Hii ni miongoni mwa barabara za Manispaa ya Sumbawanga zenye urefu wa km 5.9 zilizojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni hiyo kwa gharama ya zaidi ya bilioni 1.2, na kuzua gumzo kubwa kwa wakazi wa mjini humo wakililalamikia kampuni hiyo kuwa imezimejenga kwa kiwango cha chini mno.
Hivi karibuni kufuatia malalamiko hayo ya wananchi uongozi wa serikali mkoani hapa chini ya Mkuu wa Mkoa Mh. Daniel ole Njoolay umetuma maombi rasmi ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali(CAG) kuunda timu ya wataalamu kutoka ofisini kwake itakayotathimini thamani halisi ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa barabara hizo katika kiwango cha lami. Picha na habari na mdau Peti Siyame.


lami iko wapi?!
ReplyDeleteKweli tunahitaji wakandarisi wa ndani kama kazi zao ndio zilivyo? kama kampuni hazina uwezo wa kujenga ni afadhali tuchukue za kigeni ilimradi tupata barabara bora. Au ni ufisadi kama kawaida ya wa TZ? sasa hiyo barabara ya matope mnaita lami si heri ingejengwa ya changarawe ijulikana basi.
ReplyDeleteMambo ya lami hewa nini...
ReplyDeleteJamani lami si nyeusi mbona hapo tunaona vumbi jekundu!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteAmeliwa mtu hapo inabidi kusimama kidete kutetea hela za walipa ushuru hapo! Huu ni wizi wa kimachomacho haiwezekani kuliwa hivi hivi!!!!!!
NI WIZI TU, WAKILETWA WA NJE MNALALAMA, EEE WAZAWA HATUPEWI KAZI KWA MTAJI HUO, WAPI NA WAPI LAMI IKAJENGWA NA FAGIO, ACHENI WIZI HUO
ReplyDeleteJamani mnaouliza lami...
ReplyDeleteKwani ujenzi umeisha?
Ila wanajenga kichovu
Jamani mbona kila kitu kikimalizwa kujengwa halafu wananchi wakalalamika kwamba zimetumika hela nyingi au pana ufisadi ndio anakumbukwa mkaguzi wa mahesabu hivi huwa hao wanaothibitisha malipo inakuaje mpaka mabilioni kila siku yatumike ndio tukurupuke?
ReplyDeleteeti lami..
ReplyDelete