Bwana michuzi,
Kuna jambo ambalo limenitokea nikaamua kulileta kwako ili uweze kulitoa kwenye blog yetu ya Jamii huenda itasaidia wadau wengine manake hata mimi huaga najifunza mambo mengi sana kutoka kwenye blog hii.

Siku ya jmosi nilienda mjini kidogo kufanya shopping ya bidhaa nilizunguka sana nikapata kiu ya maji bahati nzuri nilipokua napita mitaa ya kisutu nikakutana na muuza maji alikuwa amebeba kwenye box lake maji ya aina ya uhai ikabidi ninunue alikua amebeba yale ya shilling 300/=.Nikanywa harakaharaka kwa sababu nilikua na kiu kali.

Baada ya kumaliza sikukitupa hicho kichupa cha plastic maaana sikuona mahali pa kutupia kwa hiyo nikaamua niende nacho mpaka nipate mahali pa kutupia.Nikawa nimekishika mkononi mara wakati naichezea mkononi nikahisi mikwaruzo kuangalia kumbe kile kichupa kilikuwa kimetumika nilipoangalia kwa makini ndani ya chupa nikaona uchafu na juu ya mdomo wake nikaona uchafu mweupemweupe...
Nakuambia,Michuzi niliishiwa nguvu.Nikapata mstuko mkubwa nikaenda mpaka pale mtaa wa Samora nilipokua nimepaki gari nikawa nimeduwaa sijui lakufanya.Wale vijana wanaokaaga pale kuongoza magari kupaki na saa nyingine kuosha magari wakaniuliza vipi?Nikawaeleza mkasa wote wakacheka sana wakaniambia umekunywa maji ya bomba sasa kilichobaki nikuomba Mungu usipate typhod.
Sasa wakaanza kunielimisha. Wakanieleza namna hayo maji vijana wa mjini wanavyoyatengeneza.
Kuna njia kuu mbili. Moja ni kuwa wanaokota hayo sijui niite makopo au vichupa vya plastic sehemu mbalimbali jijini wanajaza maji ya bomba au maji yoyote watakayopata halafu wanaenda kiwandani wananunua mifuniko pamoja na seal zake kabisa wanakuja wanasokomeza hiyo mifuniko pamoja na seal kwenye hivyo vichupa sasa wewe ukija kununua hayo maji ukafungua huo ufuniko lazima ikate seal kwa hiyo unapata imani unakunywa.

Njia ya pili wanaokota hivyo vichupa pamoja na mifuniko wanafungua wanajaza maji halafu wanachukua super glue wanaizungushia katikati ya mfuniko na seal yake wewe ukija kununua ukafungua utaona unakata seal kumbe ni super glue unakata.

Hii kitu ni hatari sana manake vichupa vyenyewe wameokota na hata kuviosha havijaoshwa kwa hiyo hapo mtu unakua na risk ya kupata TB,Typhod na magonjwa ya matumbo Kipindupindu.

Kwa hiyo wadau kuweni waangalifu na maji ya barabarani hasa ,wale vijana wanaobeba maji mikononi ambao wako katika mitaa mingi ya jijini Dar-es Salaam.Mfano maeneo hayo ya kisutu,kwenye mataa ya pale faya,manzese,ubungo na sehemu nyingine nyingi hasa zile sehemu zenye vituo au kwenye mataa.

Wako katika mitaa mingi ya jijini Dar-es Salaam.Mfano maeneo hayo ya kisutu,kwenye mataa ya pale faya,manzese,ubungo na sehemu nyingine nyingi hasa zile sehemu zenye vituo au kwenye mataa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Hii mbona iko siku nyingi?! na huu ni mtambo mzima sababu mimi binafsi nilikuwa nanunua maji jumla kwa matumizi yangu binafsi, nikagundua hilo nikamfahamisha kijana mmoja anafanya kazi huko uhai akasema atakwenda kuwafahamisha wakubwa wake, kuja kuonana nae tena ananambia kafukuzwa kazi sababu wanamshuku labda yeye ndiye anafanya mchezo huo! nilijuta kumwambia!
    mimi nafikiri kuna kigogo huko anayeuza hivo vizibo kwa wingi sababu hata maduka ya jumla maji hayo yapo utakuta chupa zina mikwaruzo balaa lakini inatoka ndani ya packet yake!

