Charge sheet

Mtangazaji wa TBC Jerry Muro akisindikizwa kuelekea chemba kusomewa mashitaka ya kula njama ya kutaka kupokea rushwa ya shilingi milioni 10 leo mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar
Jerr Muro chini ya ulinzi mkali mahakamani
ze fulanazzzz ilikuwepo pia... ry Muro akipoza koo baada ya kuachiwa kwa dhamana leo



Jerry Muro akiingia garini baada ya kuachwa kwa dhamana

Mshtakiwa mwenza na Jerry Muro, Edmund Kapama, akiondoka kwa furaha mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana leo

Mtangazaji wa TBC Jerry Muro na watu wengine wawili, Edmund Kapama na Deogratius Ngassa, wamepanda kizimbani mchana huu wakikabiliwa na mashataka kadhaa likiwemo la kula njama kutaka kupokea rushwa.

Mbele ya Hakimu Gabriel Mirumbe, Jerry Muro na washtakiwa hao wawili walishtakiwa kwa pamoja kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 toka kwa mweka hazina wa wilaya ya Bagamoyo aliefukuzwa kazi hivi karibuni na Waziri Mkuu kwa ubadhirifu Bw. Michael Wage.


Mwendesha Mashtaka wa Serikali Boniface Stancilaus akiwa na Mwendesha Mashtaka toka TAKUKURU Benny Lincolin wamedai mahakamani hapo kwamba mshtakiwa wa kwanza na wa pili pia wanakabiliwa na shtaka la kujipachika wadhifa ambao sio wao.

Inasemekana January 29, 2010 katika hoteli ya Sea Cliff washtakiwa walijitambulisha mbele ya Wage kuwa wao ni maafisa wa Takukuru wakati sio kweli.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama usitoe dhamana hasa kwa washtakiwa wa kwanza na wa pili kwa madai kwamba waliwahi kufungwa huko nyuma na kuwa kwao nje kutaharibu upelelezi ambao haujakamilika na bado unaendelea.

Hakimu alipowataka kutoa uthibitisho kwamba washtakiwa hao waliwahi kufungwa huko nyuma upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha hivyo dhamana ikawa wazi kwa m ashartia ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wataosaini bondi ya milioni 5 kila mmoja, ama kwenda rumande hadi Februari 12, mwaka huu kesi itaposomwam tena.

Jerry Muro na Edmund Kapama
walitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa.
Mwenza Ngassa amepelekwa rumande.


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. mkuu sijaelewa je, na Jerry kapelekwa au?

    ReplyDelete
  2. Wote 3 wamepelekwa mahakani (pamoja na JM) au ni wale jamaa 2? Nyosha kidogo kiswahili hapo.

    ReplyDelete
  3. Finally...there is a chance for the truth to come out.

    Network Engineer (NE)
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  4. There we are!
    The process is going to experience an extra high speed since Mr. Prime Minister has made some comments on the whole issue!

    ReplyDelete
  5. wote wana kosa moja sasa ni kwanini wasinyimwe dhamana wote? au kwa kuwa jerry maarufu wanamwogopa?

    nina mashaka sana na taaluma ya hawa mawakili wa serikali

    ReplyDelete
  6. HII MBONA KESI YA KITOTO KABISA. KULA NJAMA YA KUPOKEA RUSHWA? USHAHIDI MBONA NAONA HAKUNA TAYARI. HATA KAMA WALIONEKANA WAMEKAA NA HUYU MHASIBU UTADHIBITISHA VIPI WALIKUWA WANAOMBA RUSHWA?

    KOSA LINGINE UPANDE WA MASHITAKA TAYARI UMESHINDWA KUDHITISHIA MAHAKAMA KAMA HAWA JAMAA WALISHAWAHI KUFUNGWA. HAPA INAONYESHA HAWAKO MAKINI.

    UPUUZI MTUPU HUU.

    ReplyDelete
  7. Haiti mambo yalikuwa hayohayo Mwenyezi Mungu akakasirika, bado sisi!!! Huwezi kumuonea binadamu mwenzio kila siku. Chamoto kinakuja.

