Unaweza kupata mpango tulio nao hadi hivi sasa wa kushiriki katika kuchangia wahanga wa mafuriko yanayoendelea nchini kupitia Chama cha Msalaba Mwekundu.
Tumepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Mkuu wa Kitengo cha Maafa wa chama hicho nchini Bw. Joseph Kimaryo ambaye anatueleza hali ilivyo hadi hivi sasa (Jumamosi Januari 9, 2010).
Kwa kushirikiana na tovuti za Jamiiforums na Mdau wa Jamii Bw. Issa Michuzi; pamoja na kushirikiana na Mtandao wa Wanaataluma wa Tanzania (TPN) tumeandaa mpango wa kuwashirikisha Watanzania mahali popote pale walipo kuchangia katika adha hii inayowakuta ndugu zetu katika mikoa mbalimbali hasa Morogoro, Dodoma, na sasa hivi Shinyanga na hata Mwanza na kuna uwezekano wa sehemu nyingine nchini kwa kadiri siku zinavyoendelea.
Tumeamua kutumia Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania kwani rekodi yao katika kufika na kutoa misaada wakati wa majanga hailinganishwi na chombo au taasisi nyingine yoyote. Zaidi ya yote tumepata uhakika wa kutosha wa misaada yetu kufika kwa walengwa baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mstahiki Meya (Dar) Adam Kimbisa (CCM).
SHUKURANI MKUU WA KAYA TUENDELEE KUWA PAMOJA MPAKA CHAWA AVUNJIKE
ReplyDelete