    ReplyDelete
  2. Ahsante kwa kutuelimisha,kwani mimi mara nyingi nikija bongo huwa napenda kununua maji maji kwa vijana wa mitaani ili niwape tafu juu ya biashara yao. Maybe wanafanya hivyo kwa hali nguvu ya maisha or maybe wakifanya hivyo wanapata faida zaidi, vhasara yake wanahatarisha afya kwa wanunuaji.mambo ya bongo yanaenda kibongo bongo tu.Tutaishia kuja kutembea na kugeuza.

    ReplyDelete
  3. halafu tunalaumu wachina kwa bidhaa feki- ustaarabu kitu ghali sana!

    ReplyDelete
  4. Mie ndugu yangu nikupe pole, kama alivyosema Ano hapo juu ni kwamba huu mtindo upo muda mrefu sana, cha msingi ni sisi watumiaji wa maji kua makini, na matukio kama haya si ya kuyamazia tuu, wahusika wanaoshughulikia swala la usalama wa vyakula wanatakiwa kuchukua hatua kwa hili, kwani ni uzembe unaonekana kua wazi kuanzia kwenye kiwanda. Iweje mifuniko na hizo seal zipatikane kirahisi kama sio uzembe wa kiwanda?? Na ni kwa nini hii issue imekuwepo siku nyingi na ni kwa aina hii ya maji tuu na wenye kiwanda/biashara yao wamekaa kimya bila kujali kua biashara yao inaharibiwa na watu ambao sio waaminifu? Mie nadhani hapa suluhisho ni kuwaadhibu wote, wanaouza hayo maji na wenye kiwanda, ili wote kwa pamoja wawe makini. Ila hili litawezekana kwa kila mmoja wetu kutoa ushirikiano kwani itakua rahisi sana kuwakamata.

    ReplyDelete
  5. Bongo tambarare

    ReplyDelete
  6. Dawa kila mtu atoke na maji yake nyumbani. Ni salama zaidi,kuliko kununua maji hujui yametoka wapi.

    ReplyDelete
  7. Mfukuampunga KalambamajiFebruary 23, 2010

    Duh; Mi nimepatwa na shock!! Kha!! Kwanza sikujua maji yamefika sh.300/=.

    Afu mambo hayo ya kuhatarishwa afya jama...that's over the top. I would beat the H*** up that boy ningempata. That's some serious stuff.

    Kwanza hizo chupa huenda hazikuoshwa, Pili maji siajabu ya kisima, afadhali ya bomba, tatu wanaunganisha na super glue??? that's poison!!

    Nikifikiria ushenzi kama huu naona bora nibebe maboksi mpaka mgongo utakapochoka...sirudi ng'o.

    ReplyDelete
  8. dawa ni kutokununua maji kwa hao vijana na kutonunua maji ya UHAI popote pale,mie ndo mwisho wa kunywa maji ya UHAI,maana uzembe unaanzia kwao kutoa hizo seal.

    ReplyDelete
  9. bwana michuzi Pole kwa kazi. Naomba baadhi ya posts kama hizi mziandikie feature story ili mzitoe magazetini ili watu wengi zaidi waweze kuzisoma na kuchukua tahadhari. Mimi siku zote nakunywa maji ya chupa lakini sikumoja nilipata matatizo makubwa ya tumbo na nilipoenda hospitali niliambiwa nina wadudu wa amoeba wengi tumboni na nikaambiwa hupatikana kwa kunywa maji sio salama nikacheka sana nikamwambia Dr. Sinywi maji ya bomba mimi ni ya chupa tu akasema ni hayohayo tena inawezekana sio ya bomba bali ya kisima nikaishiwa nguvu. Ushauri kwa wasomaji msinunue maji ya barabarani ingia katika duka linaloeleweka. Maji yakikatika usinunue yale yanayopitishwa na vijana kwenye madumu ya njano kwa ajili ya kupikia na kunywa. Madumu yale mara nyingi hubebea maji ya miferejini sisi wa sinza tunayatumia sana hayo yanayochuruzika kutoka katika oxidation ponds za chuo kikuu kutokana na njaa ya vijana wetu wanaotuuzia hawawezi kwenda mbali kuchota maji wakati wanayaona hayo yanachuruzika.isitoshe maji mengi ya miferejini yanachukua maji machafu ya vyooni kwa vile Dar es salaam hakuna standards za vyoo vya kuchimba na hata septic tanks za nyumba nyingi hazikaguliwi kuona katika maeneo yenye water table iliyo juu yachimbwe vipi na umbali gani wengi huacha matundu makubwa maji yatoke ili kuepuka gharama za kunyonya.
    Haule

