wataalamu wakipima maeneo ya kiwalani katika
mchakato wa upanuzi wa uwanja wa ndege dar
wapimaji wakiendelea na kazi maeneo ya kiwalani
ambapo nyumba zote hizo zitapigwa nyundo
shoto ni ukuta wa uwanja wa ndege wa dar na
kuume ni nyumba ambazo zote zitapigwa nyundo
nyundo inaendelea maeneo haya kupisha upanuzi wa uwanja huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Afadhali, labda ule ufisadi unaweza ukapungua unaoendelea kwenye kiwanja cha sasa hivi. Kwani unaisha lini huu ujenzi?

    ReplyDelete
  2. Sina uhakika hiko kiwanja cha ndege kiko mjini kiasi gani. Nimeona kiwanja cha ndege hapa Lisbon kinataka kuhamishwa na kupelekwa nje ya mji kidogo kwa sababu makelele ya ndege imekuwa ni kero sana pia ndege zinapotaka kutua zinakuwa chini chini na ni hatari kwa majengo marefu. Sijui kama haya yamezingatiwa

    ReplyDelete
  3. Aah na nyie too much sasa, kila kitu hamna hakika, sasa hayo majumba yalikuta uwanja au uwanja ulikuta majumba? Kama ukipelekwa nje ya mji na watu nao wakaufuata kuhamia huko, itabidi nako uvunjwe?

    ReplyDelete
  4. Jamani mie naomba mnijuze! Hivi upanuzi huu unajumuisha ujenzi wa njia mpy pajona na departure na arrival launges mpya au upanuzi huu unahusisha nini? Je inawezekana tukapata ramani ya jinsi uwanja mpya utakavyokuwa baada ya kukamilika?

    ReplyDelete
  5. hiyo terminal ingeachwa ilivyo na kujenga nyingine nje ya mji kwa kujenga wanja la kisasa, pia wangefikiria kujenga reli ya kutoa abiria mjini kuwapeleka kwenye huo uwanja

    ReplyDelete
  6. nyinyi wadau mjajua inagharimu kiasi gani kujenga uwanja wa ndege mpya? Kweli mnaishi Tanzania bila ya kujua data za uchumi wa nchi yenu? Kwa manufaa yenu, Tanzania ni nchi masikini na inahitaji misaada kila mwaka kulipa gharama za kuendesha nchi na kuwalisha wananchi. Watapata pesa wapi kujenga uwanja mpya? Tuna ubavu gani?

    ReplyDelete
  7. inaonekana patakua bomba sana.na sisi wa kiwalani tupate pakujisafishia macho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...