kikosi cha misri kilichotwaa ubingwa wa afrika mara
ya tatu mfululizo kwa kuifunga ghana
bao 1-0 kwenye fainali huko angola jioni hii
jiji la cairo likizizima kwa nderemo usiku huu
kufuatia ushindi wao dhidi ya ghana
wamisri wakishangilia ushindi
hata ngamia anatabasamu..

SIRI YA MAFANIKIO YA
SOKA YA TIMU YA TAIFA YA MISRI
Kwanza twamshukuru Mungu na pili pongezi nyingi sana kaka Michuzi kwa kutupa nafasi wadau wako wa Globu hii ya Jamii kusema japo bado hatujakabidhiwa rasmini peni na makaratasi katika Maofisi Makubwa katika kuhakikisha mambo yanaenda sawa Nchini Kwetu Tanzania.

Hii tunaileta kwenu wadau Wenzetu kama Hoja ambayo tunaomba ichangiwe na kwa wale ambao wana nafasi Fulani ya kuweza wafika wahusika wa kutekeleza haya tutakayosema wachukue nafasi ya kuwaeleza ili tuzidi kuliendeleza libeneke letu la Tanzania Daima kila kitu kinawezekana.hasa katika swala la soka.

Tukiiangalia siri ya Mafaanikio ya Timu ya Misri Kuna sababu kuu nne naomba nizilete kwenu ili tupate zifahamu na kujifunza na kupitia hizo.
1. Vilabu
2. Uzalendo
3. Kuthaminiwa Wachezaji
4. Kuwa na Viongozi imara na Wajuzi
katika Soka na sikupeana kwa kujuana tu.

Maelezo kwa urefu :
1.Hapa Misri kuna vilabu vingi na imara ambavyo mtakubaliana na sisi kwamba bila ya shaka Ndio Msingi Mkubwa wa kuweza kupatikana Timu bora ya Taifa.

Binaadamu huwa hawatimii lakini kuna mabadiliko makubwa sana hapa. Zamani ilikuwa Wachezaji wa El-Ahly ndio wengi wao wanaunda timu ya taifa lakini sasa hakuna na wao wamejifunza kutoka kwa Mataifa mengine Mchezaji kama Mohammad Nagy Gedo ni wa Timu za kawaida inaitwa Ithad-Sekandari.
Kuwa na vilabu vingi si tija ila katika Vilabu hivyo kunazalika vipaji ambavyo haviandikiki. Hapa Tanzania tuna Ndugu zetu wengi wana vipaji lakini waleaji hakuna Viwanja hakuna na hata kama vipo hata Mipira hakuna inawezekana mpaka kesho Wadogo zetu wanachezea Mipira ya Vitambaa maarufu Cha ndimu.

Hapa Misri Mtoto Mdogo anazoweshwa kupiga gozi sio mpira wa makaratasi baadae akichezea gozi miguu inauma kwa hiyo Mazingira mazuri na ya kisasa.
Ni Moja ya sababu kuu ya kukua soka hapa Nchini Misri.

2.Uzalendo
Wachezaji wote wa timu ya Taifa wanaipenda Nchi yao ndio maana unapowaona uwanjani wanacheza mpira wa kujitoa Muhanga kwa sababu ya kuleta furaha katika Timu yao na Taifa lao kwa Ujumla.

Nasaha
Wachezaji wetu wajifunze Uzalendo na sio Lawama tu Maximo kila Siku kuwa anabadilisha timu bila ya kuangalia sababu. Huenda Nidhamu hakuna na hii inakuja kutokana na kujengeka kwa jeuri Fulani kwa Mchezaji kuwa mimi ni mimi bila ya kulinda maslahi ya kuliletea Heshima Taifa na furaha kwa Watanzania kiuzalendo wa kikweli kweli.
Nidhamu muhimu sana Kaka zangu.

3.Kuthaminiwa Wachezaji
Kama mwanzo tulivyoeleza suala la vilabu kuwa vingi basi tunaomba tuwaeleze kuwa si wingi tu wa vilabu bali vilabu vinawajali sana wachezaji wao. Wenzetu hapa Misri hakuna mgogoro wa Mishahara na wala hutokuta mchezaji anagoma kisa posho kuthaminiwa kwao inafikia kiwango kwamba hupati nafasi kabisa ya kupigana vikumbo na Wachezaji katika Mabasi au hata migahawa ya kahawa.