    ReplyDelete
  10. pole sana kaka mbona mara kwa mara kwenye TV wanatangaza maji ya barabarani si salama nunua sehemu ambayo unaona afadhali kidogo salama,au beba toka nayo hoe

    ReplyDelete
  11. jamani wa-tanzania wenzangu kuna kiwanda cha ketengeneza hivi vizibo na chupa pamoja serials lakini hapo kiwandani kuna watu wanalipwa Tzs 70,000/= kwa mwezi halafu huyu ndo store keeper akija mtu anataka hivyo vizibo lazima amuumuzie ili apate kumudu maisha sio Uhai tu hata kilimanjaro, syrup za watoto,baadhi ya vyakula vya kupaki hata viroba vya sukari,ngano hata ndoo za sabuni na viroba vyake watu wanamksi na machicha ya nazi hii ndo bongo land bwana kila kila kitu kipo kwa gharama unayotaka wewe.tuwe makini katika ununuzi wetu wa majumbani

    ReplyDelete
  12. Kama wenye viwanda hawajali maisha ya watu basi Canteen ziuzwe kwa wingi. Kiwanda kikose wateja wafunge ndio watajifunza.

    Bongo bwana...ingawaje hata huku tunaambiwaga spring water hayatoki huko kwenye spring maine kweli...

    Ila huku hawadouble dip chupa...sasa huko huyo anayelundika tu maji hujui aliyetumia hiyo chupa before alikua anamagonjwa gani na kama hayo maji yamechemshwa kweli...Kichochooooooo

    Nikuomba Mungu tu

    ReplyDelete
  13. Waswahili walishahisi kuwa binadamu hana thamani hasa mtanzania. Hapa tukaze roho tu. Tunakula vitu vingi ambavyo ni feki. na wakubwa wote wanajua lakini wanaishia kuchekelea kwa kuwa wao haviwafikii.

    Sasa watanzania tunajiua wenyewe sasa. watu wengi wamekufa kwa typhoid, wizara inaishia kusema ohooomnakunywa maji bila kuchemsha. Sasa biashara ya maji imeingiliwa.

    Watu tulikuwa tunashangaa: maji ya kunywa tunachemsha, na mengine tunanunua ya chupa , iweje typhoid?!

    Asante kwa kutujulisha.

    ReplyDelete
  14. Hizi ndizo mada Zinazotakiwa kuwekwa hapa.Ahsante kwa kutuelimisha.

    Maisha Dar yako expensive kuliko Los Angeles,na hawa vijana sijui wanaishi vipi na hii ndio inaeleza kila kitu.

    ReplyDelete
  15. Lakini huu mtindo ulianza zaidi ya miaka 10 iliyopita. Mimi sinuni maji barabarani. Hata niknunua kwenye mgahawa naikazia jicho hiyo chupa kuhakikisha kuwa hata hao wa mgahawani na hawakununua barabarani.

    Pole sana. Bongo ni ujanja tu, watu wanaishi.

    Pengine suluhu inaweza kuwa kuweka utaratibu wa ukusanyaji makini wa chupa zilizokwisha tumika. wenye viwanda vya maji wanaweza ku-recycle hizo chupa/ plastic

    ReplyDelete
  16. florian rweyemamuFebruary 23, 2010

    Pole!!!
    shule nzuri siyo tu kwa walioko nje ya nchi bali pia na kwa sisi tuliyepo hapa Bongo Dar Es Salaam.

    Hii ndio bongo, kila mtu ni mjasiamali. Ujasiamali usiokuwa na uangalizi makini.

    pole tena.

    ReplyDelete
  17. bro misupu
    Dawa ni kustop hii biasha ya hao vijana maana mi sioni kijana amekuja mjini kuuza maji au korosha na ile kijijini nguvu kazi hamna tena unakuta ana simu ya mkononi. hivi huyu anatarajia kuendelea kwa kuuza maji barabarani. come on michuzi what are the chances of succeding in that business tatizo la nchi yetu viongozi bongo lala na kampeni ni nguvu ya soda. serikali itimue hawa machinga wote. hakuna kijana kuja mjini kuuza maji au karanga.
    Mdau Bongo forever

    ReplyDelete
  18. ivi wadau vipi kama ukimaliza kutumia chupa yako ya maji ukaiminya ilikupoteza ulemuonekano wake, mantiki yanngu ni kwamba sidhani kama hawa watengenezaji wa maji feki wanauwezo au utalaamu wa kurudisha hizi chupa kwenye orginal shape.

