Brother Michuzi kwanza naomba nikupongeze sana kwa blog ya jami.
Bwana Michuzi kwa kweli kuna kitu kinanikera sana na sijui jinsi ya kukabiliana nacho. Nilikuwa najenga nyumba yangu hapa katika eneo la Mlalakuwa na kabla tu ya kumaliza akaja jamaa mmoja na kuanza ujenzi wa bar kubwa sana ghafla na kwa spidi sana. Sasa hivi bar imeshafunguliwa na inasemekana kapata kibali toka manispaa ya Kinondoni.
Baada ya kufatilia kwa muda mrefu na serikali za mtaa tukagundua kuwa kumbe mwenyekiti wa serikali za mtaa huwa anapewa offer pale bar na kwa kuwa ni "chapombe" huwa anazima attempt zote za kutaka kuzuia bar hiyo isipige mziki.
Sasa kama unavyoelewa adhari za bar kweli huu ni uungwana? Na huko manispaa ya kinondoni kweli mambo wanayoyafanya wanadhamira kweli moyoni mwao. Jamani bar kuwekwa kwenye makazi ya watu adhari zake si zinajulikana.
Hebu angalia pale Kona bar Sinza palivyoharibika achilia mbali mifano mingine mingi iliyopo. Tafadhali bro Michuzi hebu angalia jinsi ya kuanzisha mjadala huu ili tuweze saidiwa, namna hii watu tunajawa na chuki ambazo si nzuri.
Wako Mdau Philip
---------------------------
naunga mkono kero za mabaa
Ningependa kuunga mkono kero za mabaa katikati ya makazi hasa maeneo ya "high density" maana nyumba ina pakana na nyumba mita chache tuu... iliogeuzwa baa au siku hizi zinaitwa "club" wanaopata vibali vya kukodisha kumbi hata iwe ndogo vipi. Mradi inakodishwa na anaekodi atapiga mziki anavyo taka.
Kuanzia kitchen party, graduation, kipaimara na kuendelea. Kelele za maadili ya watoto na vijana kuporomoka inatia kichefu chefu, nani anaeporomosha maadili hayo na malezi mabovu? swali hili lina upana sana ukizingatia hayo mabaa na club ziliopo katikati ya maeneo ya makazi wala sizungumzii nyumba ziliopo labda main road ama barabara kuu... naongelea nyumba ziliopo ndani ndani kabisa.... wanaotoa vibali hawalijuwi hili kwani wao hawakai jirani na kero hii....
watoto wao wanasoma boarding, wazazi ama wazee wao wamejengewa nyumba nzuri katika mashamba yao wako mbali na kelele hizi.....
Huku mitaani vijana hasa wanafunzi wanaumia sana eti kiwango na elimu kimeshuka, ni wakati gani mwanafunzi atapata utulivu wa kujisomea nyumbani wakati kuna muziki mkali unapigwa siku ya Jumatano au alhamisi, na jumamosi yake na kuamkia jumapili, je jumatatu mwanafunzi huyu anakitu kichwani? Hivi kweli tun mazingira ya kutosha kuwapa wanafunzi chachu ya kusoma kwa bidii? kwakweli uchoyo na ubinafsi wa viongozi wetu katika kila ngazi unarudisha nyuma maendeleo ya wananchi wengi ni wale wachache waliobahatika kupata vyeo ndio familia zao zitapanda kimaisha.
Inavyoeleweka hao wanaotaka kuendesha biashara katikati ya makazi ambao wanapiga muziki wanatakiwa kuweka "sound proof" pamoja na kuhakiksha kuna staha ya aina fulani ili mazingira yanayo mzunguka yasiathirike kwa shughuli hizo ni aina ya kuwalinda vijana na watoto. Lakini wapi hii ni Bongo watu wenye uwezo wanafanya wanavyotaka sheria zinapindishwa kwa manufaa ya yule aliopo katika maamuzi...
Kuna baa zingine zimejengwa juu ya mitaro ya kupitisha maji machavu, kama baraza la baa halitoshi basi Bossi anafunika mtaro kwa mbao, viti na meza zina pangwa na shughuli zinaendelea kama kawaida, hapo makopo ya vinywaji, viplastik ya konyagi, ma plastiki ya chips na uchafu mwingine yanatupwa hapo hapo mtaroni na wateja au hata wahudumu, kazi mvua ikinyesha, balaa ya magonjwa ni ya wale wanaoishi jirani.
Ndugu zangu imeshakuwa hulka ya wabongo kukubali mazingira ya maisha kama haya na kuvumiliana hata kama yanaturudisha nyuma kimaendeleo, kiafya na kwa ujumla kimawazo maana tumeishiwa hata na mawazo endelevu..... ukipiga kelele wewe ni jirani nuksi, au utasukiwa jambo.... tutafika kweli? ninayo mengi lakini leo nitaishia hapa
Mdau MZ

