Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi waandamizi wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka hayati mzee Rashid Mfaume Kawawa muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati hiyo mjini Dodoma leo asubuhi.

Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba na Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ni sawa lakini ningependa ajitayarishe kwa masuala haya yafuatayo iwapo atafanikiwa kuupata hicho anachokitaka
    a)Jee anaweza kuondosha umaskini miongoni mwa wananchi
    b)Jee anawezake kutokomeza rushwa
    c)atawezaje kuigeuza mahkama ni nyumba ya haki
    d) atawezaje kusimamia haki na usalama wa wananchi ambapo kila siku wananchi wanauliwa barabarani
    e)Jee ataweza kutokomeza culture ya wananchi kuwa kuonewa,rusha,kuingia madarakani lazima utoe kitu kigodo ili upite kupata eg ubunge, uwakilishi,etc ni vitu vya lazima na wananchi wenyewe wamejikubalisha waonewe.
    f)huduma bora mahospitalini, ufanisi kazini,job creation ili wananchi wapata cha kujishughulisha na kuacha omba omba.
    Mi fikra zangu Governmet of unity is nothing kama hakuweza kuwa na mikakati yakuondosha hayo hapo juu.
    kwani hayo ndio makero ya wananchi na sio vyenginevo
    wako,
    mwanaharakati wa maendeleo

    ReplyDelete
  2. Nyerere ni baba wa taifa, na wala si baba wa CCM, na ni matusi makubwa sana kwa baba wa taifa kutumia jina lake kufanyia kampeni za kuendeleza wizi, uhuni, urichmond, ulowasa, ubalali, ubenondulu, uchenge, uEPA na upuuzi mwingine.

    ReplyDelete
  3. Kila la kheri Kamati Kuu.

    Maina A Owino.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...