anajua sasa nani tumshitakie kama wote hao wanajua na pengine ni wao wanayataka mashamba hayo. sasa utasema nini hili la Muro kama system zima inajua?? kilichobaki nimoja nacho kitajulika siku hiyo itakapofika watu wanawataka watanzania waache uoga wa strive kuata chao, tuliwato wakoloni wazungu tumebaki na wakoloni weusi. utawala bora ambao hata UN wanasema tanzania uko wapi?? UN where are you open your eyes and Ears.

    Waandishi Mko wapi au mnashangilia hili, wahalili mpo, NGOs, Legal and Rights mpo, Lawyers, Political Parties e.g. chadema, CUF, NCCR, CCJ mpo or just matumbo yenu and not for Nchi and watu wake???


    Mwl.Nyerere Rudi Uwanyooshe warafi hawa! Wamelitupa Azimio la Arusha na sasa impact inaonekana.

    Aluta Continua...Tumechokaaaa

    The 2015 Minister of Communications, Science & Technology

    ReplyDelete
  58. KAKA MICHUZI TUKO UGHAIBUNI ILA TUNAIELEWA VEMA NCHI YETU. HIYO FILAMU KAKA!!! NA HAIJAANZA KWA MURO. WAKO WENGI WALIOKUWA FIXED NA KUFUNGWA, NI MAMBO YA KAWAIDA KUBAMBIKIZIWA KESI KWA POLICE YA BONGO. TUTAFIKA!!! WALA RUSHWA WAKO URAIANI WANAPETA, WAPIGA VITA RUSHWA WANAPELEKWA SENTRO.

    ReplyDelete
  59. Mara Muro kapokea rushwa,,,,mara kaomba rushwa,,,mara kataka kupokea rushwa,,,hii habari mbona haipo clear kwani kuna mambo mengi yenye utata ndani yake mfano:

    1 jery muro ni mtu anaefahamika sana hivyo sio rahisi afanye vitisho vya kutumia nguvu ( silaha)asihofie kukamatwa.unless atkua hatumii akili na elimu haipo karibu nae.

    2 kama huyo jamaa alitoa taarifa pccb then ni dhahiri kua watu wa pccb wangehusika na pia wangempa fedha ambazo zina namba za siri ili aweze kumpa muro,,kama Muro angekamatwa na fedha hizo za pccb then ni wazi kua kapokea rushwa.

    3 kama Muro alipokea hiyo rushwa hata kama sio fedha za pccb basi ni wazi kua alipowekwa chini ya ulinzi na kukaguliwa angekutwa ni fedha hizo (milioni 10) kama mlalamikaji anavyodai.

    4 suala la Muro kumiliki silaha nadhani itakua ni halali kwani Muro ni mtu anayefanya kazi mazingira ambayo anahitaji kujilinda,,na inaeleweka kua kuna sheria ya kumiliki silaha kwa watu binafsi kihalali.

    5 suala la kukutwa na miwani inayodaiwa kua ni ya mlalamikaji lina utata kwani hata Muro pia anaweza kutumia miwani kama hiyo kwani hakuna brand maalum ya miwani kwaajili ya huyo mlalamikaji. hivyo itabidi uthibitisho utafutwe wa miwani hiyo ikibidi kama kuna risiti pia iwasilishwe na mlalamikaji

    bado yapo maswali mengi sana yasiyo na majibu ila ntaandika zaidi kadiri tutakazidi kupewa taarifa

    mdau wa Blog
    India

    ReplyDelete
  60. Ukweli utajulikana tu, tuwe na subira.

    1. Watu kubambikiwa kesi inawezekana. Mifano ipo michache.

    2. Mtangazaji/Mwandishi wa habari kuomba rushwa inawezekana sana tu. Yaani wanaofanyakazi bila kupokea au kuomba rushwa au Takrima au kupindisha ukweli wa habari ndio wachache! Mifano ipo mingi sana.

    Michuzi wewe ni mkweli, ukipenda basi tuwe wazi hapa uturuhusu tu tuanzishe thread ya kuwataja Wanahabari hao toka mikoa yote ya Tz muone maajabu ya nani atabaki huko!

    3. Mtangazaji kuwa na bastola inawezekana sana. Kuwa na pingu inawezekana pia ingawa si kawaida.


    Watu tusikimbilie kutoa mahitimisho kabla ya kupata habari kamili. Wala tusikimbilie kusema kuwa oh! Jerry ni mtu wa Usalama wa Taifa.

    Jamani, msije mkamuongezea kesi nyingine maana kujiita mtu wa Usalama wakati sio ni kosa la jinai pia.

    Yaani idara ya Usalama wa Taifa imekuwa ya kuchezewa chezewa tu na kumwita yeyote asiye eleweka eleweka hivi. Hata wale vichaa (schizophrenic)tukiwaona mara wanavaa vizuri kidogo au siku nyingine wanaongea yenye mantiki basi tunakimbilia kusema ni wa Usalama wa Taifa. Yaani UWT unatumika sasa kama mwavuli fulani au fashion fulani hivi ya kujitambulisha katika jamii.

    Nadhani ni wakati muafaka Idara hii ipewe heshima yake na wapewe meno makali zaidi ya kushughulikia yeyote anayejipachika wadhifa huu na pia kwa yeyote anayerudisha nyuma maendeleo ya Taifa kiusalama na hata kiuchumi!