    ReplyDelete
  19. Asante kwa kutuelimisha ila kwa Mkuu wa Mkoa na Manispaa zote ni bora wawakamate hawa Vijana wnaouza maji mitaani kwani ni wauwaji. Sitawaonoe huruma kabisa hatua hizi zikichukuliwa.

    ReplyDelete
  20. ASANTE SANA MDAU WETU KWA GLOBU YA JAMII TAARIFA.HIVI KARIBUNI MHESHIMIWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ALIKIONA KIWANDA FEKI NDANI YA SOKO LA ILALA NA KUT0A AMRI KUWA KIWANDA HICHO KIFUNGWE.HII NI CHANGAMOTO KWA MAMLAKA ZA MANISPAA NA JIJI ZIOKOE UHAI WA WAKAZI WA JIJI NA WAGENI WOTE KWA UJUMLA.

    ReplyDelete
  21. Ujanja ni kuwahi, ndiyo ujasiliamali huo. Nimeipenda hiyo.

    Ni suala la mnunuzi tu kuwa makini. Usipende kununua vitu rahisi njiani. Bidhaa za aina hii ni nyingi sana siku hizi siyo maji tu.

    ReplyDelete
  22. Nashuru sana kwa taarifa hii na nawashukuru waungwana kwa kuchangia mada. nikiwa kama mhusika wa karibu wa kiwanda hicho cha kutengeneza maji ya uhai nimefurahishwa kwa kupata taarifa hii ambayo inabidi nikaifanyie kazi haraka sana.

    shukrani za dhati kwa aliefikisha taarifa hii na bila kumsahau mhusika wa blog hii.

    ReplyDelete
  23. Wadau wa globu ya jamii ni vema tuache utani kwenye masuala yahusuyo uhai wa binadamu.Mada iliyowekwa mbele yetu na mdau ni nzito na inamgusa kila mkazi wa jiji kwa njia moja au nyingine.Hapa ni jukumu letu kwa ushirikiano na mamlaka husika husika tufichue viwanda feki mitaani kwetu na kuomba kuanzia sasa askari wa manispaa waelekeze nguvu zao zote kwa wauza maji na bidhaa feki kwa ujumla.Wakati hayo yakisogea mbele tunaomba manispaa iweke matangzo mitaani na kupita na gari la matangazo kuwaonya wananchi wajiepushe na kipindupindu kupitia ununuzi wa maji feki.Hii itasaidia kuokoa maisha ya wakazi wa jiji na wageni wote kwa ujumla.

    ReplyDelete
  24. Kwa haraka haraka, nashauri nunueni Brand ambazo sio maarufu lakini zina qualiy...nina maana ambozo sio fast moving, hii issue AZAM wanaijua lakini wanadharau kwakua hawako Customer Care Oriented. Jamaa wako kienyeji sana...unakuta nafasi muhimu amepewa mtoto wa shangazi, tena amekimbia umande. Ila watoto wake Tajiri shule wamepiga za nguvu! kuna haja ya kumshtua huyu mzee..sijui kivipi....wadau changieni.

    ReplyDelete
  25. kwendeni zenu huko sa nyie mnataka watu wakale polisi??? mkipigwa loba mnalalamika, sasa leo hii mnauziwa maji mnalalamika tena, wakalibisheni makwenu basi vijana hao waje kula aaargh wabongo bwana!!!

    ReplyDelete
  26. Serikali na TSB mnafanya nini?

    ReplyDelete
  27. Hawa wafanyabiashara wadogo wadogo wa mitaani serikali ilifanikiwa kuwaondoa wote wakatiule mwanzo mwanzo wa utawala wa serikali ya awamu ya nne sasa cha kushangaza sasa hivi wamerudi mitaani kama kawaida,sasa mimi naona kama serikali inaona hao vijana wanawashinda nguvu (japo sitaki kuamin hivyo)na hapa tunaona wamefikia hatua ya kuhatarisha afya za watanzania basi waingie mkataba na MAJEMBE wa kila mwaka wafanye hicho kibarua.

    ReplyDelete
  28. huyo anon wa Feb 23 09:05:00AM ametoa a very good idea.

    ReplyDelete
  29. bebeni maji toka home kwenu jamani usimwamini mtu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...