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. ANKAL NANIHIIII. NAKUMBUKA NABII MTAKATIFU YOHANA MASHAKA ALIWAIGI KUANDIKA ATIKO MOJA MURUA SANA KUHUSU HUU UFISADI. TUNAOMBA UIRUDISHE ILI WADAU TUICHANGIE UPYA. KUNA MENGI SANA ALISEMA KUHUSU ILI TATIZO, NAOMBA TUKISHAMALIZA URAIA WA NCHI MBILI UTUFUNGULIE ILE THREAD UPYA MKUU. HESHIMA MBELE, VIJANA LAZIMA TUPIGE KELELE

    ReplyDelete
  2. Mdau
    Maoni yako yanaonekana kuwa 'genuine'..lakini kwa ushauri wa bure,kuna vyombo vya serikali ambavyo huwa vinashughulika malalamiko kama hayo...kama ngazi ya serikali za mitaa iko corrupted basi nenda hatua za juu zaidi (sina uhakika kama ni kwa diwani,mbunge,mkuu wa mkoa nk)upeleke malalamiko yako officially....
    Ila dah pametulia kimtindo pale...

    ReplyDelete
  3. Tanzania kuna matatizo ya kila aina.tutakapoanza kukatana mapanga kama mkoa ule waliochinjana jana ndoo tutakuwa na akili...corrupted system tuliyokuwa nayo ni mbaya sana...wapo juu ya sheria..hapo mkuu,umeumia!!!!pole sana.

    ReplyDelete
  4. wewe filipo acha chuki binafsi!
    ulitaka wewe ndo ukapewe hizo pombe za bure? kwani wewe ni m/kiti wa serikali ya mtaa?
    au unataka baa ifungwe waje wale kwako?

    ReplyDelete
  5. Hivi wewe unataka pombe ziuziwe wapi? Raha ya pombe unywe jirani na nyumbani ili ukilewa unamuita mama anakuja kukubeba. Pole sana kwa tamaa za kukaa maeneo ya starehe, njoo huku Mbezi, Kimara unakuta mtu ana ekari 2 peke yake. Hata ukijenga bar jirani na kwake wala hasikii hata chembe ya kelele. Lete biaaaaaa

    ReplyDelete
  6. nyie badala ya kuanzisha mijadala ya kitaifa mnahangaika na watu wadogo wanaojitafutia riziki. mnafikiri wateja wa baa ni kina nani? ni lazima baa zijengwe karibu na makazi ya watu kwa sababu wanywaji ni watu.

    au mnataka bar nazo zitengewe maeneo kama viwanda? bar zote na kumbi zote zikihamishiwa let sei kipawa, mtu wa kinondoni atenda kunywa??? mtu akishalewa kama hayupo karibu na nyumbani vibaka watamwacha?

    yaani mtu kwa sababu ya imani yako binafsi ulokole/uswaliina unataka jamii nzima ipate shida?

    hayo maharusi, vipaimara n.k ni watu huandaa, kumbi za starehe zikijengwa mbali je ni kila mtu ana gari?

    mtu mmoja unataka usababishe wateja 50 wataabike? au washerehekeaji 300 wa harusi washindwe kusherehekea?