    ReplyDelete
  61. sishangai kwa jerry kufanya hivyo namjua vizuri sana maana nilipata nafasi ya kusoma naye kolila high school so far nilishangaa sana niliposikia alipata tuzo ya mwandishi bora ,kama unakumbukumbu vizuri ni huyuhuyu jerry aliyepigana na askari mgambo wakati wa sakata la wamachinga .lakini ndiye huyu pia alitemewa mate na afisa wa ubalozi wa canada .ni huyuhuyu pia aliyewachomea polisi kuhusu rushwa na nakumbuka mwaka fulani kwenye sherehe za nanenane kule morogoro alipigana na askari wa mkoa wa morogoro sina uhakika kama tukio hili lilipotiwa polisi .kwa kifupi jerry ni mtu aliyejaa vituko na kumbuka tulipokuwatunasoma naye kolila alikuwa ni mpenda ugomvi sana na mbaya zaidi hakuwa mtu mkweli alikuwa mwongo na tulimpachika jina la nyau maana alikuwa ni mtu anayepeleka taarifa za siri za wanafunzi kwenye uongozi wa shule .kwa kifupi hakuna alichosingiziwa hapo huyo dogo ni mwalifu ni vile watui kutomfahamu tabia zake toka awali .anyway ngoja tusubiri sheria itakavyosema

    ReplyDelete
  62. cha kushangaza, Jerri angetaka rushwa kwa mtu aliyesimamishwa kazi na waziri mkuu iweje? watueleze vizuri atuelewi

    ReplyDelete
  63. Siku zote nchi inayopenda rushwa ndio ilivyo mi hata sishangai kuona mambo kama hayo ni watu wanaopenda kula rushwa wao ukiwaambia ukweli wanakuona mbaya na kukutafutia kila aina ya sababu wakuharibie na wewe uonekane mbaya.Ila kaka jerry we endelea hivyo hivyo kwa ujumla watu wa namna hiyo sisi tumewachoka ile mbaya.

    ReplyDelete
  64. huondo mchezo wa polisi ya tanzania kusingizia watu

    ReplyDelete
  65. Ushahidi ambao wamemkamata nao ni wa kipuuzi,kwani mtu kuhakikisha kwamba kuna mawani yalke kwenye gari na pingu ndio ushahidi wa kumkamata mtu kwa madai ya rushwa.

    Je vipi kuhusu wale mafisadi wa EPA, kulikuwa na ushahidi wa kutosha lakini hata mahakamani hawakwenda na wala wengine hawajulikani, hiyo ndiyo double standard ya mapolisi wa kwetu wakichokonolewa tu kwamba ni wezi na wala rushwa wanakuja juu na kuamuu maamuzi ya kipuuzi.

    Tanzania nchi yangu najivunia sana lakini Viongozi wetu na vyombo vyake ni mafisadi na waonevu.

    Bullocks

    ReplyDelete
  66. SWALI LA MSINGI

    HIVI MPAKA KUFUKIA HATUA YA KOVA KUIONYESHA HADHARANI SILAHA YA JERRY AMBAYO ANAIMILIKI KIHALALI, KWANI ALIMTISHIA MTU NAYO AU ALIVUNJA SHERIA KUTEMBEA NAYO? KWANI KOSA NI KUTEMBEA NA SILAHA HALALI AU 'KUTAKA' KUPOKEA RUSHWA?


    mzozaji

    ReplyDelete
  67. JAMANI TUSIWE WASHABIKI, TUJARIBU KUANGALIA VIZURI NA KUCKILIZA MAELEZO YA MURO, HUYU JAMAA ATAKUWA NI KACHERO, AU ANAFANYA KAZI TAKUKURU, KWA SABABU KWENYE MAONGEZI YAKE ANASEMA AMESHAWAHI KULETEWA RUSHWA YA MIL 150, HEBU MTU MWENYE AKILI YAKO HIYO RUSHWA YA MIL 150, ALIKUWA AMEITIWA KAMA MWANDISHI WA HABARI AU MTU WA TAKUKURU? CHA MSINGI TUSUBIRI,

    ReplyDelete
  68. anonymous kwa 1st.

    US Blogger ataendelea ku blog from US.

    Asante kwa swali.

    Sitaki kubambikiwa kesi kwamba nimemtukana nabii kumbe tumetofautiana hoja tu.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  69. Acheni kubadili topic, the reason why Jerry was arrested -was an attempt to give bribe, and not on charges to posses a firearm that he had a permit for it.
    It is not a crime/felony to own handcuff, you can get those off the market. Handcuffs are not threat to life, so people need to drop that shit.
    Chief of Police has made a fool of himself, and he needs to step down as public servant, as he doesn't fit to be one. He has lost our public trust

    ReplyDelete
  70. Pole sana bro.Jerry kiukweli wamekucngizia kwani Bactora unamiliki ki halali na pingu zipo sokoni kama bidhaa nyingine.Mie nashangaa kama walisema uliomba rushwa mbona hizo hela hawakukuta nazo?Uckate tamaa endelea kutoa ukweli wa mambo.MUNGU atakusaidia ushinde maswaiba hayo.


    NI Baraka a.k.a Senetor.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...