Globu ya Jamii itatoa ze fulanazzz 100 kwa wadau mia wa mwanzo watakaokuwa katika ulingo wa wadau wa milioni 8, hesabu ambayo itatimia muda si mrefu ujao (angalia takwimu chini kabisa kuumeni kwako).
Hii ni badala ya kumzawadia mdau mmoja mmoja. Hivyo mdau kaa chonjo mara tu hesabu itapogota 8,000,000 lete haraka jina na anuwani yako utumiwe ze fulanazzz ya Globu ya Jamii kama inavyoonekana hapo juu. Hakuna malipo na utapoleta jina na anuani utatumiwa popote ulipo ulimwnguni...
Sina uwezo kwa kumshukuru mdau mmoja mmoja kwa kampani baab'kubwa mnayotoa kwa Globu ya Jamii, ingawa iko siku panapo Majaaliwa kila mdau atapata zawadi.
Hao wataobahatika naomba wajione na wajulikana kuwa ndio wawakilishi wa wadau wote ambao nawapenda na kuwaheshimu sana kwa kutembelea Globu ya Jamii kila kukicha.
Bila ninyi nyote Libeneke hili lisingefika hapa.
Asanteni sana sana sana....
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kesho panajaa hapa nakwambia, ngoja nikae mkao wa kula nione watavyobanana na kuanza kulalama.
    Senkyu Ankal Mechoodhe kwa dhawadi.

    ReplyDelete
  2. naona vijaba wanauza sura !!sorry afagiliwi mtu hapa. yafagiliwa pesa

    ReplyDelete
  3. ebwanaa ehh globu letu la jamii na mkuu wetu wa wilayaaa ya nahiii!we mwaga pambaz hizo mkuu maana summer ndo inatupiga chabo kwa mbalii.

    mdau kigali makazi boxini

    ReplyDelete
  4. Mr M.Kobole p.o.box 8769 Dar.'nasubiri the fulanaz.

    ReplyDelete
  5. mjengwablogspot.comFebruary 27, 2010

    Kaka ngoja na mie nijaribu bahati yangu safari hii. HONGERA KWA UTUMISHI MWEMA KWA JAMII.
    Maggid
    Iringa.

    ReplyDelete
  6. Si kila mtu atataka kukutumia email na address yake......jinsi ya kushiriki?

    ReplyDelete
  7. Sifahamu! hao wote watakao pata watakuwa washindi wa milioni 8 tu, au kuanza 8,000,000-8,000,001-8,000,099.

    Msaada kwenye tuta kwa hilo!

    ReplyDelete
  8. NA WAKIPATA FULANA HIZO WAPIGE NAZO PICHA TUWAONE SURA ZAO.

    ReplyDelete
  9. ... Tunaruhusiwa kufua na kuvaa tena? au tukishafua ndo imetoka?

    ReplyDelete
  10. ankal mimi sitaki kushinda wala nini hebu plz nipatie zefulanaz ya bure bila jasho mdau magharibi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...