Wachezaji wao wanajituma sana na watoa nguvu zao zote kwa sababu wanajua kwamba mwisho wao hauna longolongo kwa vilabu. Hakikisha hilo Mdau Kocha wa Timu ya Taifa Maalim Hassan Shehata alikuwa ni Miongoni mwa wachezaji wa timu ya Zamaleik na wengi tu wapo.

Tuwathamini wachezaji wetu ili wajue kwamba hawapotezi muda wao katika hayo wanayoyafanya katika kuliletea Heshima soka la Bongo na Taifa Kwa ujumla. Ni aibu kubwa sana kumkuta Mchezaji mkubwa kama Ngasa,Tegete na Huyo Kocha Maximo eti wanapata nafasi ya kwenda kuuza sura zao katika soko la filamu za Bongo lakini hatuwezi sema sana soko la filamu linalipa sana kuliko Soka.Tuelewane hapo sio matangazo ya dakika mbili tatu.

Inatia uchungu na Masikitiko wachezaji ambao wametoa Mchango mkubwa katika soka la bongo kama kaka Lunyamila,Mwameja n.k kutothaminiwa tena.
Hata thamani ya Muda wao ambao waliutoa katika mchango wa soka la bongo hatuuoni na hatuwajali kabisa leo hata kuwaongopea kuja kuwapa Ndugu zao nasaha,Moyo katika kambi za kimichezo(vilabu)sijui kama inafanywa.
Fani haizeeki,tunawaona si lolote si chochote Ng'oo soka haitaendelea kwa kutowathimini wakongwe hao.

5. Viongozi Imara
Kuwa na Viongozi imara na Wajuzi katika Soka na sio kupeana kwa kujuana tu. Kaka hapa Naomba pazingatiwe sana katika swala kupeana uongozi kiholela Bongo tunaongoza Mtu hata maana ya huo Mpira ajui anapewa Uongozi hapo hatutofika kabisa.

Jamaa huku Wote ambao wanakuwa katika benchi la ufundi ni wajuzi wa soka hakuna kuingiliana katika Sekta ifike kipindi Jamani tubadilike kama Mtu ni Dr. Atulie katika fani yake,mwanamuziki Tulia kwako ila kama unakuja huku katika soka kutoa Mchango wa Mawazo na uwezeshaji wa mambo Fulani karibu sana na sio kukimbilia Madaraka.

Wataanzania pia na tuinuke tuache Usimba na Uyanga tuweke uzalendo mbele! Tuwaandae vijana vyema katika kutangaza soka letu la Bongo na Nchi yetu kwa Ujumla na Serikali vilevile iwekeze katika soka sio Utalii tu soka muhimu sana katika kutangaza taifa sisi tuliokuwa Nchi za nje tunapoona nchi yetu inasafiri kwenda nchingine kucheza soka Tunajisikia raha sana tumechoka kusikia Naigeria,Ghana,Misri Kila siku.

Wadau tusaidiane katika Kupigia debe soka la Tanzania likue zaidi na zaidi.
Tunashukuru sana kwa nafasi hii yapo mengi sana ya Kuandika lakini Naomba Tuiishie hapa.

kwa Maelezo zaidi ya Kiufundi katika soka wasiliana na
wadau wa soka Nchini Misri
Hussein M Afif katika E-mail
husenoo85@yahoo.com
au
Ghalib N Monero. katika E-mail
gmonero@yahoo.com
Imeandikwa kwa mashirikiano ya watu Wawili.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Africa
Hongera Sana Misri kwa Kuchukua
Kombe mara Tatu Mfululizo
Milioniiiiiiiii Mabrouk.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Du kumbe kulikuwa na michuano ya AFrica mwaka huu, haa ok leo ndio ilikuwa final sio kwa mujibu wa maelezo yako.
    Mimi nilikuwa nashuhudia MAN U wakimpa Arsenal dozi ya nguvu.
    Next jitahidi uweke tangazo hapa kabla ya mechi labda nitaangalia hilo soccer bovu