    Jadilini hoja kama nyumba 2 za vigogo BoT kugharimu pesa nyingi za kodi ya walalahoi huku gharama hizohizo zingetosha kuweka vitanda hosipitali zote za dar es salaam, na vigogo wa BoT wakakaa kwenye nyumba za kawaida na wasife. kama hawataki waache kazi tukazifanye sisi.

    JE HII NI HAKI?
    Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete imehalalisha na kukubali matumizi
    ya karibu shilingi bilioni 3 za kitanzania kujenga upya nyumba mbili kwa
    ajili ya maisha ya kifahari ya Gavana wa Benki kuu na manaibu wake..
    Wamefanya hivyo kwa sababu mikataba ya watumishi hawa inawataka wapatiwe
    vitu hivyo, vinginevyo wangegoma kufanya kazi BoT na kuishtaki serikari.
    Mastahili ambayo yanazidi yale ya Magavana wa Benki kuu za Uingereza na
    Marekani!
    Hapa chini ni picha zilizochukuliwa katika wodi ya kina mama
    waliojifungua wakiwa wanapumzika pale Hospitali ya Temeke. kama
    utakumbuka.... hali hii ndiyo ilimfanya mwanamapambo Naomi Campbell
    kutokwa na machozi alipotembelea Hospitali hii.

    SWALI: NANI ANASTAHILI ZAIDI, KATI YA GAVANA WA BENKI KUU ILIYOGUBIKWA NA
    UFISADI NA KINA MAMA HAWA NA WACHANGA WAO? TAFAKARI..................

    jadilini hoja kama:
    IPTL
    RICHMOND
    DOWANS
    SAKATA LA RADAR
    GHARAMA ZA MINARA PACHA YA BoT
    GHARAMA ZA NYUMBA YA UBALOZI NCHINI ITALIA (kumbuka kesi ya Prof. Mahalu),
    MISHAHARA NA POSHO ZA WABUNGE - bado wanaongezewa fedha za maendeleo jimboni (je majimboni zinaonekana?). wanazo pia pesa za kila mwezi kwa ajili ya chai ofisini kwa mbunge. wanajaziwa mafuta kwenye mashangingi yao!!!
    PESA ZILIZOCHOTWA BoT KAMPUNI KAMA
    KAGODA
    RUSH HARSH
    NJAKE
    MEREMETA
    DEEP-GREEN
    n.k

    Kitendo cha baadhi ya vigogo kujiuzulu na mikataba ikasitisha ni kwamba makosa yapo. Je, wakosaji ni kina nani??? Mbona hawachukuliwi hatua?
    Ni hatua gani zilizochukuliwa dhidi ya watendaji wa serikali waliolisababishia taifa hasara zote hizo?

    Kwa hiyo mtu achote pesa halafu ajiuzulu? Huu ndio mtindo???

    Hata hili bunge lija haja ya kuwepo kama wabunge wanaionea haya serikali?

    Ni kitu gani cha maana walichokifanya??

    Kazi yao ni kutunga sheria za kuwabana wananchi?

    Inawezekana hizi bia zilizopanda bei ni mpango umesukwa kuwawezesha watu/chama fulani kipate pesa za kampeni!!

    Je, tufanye nini?

    Hakuna haja ya kuwarejesha madarakani viongozi wa namna hii.
    Tupige kura lakini tusiwapigie hawa mafisadi kura.

    Tukiona matokeo ya uchaguzi yametofautiana na matarajio ya wapiga kura ni kuanzisha kunji; kama noma naiwe noma!

