akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa mnikulu Bwana Rajabu Kianda aliyefariki jana jijini Dar es Salaam.Marehemu Kianda anatarajiwa kuzikwa kesho(tarehe 9/2/2010) nyumbani kwao Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro.
akimfariji Bi.Khadija Kianda ambaye ni mjane wa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa Mnikulu ambaye alifariki dunia Jumapili jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam kuifariji familia ya marehemu ambaye anatarajia kuzikwa huko Kihurio Same,Mkoani Kilimanjaro.Pembeni ni Mama wa Marehemu Bi. Mwanahawa Samuel.
Mama Salma Kikwete akimfariji Bi.Khadija Kianda mjane wa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa mnikulu kufuatia kifo chake kilichotokea jumapili jijini Dar es Salaam.

Angalizo: Mnikulu ni kama mratibu mkuu anayesimamia
shughuli zote zinazofanyika Ikulu kama vile dhifa, kupokea wageni wa ndani na wa nje kwa itifaki zote. Ni kama meneja wa Ikulu. Kwa kimombo ni State House Comptroller.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Mnikulu ni nini au ni cheo gani, msaada plz

    ReplyDelete
  2. duh,na uswahili wangu wote yaani sijawahi kulisikia hilo neno hata siku moja.Ndio maana yake nini mnikulu? does it mean someone working in ikulu?

    ReplyDelete
  3. Poleni sana wafiwa. Michuzi tunaomba ufafanuzi mnikulu ni nini hasa? Nadani kama inahusiana na mambo ya ikulu ila nini hasa?
    Mzozaji

    ReplyDelete
  4. IbhombanguluFebruary 08, 2010

    MNYIKULU- Hili ni neno la kinyamwezi lilikokuwa likitumiwa wakati ule wa utawala wa kitemi, Mtemi Mirambo wa wanyamwezi alikuwa na wasaidizi wake, hawa walikuwa wakiitwa "Wanyikulu" kwani nyumba ya mtemi ilikuwa ikiitwa "IKULU" sehemu ambapo maamuzi ya vita na mipango yote ya kiutawala inafanyikia. Hivyo basi sisi wanyamwezi tulikuwa tunawaita wasaidizi wa mtemi kuwa ni "WANYIKULU" ambao walikuwa na dhamana ya kuhakikisha mambo yote ya kiutawala yanaenda kama kawaida wakisaidiwa na "MAKATIKILO"-hawa ni kama wajumbe wapeleka habari.

    ReplyDelete
  5. Ankal! shukrani sana kwa kutusaidia maana ya neno hilo!maana
    hata mjomba Mpoto nae aligonga ukuta kwa kutolijua neno Mnikulu

    ReplyDelete
  6. MDAU WA ELIMUFebruary 08, 2010

    POLENI SANA FAMILIA,NAWAFAHAMU TOKA KIPINDI KILE MPO SINGIDA PALE MZEE NA MAMA WOTE WALIKUWA NI MARAFIKI WA FAMILIA YANGU KULE,NIMEPOKEA KWA HUZUNI SANA KIFO CHA MZEE WETU.
    MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEPA PEPONI.

    ReplyDelete
  7. Jamani Mnikulu ni State House Controller kwa lugha ya ungenge. Yaani shughuli yeyote Ikulu haiendi bila idhini ya Mnikulu.Wanikulu waliopita ni F. Kuzilwa na A. Itatiro

    ReplyDelete
  8. Inakuwaje nyie vijana ambao mnajifanya mmeenda shule hata maana ya mnikulu hamjui? In english anaitwa State House Comptroller. Huyu ndiye msimamizi wa masuala yote yanayohusu house keeping ya ikulu kama vile mahitaji ya chakula, vinywaji nk kwa matumizi ya Rais binafsi au na wageni waalikwa pale ikulu. Aidha mandhari ya kwenye bustani, usafi wa mazingira ni kazi yake. Ndiyo maana utaona sikukuu ya idd au pasaka/xmas misaada inayotolewa na Ikulu utamuona Mnikulu ndiye anaetoa kwa niaba ya Rais.

    ReplyDelete
  9. hahaha hapo juu mnikulu eti ikulu,IKULU NI HEKALU NDANI YA MARAHA YOTE MZEE HADI VIMADA TOP TEN NDIO WANAINGIA WAGENI WANABULUZA KAMA KAWA,

    ReplyDelete
  10. Huyu bwana alipenda sana kuangalia maslahi ya waandishi wa habari wakati wa safari za rais mikoani na hata nje ya nchi. Binafsi nimehuzunika sana na msiba huu. Nakumbuka nilikuwa na-cover ziara ya rais Kigoma two years ago na tulipofika Kasulu nilikosa mahali pa kulala. Rajabu alihakikishia nimepata sehemu ya kutia mbavu. Go in peace my brother. Mdau - Daily News

    ReplyDelete
  11. ivi nyie uko juu mnaouliza maana ya neno hili ina maana HAMUONI maelezo apo chini ya izo picha?wanga tu

    poleni wafiwa mungu awatie nguvu sana na muishi kwa amani wote

    ofkoz kiswahili hatukijui kbs ata me sijawai sikia ili neno dah!adi aibu sana!!!ila neno limetulia

    ReplyDelete
  12. Chiku, Amina, Hawa na Zainabu poleni mungu awape nguvu ktk wakati huu mgumu.
    Na nyie hapo juu balada ya kutoa pole mmekaa mnang'ang'ania kujua maana ya neno mnikulu wakati michu keshawaelezea.

    ReplyDelete
  13. this shows that he was loved more than anybody,If we love him too, we have to stay strong while having peace and faith that one day we will meet him. poleni wafiwa wote lets stay strong.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...