


Ankal,
Hii taarifa ya Globu ya Jamii juu ya gemu la leo haiko sahihi. Ukweli ni kwamba Taifa Stars leo imefungwa nusu bila.
Kituko cha leo ni kwamba Taifa Stars imecheza na timu mbili tofauti
zote zikijiita timu ya taifa ya Cote d'Ivoire. Kikosi cha kwanza
(akiwemo Drogba) kilishinda 1-0, halafu ngwe ya pili kikaja kikosi
kingine kipya kabisa cha ma-underground kikatoka kapa.
Naomba kuwakilisha.
Hii taarifa ya Globu ya Jamii juu ya gemu la leo haiko sahihi. Ukweli ni kwamba Taifa Stars leo imefungwa nusu bila.
Kituko cha leo ni kwamba Taifa Stars imecheza na timu mbili tofauti
zote zikijiita timu ya taifa ya Cote d'Ivoire. Kikosi cha kwanza
(akiwemo Drogba) kilishinda 1-0, halafu ngwe ya pili kikaja kikosi
kingine kipya kabisa cha ma-underground kikatoka kapa.
Naomba kuwakilisha.
Mdau FM
acha kujiridhisha mtaalam. hapo lingekuwa kombe la maana kwao basi hata hao maandagraundi wangetuchapa tena hata 6. the drogba who plays against liverpool, man-yu, gunners or against barcelona is not the drogba you saw today. toure man city, yaya barcelona drogba cehlsea eboue arsenal dindane portsmouth we wafa'mchezo nini!!. subiri uone moto wao weldi kapu na sio angola sababu drogba hata kwenye african cup of nations huwa anacheza kwa kuibiaibia akiogopa kuumizwa. jamaa akili na maisha yake yote yapo kule anapopatia tonge la ugali chelsea.
ReplyDelete...sasa Drogba kudaivu ndo hadi Bongo, jamani?
ReplyDeleteIvory coast wameamua kuwa wapole kwa mwenyeji, hebu tuache kujisifu bure, wangetaka kupiga bao 10 wangeweza. Hivi unazani Drogba angeleta game A hapo? yeye kama super star ametimiza wajibu wake kwa kuwaonyesha wapenzi wa soka mavitu yake, lakini huku akiwa mpole sana, wote mmefurahi kuona na wao wamejipatia tizi. Akili yao yote ni Sauzi tu tuelewe hilo, sie ndo wenye bahati kwa kuweza kujipima na a very relaxed big team.
ReplyDeleteAnkal, kutufunga wan'tufunga ila chenga tu'nwalaa.
ReplyDeleteAsanteni Ivory Coast kwa kutufunga kiduchu na kutulindia heshima yetu. Sisi tulitegemea yakiwa kidogo basi ni matatu tu.
Kwa wale tuliouona mchezo, achilia mbali Ivory kuwa wanajipima, timu yetu inahitaji kwanza pongezi..pili ndo tukosoe, wachezaji wetu wanazubaa sana sasa sijui ndo kuogopa majina makubwa, Ngasa kabaki na kipa akashangaa..beki 3 hivohivo, otherwise defence imecheza vizuri mno na kiungo kiasi..ila forward hatuna..
ReplyDeleteHiyo Luning ya TVT ni ya mwaka 47? Huyu TIDO vipi?
ReplyDeleteHallo Ankal Michuzi, natumaini hautaibana hii post yangu.
ReplyDeleteKwanza, hiyo picha ya mwanzo, Nadir Haroub "Cannavaro" alicheza bonge ya proffessional tackling toka kwa Drogba, otherwise hilo ndio lilikuwa goli la kwanza. Kwa yoyote aliyoiona live atakubaliana na mimi. Ilikuwa ni the best,naamini hata Cannavaro akihojiwa hiyo ndiyo ilikuwa best moment kwake. Mimi inanikumbusha tackling aliyoicheza Edgar Davids kwa Ronaldo De Lima kwenye nusu fainali ya World Cup 98.
Pili, Wabongo tusipende kuwa negative tuuu muda wote na hii ndio
shida kubwa ya watazamaji mpira wa kibongo. Ila kiukweli kwa mjua soka yoyote duniani na aliyeangalia ile game live ni kwamba Taifa Stars walicheza vizuri sana ila tatizo kubwa kama ambavyo mara nyingi timu yetu ya taifa na hata vilabu tunalo ni ukosefu wa goal getters, Tanzania bado tuna tatizo kubwa la umaliziaji, game ya jana tumepoteza two clear chances za kufunga, moja ni ya Ngasa na ya pili ni ya Tegete iliyogonga nguzo ya goli. Ndio maana ni nadra sana kusikia timu yetu imeshinda goli zaidi ya mbili, regardless timu tunayocheza nayo ni ya kiwango gani. Tuna tatizo kubwa kwenye foward.
Tatu, hapa mchawi sio Maximo wala mfumo wake wa uteuzi wa wachezaji, tatizo kubwa ni mfumo wetu wa soka, hatuna msingi wa soka kabisa. Hakuna nchi yoyote duniani yenye mfumo mbovu wa kukukuza vijana wadogo kwenye soka kama wa Tanzania na ina kiwango cha maana kwenye mpira, na anayebisha hili aniambie ni nchi gani ina mfumo wa mpira kama Tanzania na ina kiwango cha kushiriki world cup. Hakuna.
Ligi kuu yenyewe ina timu 12, halafu inasimama mwisho wa mwaka toka November baada ya mchezaji kucheza mechi 11 tu hapo ni mpaka February, hivi huyo mchezaji ataweza kuwa na ubavu, pumzi na stamina wa kupambana na akina Drogba? Na kwanini ligi yetu inasimama, wenzetu wanaosimamisha ligi mwisho wa mwaka ni kwa ajili ya kupisha majira ya baridi, hapa kwa nini tunasimamisha ligi? Halafu wabongo mnamlaumu Maximo, hapa hata aje Guus Hiddink kwa mfumo mzima wa mpira wa kibongo hakuna kitu.
Nawakilisha Ankal.
International Observer aka IO
Mzee Mayai nakuona mwenyewe enzi zako ulitesa, sasa unaangalia watoto nao wakihangaika bravoo mkuu kula nondozzzz hizo
ReplyDeletejamani mnalalamika kwa ivory coast kubadili timu,tushukuru waivory coast sio majigambo.manake wametia timu iliyokomaa mwanzo na wameona watashinda magoli kadhaa na wameamua kuweka timu ammabyo inafanana angalau na ya bongo ili watu wainjoy soccer,manake kipimo cha tz kilikuwa si cha kuweza kucheza na mastaa wengi wa uefa kama kina didier.mie mwanangu wa miaka 13 anacheza kwenye club moja ya premier hapa na tukipambana na wachovu anamuweka kipa kuwa striker sababu anajua awezi shindwa.hao waivory coast watu babu kubwa na wamefanya vema kuja bongo na najua watakuwa wameinjoy kinoma..hongera Taifa stars kugangamaa .maximo kazi poa .
ReplyDeleteDROGBA TABIA YAKE YA KUGARAGARA KAMA KABEMENDWA MPAKA TANZANIA KAYALETA. MIE NILIJUWA ANAWAFANYIA UK TU. PAZI.
ReplyDeleteHii clip inaonekana vizuri sana
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=gR1iMA3MXvg
Tanzania 0 vs 1 Coast on 4 Jan 2010 highlights.flv