    ReplyDelete
  7. Haya mambo ni mazito sana. Pia matatizo ni mengi sana. Mimi naona wakati umefika wa Wakuu wote wa wilaya zote za Tanzania kuwa na siku maalum kila week ili kusikiliza matatizo kama haya. Tukumbuke enzi za Mhs Mpendwa Raisi Mustaafu Mwinyi. Yeye aliamua kutoa hata ruhusa ya kumuona directly katika matatizo kama haya hasa viwanja na nyumba.
    Kwa mawazo yangu naomba hao wakuu wa wilaya wafanye hiyo kazi kwa masharti yafuatayo:
    1. utatuzi wa maswala kama haya ufanyike na kumalizika ktk week 2 tu na si zaidi (hapa tumukumbuke hayata mpendwa bwana Sokoine)
    2. Waasirika waruhusiwe kupata maelezo pamoja na msimamo wa serikali ya mji unaohusika.
    3. Waasirika waungane ili waunde kamati ya kuwasaidia kupeleka matatizo yao ktk mgazi za juu (hii ni kuondoa confrontation kati ya mwenye baa na mtu mmoja).
    Mwisho, ninakubariana na huyu Mdau kuwa ubinafsi umezidi kuliko kipimo.
    TUSIKATE TAMAA KWANI NI SISI TU TUTAKAO BADRISHA HAYA MAMBO!!!!

    ReplyDelete
  8. Mi na-support hiyo hoja, hao wanaoweka bar na kupiga makelele kwenye makazi ya watu jamani wasipewe vibali kwani ni kero mtindo mmoja. Bar zingekua mabarabarani na si mitaani.

    Najua serikali ina uwezo wa kuwanyima wafanyabiashara wapya wa bar leseni km vile ewura kwenye vituo vya mafuta karibu na makazi ya watu.

    ReplyDelete
  9. Jamani acheni wivu,kwani mliposema tujiajiri mlikua mna maana gani? Huu ni ubunifu wetu ndio sababu hata mamlaka husika zimetupa baraka tuanzishe klabu kama hizo mbona hampigii kelele mambo mengine kama gereji bubu,machinga.....

    ReplyDelete
  10. pale manispaa ya kinondoni afisa utamaduni ni corrupt vibaya ndiye anayeruhusu hivi vitu kwa kupewa mlungula.

    ReplyDelete
  11. Jamani MABAA ni kweli yamekuwa kero sana kwa Manispaa hii ya Kinondoni. Baada ya mitaa ya Sinza kukosa nafasi ya kuweka mabaa mapya sasa mabaa yamevamia maeneo ya Mbezi Beach and Tegeta.

    Usishangae Tanzania likawa Taifa la walevi kama vile ilivyokuwa nchi fulani ya jirani.

    ReplyDelete
  12. Kaka Philipo pole sana. Natambua kwa dhati adha unayoipata.

    Kama mdau mmoja (anonym. wa 02.40 PM) naongezea tu kwa ushauri. Nenda Halmashauri husika (I mean Ulipo)uliza OFISA anayeshughulikia kero mbali mbali za wananchi, mpe issue yako nahakika kama wapo makini tatizo litatatuliwa ndani ya siku 7 hadi14.

    Endapo watakuambia hakuna Ofisa kama huyo,ima hawakushughulikia ipasavyo, ama wataleta ucheleweshaji wa aina yoyote, tafadhali toa habari hiyo michuzi haraka sana tutajua nini cha kufanya. Nakuhakikishia mkurugenzi atawajibika. Nakuambia huyo Mkurugenzi atakua mfano.

    TAHADHARI: Issue iwe ya kweli.

    MAONI: Endelea kutuhabarisha nini kimejiri. sina haja ya kukupa namba ya simu ama email kwani ni vema dunia nzima ikajua nini kinaendelea juu ya ufisadi, udhalimu na ufedhuli wa namna hii. Pia ukifanikiwa tuhabarishe kwani baadhi ya ndugu, wapendwa wakianzisha issue ikitiki wanakaa kimyaa.
    Polsana. Ila tambua ya kuwa inawezekana.