    ReplyDelete
  8. Jery Muro niliwahi kukutana nae yeye akiwa kama muandishi wakati ule akiwa ITV na mimi kama mtoa habari(PRO)wa ofisi fulani nya umma ki ukweli ni mtu anayependa kunata na kujisikia na hata kwangu alinitishia kuwa atanibomoa kwenye media iwapo sitompa taarifa anazozitaka ambazo kwa mimi zilikuwa bado kutolewa kwa PUBLICK kwani hazikuwa zimethibitishwa..sasa mimi siwezi kumtetea kwenye hilo la kudai rushwa.Kana kwamba haitoshi akiwa tayari yupo TBC alimuhitaji mkuu wangu wa kazi ahudhurie kwenye kipindi chake cha USIKU WA HABARI mimi nikamtaka afuate utaratibu ikiwemo kuandika barua ili iwe kama kumbukumbu ili isije ikaonekana bosi wangu kajipeleka mwenyewe kwani waziri wetu ni mkorofi yeye Muro hakukubaliana na hilo na akaenda mabali zaidi kwa kumpigia mkuu wa taasisi yetu kuwa sisi tunamsumbua na tunakwamisha TBC ambayo ni TV ya Serikali kupata habari hali iliyopelekaea mimi na mkuu wangun wa section kufokewa na kukaribia kufukuzwa kazi....hapo vipi wadau..huyo ndie Muro nimjuae mimi.

    ReplyDelete
  9. Kweli Nchi yetu ya Tanzania haina haina mwelekeo,Nahasa viongozi wetu.Mmi nashindwa kuelewa kama huyo mweka hazina wa wilaya kafukuzwakazi na waziri mkuu, kwa ubadhirifu yuko nje na hajachukuliwa hatua yoyote ingiwa inajulikana makosa yake kuwa ni mbadhirifu wa mali ya umma.Inakuwaje mwandishaliyotoboa siri ya ubadhirifu ndio anaefunguliwa kesi.Kikwete angalia upya uongozi wako.

    ReplyDelete
  10. Hivi mbona mnakuwa wagumu kuelewa? hata video pia hamkuiona? wote watatu wametinga kwa mbele ya pilato!na kuhusu dhamana jerry na mwingineo wamepata dhamana., isipokuwa mmoja tu ambaye hakutimiza masharti ya dhamana. tuwe waelewa ndugu zangu!

    ReplyDelete
  11. Abiola wa Kuchovya, Mikanjuni- TangaFebruary 05, 2010

    Jamani, huyu Jerry Muro amedhihirisha kuwa anaichukia rushwa hadi amenunua pingu ili akitokea mtu anayetaka kumpa rushwa basi amfunge hapohapo kabla hajampeleka kwenye vyombo vya juu vya sheria. Teh!! Teh!!!! Teh!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. Hiyo HOSPITALI ya Sea Cliff walipokutana walienda kuangalia mgonjwa au nani alikuwa anaumwa. Sijaelewa uncle Michu.

    ReplyDelete
  13. Kafungwa Papii Kocha hiv hiv kimasihara ila Kaka Mithupu Hii nchi inaendeshwa cjui kma sie Vipofu ila Ipo siku wajue Bongo Patachimbika JM sie twasikiliza tuuu hawatujui wachaga

    ReplyDelete
  14. Ankal Michuzi jamani ni "Hotel ya sea cliff" na siyo Hosptali ya sea cliff!!!!

    Naomba u-edit hiyo taarifa.

    ReplyDelete
  15. we are waiting till the end...

    yani atake pokea rushwa kwa nguvu,ilhali katoka kuwaumbua polisi kwa rushwa?????

    kesi za EPA,RICHMOND,MEREMETA,IPTL,LOLIONDOnk akhaaaa zimepowaaaa sijui zitafikia mwisho?

    anyway lets see

    ReplyDelete
  16. AISEE.. SIENDI TENA SE CLIF KUMBE HAKUNA PRIVACY NAMNA HII! NI HATARI KWA MAISHA HASA UKUTILIA MAANANI MAMBO YETU..

    DUH!

    ReplyDelete
  17. This country is as corrupt as Haiti was. No wonder even the state house was not spared! Haitian president was forced to work from police station as make shift state house. Tanzania is evil like Haiti was!

    ReplyDelete
  18. Hivi kwa nini mapolisi wote they r UGLY look at that KOVA ..KAVA whatever his name is .MAHITA..wote yaani is it a job requirement ...lol

    ReplyDelete
  19. The FULANAZ na Video camera leo. Sio Picha mnato/mgando tena

    ReplyDelete
  20. Kaka Michuzi, Hongera kwa kutuletea LIVE sakata la Jerry Muro, Hawa Polisi wanampeleka mahakamani JM kwa kutaka kupokea rushwa.
    1. Je wale askari ambao wamenaswa wanapokea mbona hawajafikishwa mahakamani? au wanatuzuga ili tusawasahau askari waliochukua rushwa.
    2. Sakata la JM likiisha tunataka na polisi wote walionaswa nao wafikishwe mahamani.
    3. Unko Michu, Mungu akubariki kwa kutuhabarisha LIVE, ni kama naangalia CNN Breaking Nyuuuzzz

    ReplyDelete
  21. Watu hawajaelewa kinachoendelea hapa. JM akifungwa kesi ya mapolisi hakuna tena. Kwani shahidi atakuwa jela!

