Habari za leo kaka Michu.
Sisi wana Mafia tumeona bora tuchukue fursa hii kujitambulisha rasmi kwenye blog yetu ya jamii na kama utakavyoona kwenye tovuti yetu kuwa sisi ndio wenye asili ya Kisiwa chetu cha Chole ambacho maarufu kama Mafia.

Pia tumeona bora tuchukue fursa hii kuweka wazi kuwa sisi kama wenyeji na wazawa wa Kisiwa hichi ambacho kwa bahati mbaya tumetengwa Ki Jiografia na Kimaendeleo kuwa tutashirikiana kwa hali na mali na serikali na jumuiya zote zenye nia ya kuendeleza maendeleo ya Kijamii ambazo zitaenda sambamba na kulinda utamaduni, mila na desturi zetu bila kuvunjwa heshima kwa kisingizio cha Maendeleo.

Sisi wana Chole hatufungamani na upande wowote kwenye mambo ya Siasa au Itikadi yoyote ile ila hatutokaa kimya kuona watu ambao hawana nia njema na Kisiwa chetu kuendelea kufanya watakayo bila kuomba ridhaa ya wana Chole. Na pia hatutosita kutoa maoni yetu kupinga au kuunga mkono watu au jumuiya ambazo zitakuwa zinafanya shughuli zake hapa Kisiwani kwetu.

http://www.friendsofmafiaisland.com/
Karibuni sana kwenye tovuti yetu na

tunaomba maoni yenu kupitia anuani za barua pepe zifuatazo:

General enquiries: info@friendsofmafiaisland.com

Campaigns team: campaigns@friendsofmafiaisland.com

Publications: publications@friendsofmafiaisland.com

Membership and supporter services: supporterservices@friendsofmafiaisland.com

Pia mwaweza kutupata kupitia e-mail hii:

friendsofmafiaisland@gmail.com

Tunatoa shukrani zetu za dhati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. haya wana wa chole-mafia,tumeona na tutakuja kutembea.

    ReplyDelete
  2. Mafia kuna mandhari safi sana.

    Hata Bill Gates huchukuwa low profile vacations huko Mafia. Nilishaonana naye huko.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  3. Mzee Wa Zeze, OhioJanuary 08, 2010

    Wana Mafia mbona mmeanza na mkwara mzito sana juu ya utamaduni, siasa na maendeleo yenu? Msiogope jamani, utawala wa kisultani hautarudi milele hivyo kuleni changudoa wenu kwa raha zenu na sisi wabara tunakuja kudowea.

    ReplyDelete
  4. Pongezi kwenu wana Mafia kwa kujitosa rasmi ktk libeneke.

    http://tembeatz.blogspot.com/

    ReplyDelete
  5. Mbona webusaiti nyenu mikwala kibao kama vile unatembele webusaiti ya benki au hospitali, yaani ka vile mna taarifa nyeti (confidential data)

    Ushauri: webusaiti yenu iwe 'customer-friendlly' aka muwaenzi watalii watarajiwa/donors n.k kwa kuifanya webusaiti yenu iwe na picha/info kibao za hoteli za huko kisiwani, pwani safi, dolphins n.k

    Mdau
    Canary Islands

    ReplyDelete
  6. hii ni nzuri sana tusiitegemee sirikali iliyotuongoza kwa miaka 48 ifanye mapinduzi ya kiuchumi kwa miaka 5.!

    tnawangoja iringa,tanga, kigoma, mtwara na wengine waliosahaulika wawafuate kuyakomboa maeneo yao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...