    ReplyDelete
  2. Kwanza Wadau hongereni kwa kutoa mada yenye changamoto katika kijiwe hichi chetu. Pili naipongeza Egypt kwa kutwaa kombe la Africa moja kwa moja. Kwa kweli kwa waliofuatilia kombe la Africa mwaka watakubaliana na mimi Africa is a future of Football in the World. Tukija kwenye mada:
    KWANZA: Kuhusu Vilabu hata mimi nakubaliana na wewe kuwa bila vilabu vyetu kuwa na mipango ya maana ipo siku vitaishia choooni. Kuhusu uwingi wa Vilabu hilo hata mimi nakubali kuwa ni tatizo kubwa. Kwanini zisikusanywe nguvu zote katika vilabu vichache vyenye kufanya ya maana. Badala ya kila siku kufungua vilabu vingine vipya kwa nini hizo nguvu na fedha zisitumike kujenga viwanja vya mazoezi kwa vilabu hivyo vikuu?
    PILI:Uzalendo ni jambo la maana sana katika kuiwakilisha nchi. Hili lianaanzia katika siasa hadi michezo. Kama ulikuwa unafuatilia kombe hili utaona wenzetu wanacheza kwa uzalendo zaidi.(passion) Hili lina shaibiana kati ya mchezaji na nchi yake. Mimi binafsi sijui tatizo liko wapi kwa nchi yetu lakini nadhani Uzalendo unakuja pale unapoona kuwa Unathaminiwa na Nchi yako. Tukianza kuwathamini na kuwalipa vizuri wachezaji basi nadhani uzalendo utafuata.
    TATU; Nidhamu ni kitu cha muhimu katika fani yeyote ile. Na katika soka hasa timu ya Taifa mchezaji huna muda mrefu wa kuichezea kwani ni timu ya nchi na kila Mtanzania ana haki ya kuchezea kama uwezo una mruhusu. Sasa mchezaji anapaswa kuelewa kuwa kwa muda huo mfupi utakao pata kuliwakilisha Taifa "You have to deliver" hii kwa manufaa ya Taifa na yako pamoja na maisha yako. Tumieni nafasi muipatayo kuliwakilisha Tiafa kwani sio wote wapatao nafasi hiyo. Kuweni na uchungu na langi za Bendera!
    NNE: Tutapiga kelele weeeee mpaka tuote vibiongo lakini kama hatutathamini wachezaji wetu basi soka yetu haitafika kokote. Kama Gavana wa benki anatahmniwa kwa kukaa katika hekalu la Bilioni 2.4 eti kwa kuwa anagovern Benki sioni sababu ya kutomjali mchezaji ambaye anatoa jasho lake kuitangaza nchi, kuburudisha wananchi. Ndahani hapo tatizo linakuja kuwa Mtanzania wa juu hathamni umuhimu wa Mtanzania wa chini. Jiulize hivi nchi bila burudani itawezekana na kama haitawezekana basi hapo mtambue kuwa wanasoka pia wana fani muhimu katika nchi kama Magavana wa mabenki. Tatizo hamtambui kwa kiasi gani Timu ya Taifa inachangia kuunganisha nchi. Na hakika leo hii huko Misri hakuna mtu anajali kuwa huyu Mkristu na huyu Muislam yani raha tu!! Nadhani ni Tanzania tu kukuta mchezaji mkubwa wa timu anapigana vikumbo na watu katika mabasi. Ni kitu cha kushangaza eti Miss Tanzania anakabidhiwa gari wakati Mfungaji Bora wa nchi anakatiza mitaani kwa miguu. Hi hii ni akili au madudu. Kinashindikana nini kutoa motisha kwa mfungaji bora wa mwaka anakabidhiwa gari?? Mbona wabunge wanasinzia tu kule Bungeni na kila mtu ana prado?? Hivi hawa watu wazima kweli??
    Kama hilo haliwezekani basi walipeni mishahara mizuri ili waweze kukimu Maisha yao!
    UONGOZI: Ni muhimu katika jambo lolote kuwa na Uongozi Imara na unaojua nini unafanya na wapi unaelekea. Hivi leo nikimuuliza Tenga ni wapi soka la Tanzania litakuwa in next Five years sidhamni kama anajua!! Tuwe na Viongozi Imara kutoka katika ngazi ya Vilabu hati TFF. Sio kupeana madaraka tu bila kujua kama huyu ni Mwanajeshi au Polisi. Kama wewe Mwanajeshi na unapenda Michezo basi anzisha timu ya Jeshi ili utoe mchango wako. Mmmeua michezo ya Majeshi sasa mnataka kuua TFF?? Jamani tuhurumieni. Wachezaji wakuu washirikishwe katika program za kuijenga Michezo ikiwa kucoach au hata kutoa vi warsha vidogo vidogo huko Wilayani.
    Jamani heeeee mimi nishachoka na nchi hii! Mbona siri ya Mafanikio iko Wazi kabisa?? Hivi sidhani kama unaihitaji exposure kutoka nje kujua kuwa Nikimlipa Vizuri Ngassa na Chuji basi atacheza vizuri na Pia watoto wadogo watajituma ili wawe kama wao! Kha! Hivi hii si sawa na 1+1=2??