    ReplyDelete
  22. jamani wadau niko nje ya topic naombeni tu muingie kwenye blog ya "dina marios" mscroll zile picha kwa upole then mtaona ze fulaz ikiwa imeanikwa haki ya nani ile ni ya ankal tu one and only!! du nimejichekea weeee

    ReplyDelete
  23. Pole Sana Jerry!
    Anonymous USA

    ReplyDelete
  24. ETI,

    KWA MUJIBU WA VIDEO ULIPOST SIKU YA NYUMA, ZILIONESHA JERRY MURO AKIELEZA KUWA KOVA ALIITA PRESS CONFERENCE YA KUDAI JERRY AMEPOKEA RUSHWA HATA KABLA YA YEYE NA VIJANA WA KOVA KUFIKA CENTRAL POLICE.

    ANGALIA, MAELEZO HAYO YA MAHAKAMA YANASEMA JERRY ALIJIFANYA MFANYA KAZI WA PCCB, HAPO HAPO WALIOMKAMATA JERRY SIO WATU WA PCCB, NA HAO WALIOMKAMATA JERRY KWA KOSA LA PCCB NDION WALIOKATAA KUFUATLIA SUALA LA JERRY KUTAKA KUPEWA RUHSWA YA TSH 150 MILLION NA KUMTAKA AWATAFUTE PCCB.

    HAPA KUNA KITU, MI SIPO UPANDE WOWOTE ILA NATAKA HAKI ITENDEKE.

    KOVA ALISHINDWA KUPROVE SUALA KA JERRY KUPOKEA UA KUTAKA KUPOKEA RUSHWA NA BADAL YAKE AKANZA KUSEMA MAMBO YA PINGU NA BASTOLA YAKE AMBAYO KWA JERRY ANADAI NA KUWAKILISHA VITHIBITISHO VYA UHALALI WAKE.

    VIPI JAMANI?

    ReplyDelete
  25. Muro amefoji risiti za pingu toka Mzinga. Why?
    Soma: http://thecitizen.co.tz/newe.php?id=17202
    As this unfolded in Dodoma, the saga took a twist in Dar es Salaam with the Tanzania People�s Defence Forces Mizinga section in Upanga refuting claims that handcuffs could be sold to individuals.

    An official told The Citizen that handcuffs, similar to the one allegedly bought by Mr Muro could not be issued to individuals other than the police and prison personnel.

    "We do not sell handcuffs here. It is easier to grant a gun if all procedures are followed to warrant an individual to own one, but not handcuffs," explained an official at the unit who did not want to be identified.

    On Wednesday, Mr Muro displayed a receipt to a section of the media to show that he had bought the handcuffs from the Mizinga agency.

    ReplyDelete
  26. Kwa wale mnaolalama kiswahili chetu kizuri ni lugha yetu ya kiafrika na Taifa.
    Kwanini hizo court documents za serekali ya jamhuri ya muungano zimeandikwa kiinglish?

    ReplyDelete
  27. tATIZO LETU WABONGO TUNA UJINGA WA KUPENDA MAANA HATA MKAPA ALIMFUNGA MPAKA WA WAZIRI WAKE AU SIJUI NIKATIBU YULE ILI KUONYESHA UMMA WA WATANZANIA KUA ANACHUKIA RUSHWA, KUMBE MAMA YANGU YEYE NDIO ALIKUA MLA RUSHWA NAMBA MOJA, KAINGIA IKULU MILIONEA AMETOKA IKULU AKIWA BILIONEA. KWA HIYO HATA HUYU MURO ANAWEZA AKAWA NDIO HAOHAO TU. TUSUBIRI MAHAKAMA ITAKAVYOAMUA.

    ReplyDelete
  28. Hii kesi ni ya "Blackmail" na sio rushwa per se. Ninachofahamu blackmailing ni kosa katika nchi nyingi, sijui TZ.

    ReplyDelete
  29. Jamani this is to much now Jerry Muro part ngapi tutazikia mpaka Pinda kaingilia ndani..wanaacha kufuatilia EPA,BOT walivyospend mabillion kujenga nyumba zao eti Jerry Muro pt 1,2,3 etc..Pls kuna vitu vingi sana vyakufanya sio mkalie na topic ya JM..

    ReplyDelete
  30. ok lakini pingu kutembea nayo kwenye gari ni kwa kusudi la kujilinda tena au mzee wa mapenzi kila kona watu kibao!! Kweli bongo tambarare maana kama pingu hairuhusiwi maduka ya silaha ya nini tena mmewapatia vibali?

