VIBARUA wa kampuni ya ujenzi ya WEBCO – BESHU Joint Venture yenye Makao mikoa ya Mbeya na Dar Es Salaam wakitumia mifagio kuondoa vumbi katika barabara ya Msakila katika Manisipaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.


Hii ni miongoni mwa barabara za Manispaa ya Sumbawanga zenye urefu wa km 5.9 zilizojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni hiyo kwa gharama ya zaidi ya bilioni 1.2, na kuzua gumzo kubwa kwa wakazi wa mjini humo wakililalamikia kampuni hiyo kuwa imezimejenga kwa kiwango cha chini mno.



Hivi karibuni kufuatia malalamiko hayo ya wananchi uongozi wa serikali mkoani hapa chini ya Mkuu wa Mkoa Mh. Daniel ole Njoolay umetuma maombi rasmi ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali(CAG) kuunda timu ya wataalamu kutoka ofisini kwake itakayotathimini thamani halisi ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa barabara hizo katika kiwango cha lami. Picha na habari na mdau Peti Siyame.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. mfipa in USJanuary 23, 2010

    lami iko wapi?!

    ReplyDelete
  2. Kweli tunahitaji wakandarisi wa ndani kama kazi zao ndio zilivyo? kama kampuni hazina uwezo wa kujenga ni afadhali tuchukue za kigeni ilimradi tupata barabara bora. Au ni ufisadi kama kawaida ya wa TZ? sasa hiyo barabara ya matope mnaita lami si heri ingejengwa ya changarawe ijulikana basi.

    ReplyDelete
  3. Mambo ya lami hewa nini...

    ReplyDelete
  4. Jamani lami si nyeusi mbona hapo tunaona vumbi jekundu!!!!!!!!!!!
    Ameliwa mtu hapo inabidi kusimama kidete kutetea hela za walipa ushuru hapo! Huu ni wizi wa kimachomacho haiwezekani kuliwa hivi hivi!!!!!!

    ReplyDelete
  5. NI WIZI TU, WAKILETWA WA NJE MNALALAMA, EEE WAZAWA HATUPEWI KAZI KWA MTAJI HUO, WAPI NA WAPI LAMI IKAJENGWA NA FAGIO, ACHENI WIZI HUO

    ReplyDelete
  6. Jamani mnaouliza lami...
    Kwani ujenzi umeisha?

    Ila wanajenga kichovu

    ReplyDelete
  7. Jamani mbona kila kitu kikimalizwa kujengwa halafu wananchi wakalalamika kwamba zimetumika hela nyingi au pana ufisadi ndio anakumbukwa mkaguzi wa mahesabu hivi huwa hao wanaothibitisha malipo inakuaje mpaka mabilioni kila siku yatumike ndio tukurupuke?

    ReplyDelete
  8. eti lami..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...