    ReplyDelete
  3. Mwisho tuache upumbavu kama wa huyo jamaa hapo juu. Mpumbavu mkubwa asiye na hakili hivi unadhani Man U ikishinda we unapata faida gani kama Mtanzania? Hizo zote ni hathari za TV katika nchi za wapumbavu. Ndio maana maana Nyerere alikataa Tv kwa ajili ya watu kama nyie!!

    ReplyDelete
  4. Mimi ni Mkristo lakini huwa ninaguswa sana na hawa Wamisri wakifunga bao wanavyokimbia katika kona moja na kumshukuru mora kwa KUSUJUDU sio kiukata mauno kama akina Drogiba na wengineo.

    Sisi wachezaji tunajua kuwa ktk mashindano, pamoja na utaalamu pia hutokea wakati mwingine kuwa na bahati. Mambo kama,
    Mpira kukonga mwamba, Golikipa kuteleza, mlinzi kujifunga mwenyewe, kukosa penalti maara nyingi yanatokea kwa bahati n.k Hivyo naamini kuwa Mola pia huwa anatusaidia kwa kadri tunavyo muenzi.

    NASEMA KUWA TIMU ZA TZ TUACHANE KABISA NA MAMBO YA KUPOTEZA FEDHA KWA WACHAWI WA TIMU ( ETI BENCHI LA UFUNDI)! BALI TUWE TUNAMWOMBA MOLA!

    ReplyDelete
  5. we mdau hapo juu acha kuita mwenzio mpumbavu kama we ni emirate meza panadoli ukalale utulize maumivu ya kipigo cha manuuu ha ha haa kwani timu zingine zinapochezaga world cup na wabongo wote kama si dunia nzima tunashangilia huwa wanapata faida gani? tena utakuta hata timu sio ya africa lakini watu wako busy kushangilia acha hizoooooo MANUUUUU OYEEEEEEEE misri inakuhusu wewe huna hata haya jelaz tuuuuuuuuuu mbona humzodoi ankali wa smimingpool??

    ReplyDelete
  6. kwa taarifa tu we ulimwita mwenzio mpumbavu asiye na akili wewe niye mbumbumbu madenge mpuuzi usie na akili wivu umekubana ni faida tunayopata ni kuwa tunapunguza bp kwa kucheka ukome kuleta ushwain wako humu ndani kila mtu na mapenzi yake kwani umesikia hilo kombe la misri linakuja kukaa bongo acha unafiki usitake watu wawe kama wewe unavyotaka tunafanya kama tunavyotaka sisi

    ReplyDelete
  7. Na sababu ya tano wanamshirikisha Mungu. Nakumbuka mahojiano ya kocha wao siku chache zilizopita. Alisema hakubali mchezaji ambaye hatambui umuhimu wa Allah Subhana wa Taala. Siyo uchawi bali Mola. Kwa kweli kila wakifunga goli wanamkiri Mungu kwa kumshukuru na kumsujudia.

    ReplyDelete
  8. misri hawana majukumu ndio maana wanashinda ghana wao ilikuwa ni sehemu ya maandalizi kombe la dunia na hata wachezaji wa timu zinazotuwakilisha kombe la dunia hawajitumi kuogopa wataumia huku wakihofia nafasi zao ktk vilabu vyao ulaya... endapo mashindano yakibadilishwa muda na kuchezwa kuanzia mwezi wa sita misri atakuwa hana chake

    ReplyDelete
  9. Mmesahau fitina pia. Misri hushinda kwa mpira na kwa hila pia. Marefa wa Afrika huwabeba sana Misri.