    ReplyDelete
  31. Hati ya mashitaka haimtaji Jerry kuhusika na kosa linalotajwa, hivyo anaburuzwa tu na hahusiki kwa kuwa Particulars of offence inawataja watu wawili tu na si Jerry.

    ReplyDelete
  32. Hivi ndo byebye Jerry Muro. Bongo si yenu kudadeki. Na ni fundisho kwa wote mnaojidai wapigania haki za wasio binadamu ndani ya Bongo

    Imetoka hiyo hairudi mwana.
    Wadau tumchangieni huyu jamaa please apate wakili mzuri. Hivi wakili wake nani au ndo kimbuzimbuzi?

    ReplyDelete
  33. NI KITU CHA KUSHANGAZA KABISA NA AIBU KUU MBELE YA UMMA WA WATANZANIA NDANI NA NJE YA NCHI YETU TUNAOFATILIA KESI HII TUNAPOONA WAENDESHA MASHITAKA WAKISHINDWA KUWA NA(VIELELEZO)UTHIBITISHO WA JAMBO AMBALO NI MUHIMU SANA KATIKA UTETEZI WA HOJA YAO KUHUSIANA NA DHAMANA YA WATUHUMIWA WAWILI HII INANIFANYA NIWE NA WASIWASI KAMA KWELI WATAWEZA KUZITETEA HOJA ZAO ZA KISHERIA WIKI IJAO KATIKA HII KESI AMBAYO MEDIA ZIMEIWEKA KATIKA KUNDI LA "HIGH PROFILE CASE".
    KULINGANA NA HILI SWALA NIMEGUNDUA MAMBO MAKUU YAFUATAYO:-
    1:- KAULI YA WAZIRI MKUU KUTAKA UCHUNGUZI UFANYIKE HARAKA IMEWAFANYA WAWAPELEKE WATUHUMIWA MAHAKAMANI HARAKA BILA KUANDAA VIELELEZO MAALUMU AU;
    2:-WAENDESHA MASHITAKA AMA WANAFANYA KAZI KWA MAELEKEZO YA WAKUBWA WAO AU KWA LUGHA NYINGINE, KUSHINIKIZWA NA ELIEZER FELESHI(DPP)AU NA SULEIMAN KOVA(DSZC)KWA VILE KAMA WANGEKUWA WAKO INDEPENDENT WANGEOMBA MUDA ILI KUKUSANYA VIELELEZO AMBAVYO NI MUHIMU SANA KATIKA KESI YEYOTE AU;
    3:- SIO WAELEWA VIZURI WA SHERIA AMBAZO WANATAKIWA WAZITAFSILI MAHAKAMANI WIKI IJAYO. from Ng'wanidaso

    ReplyDelete
  34. Kama nchi yetu ndiyo iko hivi, basi kuna siku Kagame atatupiga na ataichukua nchi yetu. Ukitaka kujua kama nchi ni dhaifu angalia nidhamu ya wanajeshi na nidhamu viongozi na watendaji wa serikali.

    Watu kama Kagame au Museveni wanavyoshuhudia matukio haya, wanasema "yes, they are now in the most vulnerable state".

    Nikiwa kama mwanajeshi wa kukodiwa mstaafu, "mercenary"; ninaelewa ninachokisema; na hii leo ni tarehe jumamosi 6th feb 2010 ndiyo nimesema mneno haya. Kwa wenye akili timamu wekeni kumbukumbu ya maneno yangu.

    ReplyDelete
  35. Kama Pingu haziuzwi zinafanya nini dukani?

    ReplyDelete
  36. Hivi, kama mfanyakazi wa TBC, Jerry Muro si mwajiriwa wa serikali? Mbona serikali hiyo hiyo imemtupa? Tido Mhando uko wapi kumtetea kijana wako? Waziri Mkuchika mbona kwa hili umekuwa bubu?I guess ndo bongo yenyewe hiyo...serikali yako haikujali bali inakudis kama ifuatavyo!

    ReplyDelete
  37. Haingii akilini,kama pingu zingekuwa ni maalumu kwa jeshi la polisi au kwa makampuni ya ulinzi zisingekuwa zinauzwa madukani. Hata wakati wa maonyesho ya saba saba pingu zisingekuwa zinauzwa kwa raia wa kawaida na watu kibao walijipendelea hizo pingu.
    Tuwaulize wao kwa nn wanaziuza kwa raia? halafu badae ndio tutajua kwa nn raia wanazinunua.

    Mdau Dar

    ReplyDelete
  38. Inawezekana Pingu zinauzwa madukani lakini kwa kuwa kakutikana nazo jery Muro wanataka wambabatize nazo kuwa ni kosa, hapo watakuwa wamechemka,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...