    ReplyDelete
  10. Eti Uzalendo.. nani mzalendo Tanzania???!!! Tunataka wachezaji mpira wawe wazelendo, wajitume na kuipenda nchi yet ya Tanzania. Ok sawa nani anaipenda nchi ya Tanzania???!! Viongozi woteeee wenye nafasi serikalini ni WEZI, MAFISADI, WALA RUSHWA, HAWAJALI WANANCHI, unakuta shule ina wanafunzi 400 na shule nzima ina mwalimu mmoja tu. Ulishaona wapi duniani??? kila kukicha viongozi ni safari safari safari na msululu wa watu kibaoooooo, wizi kila sehemu, wachezaji familia zao wakiamka asubuhi hata haijulikani watakula nini?? watoto wao wanasoma shule za akina KAYUMBA, then eti tunataka wachezaji wajitoe mhanga wafe maji wakikimbia na kutetea Tanzania. Jamani ebu tuangalie mazingira ya wachezaji wa MISRI au nchi nyingine na wachezaji wa Tanzania mhhhhhhh hainiingii kichwani hata kidogo.
    Kuipenda na kuwa wazalendo kwa ajili ya Tanzania kila mtu aanze moyoni mwake. Viongozi wa nchi ya Tanzania wawe mfano kwetu.
    Wauze baadhi ya nyumba zao na mali zao wawekeze kwenye michezo kwani hayo majumba, magari yao ya kifahari yoteeeee ni jasho la watanzania anyway.

    Michuzi usinibanie maana umekuwa ukinabania sana kutoa maoni yangu, huwa huyatoi.

    Mtoto wa Mkulima

    ReplyDelete
  11. ofkoz ghana,nigeria,algeria have nothing to loose...misri kwa raha zao tu na mapozo ni sawa tu kubeba ilo kombe...

    TOGO NEWS ankal tuwekee:
    ila sijaelewa ya Togo kufungiwa na kupigwa faini kwa kutocheza CAF,,nielimishwe maana haiingii akilini

    ReplyDelete
  12. afu mbona kichwa cha habari hakina MSHAWASHA? mh ingekuwa mitimu ya ulaya basi ankal angebandika bichwa kuuuuuuuuuuuuuuuuubwa

    afu mnasema uzalendo hakuna kitu kama icho afrika apa,ni hao waarabu tu na misimamo yao ndo inawasaidia...kama annon mlokole avosema

    ReplyDelete
  13. UNAJUA IBILISI ALIVYOKUA ANAISHI MBINGUNI KWA MUNGU ALIPACHIKWA JINA ABASAJIDDA(BINGWA WA KUSUJUDU)NA ALIWASHINDA HATA WENYEJI(MALAIKA)NA MUNGU ALIMPENDA KWA HILO.egKILA AKIPIGA HATUA ANASUJUDU.SASA LEO UMEPIGA GOLI HALAFU UNAMSHUKULU MUNGU KWA KUSUJUDU KWANINI USISHINDE.HALAFU WENZETU KILA MCHEZAJI UTAIFA AMEUWEKA MBELE ZAIDI NA NIDHAMU YA HALI YA JUU ZAIDI.

    ReplyDelete
  14. big up!!! misri..wenyewivu wajinyonge.watanzania hatutazami matatizoyetu natim zetu yako wapi kazi madonge yametujaa.mimi mtanzania asilia na naipenda nchiyangu.but nimefurahi sana hao watu kuutwaa ubingwa..hawajalala nakuamka na kupewa huo ubingwa....
    mdau mitaa yakati.

    ReplyDelete
  15. Hongera Misri na hata hivyo leo nilikuwa nasikiliza taarifa za habari za huko zinasema kwamba Naigeria wanamtaka kocha wa misri awafundishe kombe la dunia na ukiingia web ya CAF wachezaji wa 5 wamechagulia kuchezea timu ya Afrika hamna noma sisi Bongo tulale tu Majungu,kusifu watu inatosha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...