    ReplyDelete
  13. MUUNGWANA TUAKUSHUKURU SANA KWA KULETA MJADALA HUU. NI KWELI KUNA UDHIA MKUBWA SANA JUU YA HAYA MABAA YA VICHOCHORONI..NASHINDWA KUFAHAMU NI KWANINI SEREKALI INASHINDWA KUFAHAMU HASARA ZAKE..KWELI WIZARA YA MIUNDOMBINU INAFANYA KAZI AU NDIO KILA KITU UFISADI..MIMI MDAU NAISHI NJE LAKINI KILA NIKIRUDI TZ NAKUWA NAPATA TAAABU SANA KWA KELELE ZA PALE VIJANA..YAANI HUJUI WEEKEND AU SIKU ZA KAWAIDA..HIVI KWELI TUNA TEGEMEA KUWA NA TAIFA IMARA. NA WENYEVITI WENGI WA SEREKALI ZA MITAA WANA NJAA NA ELIMU IMEPINDA..HII INASABABISHA VILE VILE.

    ReplyDelete
  14. Haya sasa majungu watu wa Sinza hawajalalamika wewe ni diwani wao unalalanika kwa niaba yao? Huyo mwenye bar hata kama anapiga muziki ni sheria gani ya nchi amevujaa?
    Na huyo anayekusapoti eti maadili, taifa la mafisadi lina maadili gani?

    ReplyDelete
  15. SASA UNATAKA BAR AKAJENGWE WAPI? PORINI? NA HUKO PORINI ATAKUNYWA NANI? NYANI? CHA MSINGI NI KWAMBE KUWE NA UTARATIBU WA KUPIGA MUSIKI NDANI YA SOUND PROOF ROOM/HALL. BAR NI DUKA LA POMBE KAMA LILIVYO DUKA LA MAHARAGE.

    ReplyDelete
  16. Tatizo la hizi bar za siku hizi ni kelele. Hapa Msasani village kwa wavuvi kuna bar mbili ambako muziki unapigwa kila ijumaa, jumamosi na jumapili kuanzia saa 3 usiku mpaka saa 11 alfajiri kwa sauti ya juu ajabu (inayosikika zaidi ya kilomita mbili)na kutukosesha mapumziko watu wanaofanya kazi wiki nzima kila siku. Madiwani wetu watekeleze majukumu yao.

    ReplyDelete
  17. Wewe unayeuliza kwa kupiga makele kwa huo muziki ni sheria gani imevunjwa, hujui habari ya NOISY POLLUTION? Ni uchafuzi wa mazingira pia kwa aina yake hiyo mikelele isiyo na mipaka

    ReplyDelete
  18. Nianze kwa kumpa pole mdau Philip kwa tatizo linalokupata la kujengewa baa karibu na makazi yako. Niruhusiwe kutoa historia fupi ya tulikotoka kama Tanganyika na sasa Tanzania ili tuweze kuangalia mbele.

    Enzi ya Mwalimu, serikali haikuwa na mchezo katika hili suala la rushwa. Taifa lilikuwa ni la wakulima na wafanyakazi, hizo biashara sana sana waliachiwa watanzania wenye asili ya kiasia ambao wengi wao walikuwa maeneo katikati ya mji. Watanzania weusi katika mitaa mingine kama vile kinondoni, ilala, Temeke, Kurasini nk walikuwa wafanyakazi, tena wa kuajiriwa na serikali. Unapokuwa na genge kubwa sana la wafanyakazi wanaopata mshahara mwisho wa mwezi nani atampa rushwa mwenzake ili amkatie sehemu ya kiwanda aanzishe bar?

    Matatizo yalianza pale awamu ya pili. Ikaja zama za RUKSA. Kila mtu na lwake, mwenye kuanzisha baa ruksa, mwenye shule uchwara ruksa, mwenye nyumba ya wageni ruksa, mwenye teksi bubu ruksa. Tanzania ghafla ikawa na jeshi kubwa la wajasiamali ambao wakawa wanagombania nafasi kidogo iliyopo kufanyia biashara, Baa ikiwemo. Ghafla maeneo kama Sinza yaliyokuwa mapori miaka ya mwishoni mwa 70 yakashika kasi ya kuanzishwa mabaa ilipofika katikati ya miaka themanini. Wale waliokuwa wafanyakazi watiifu wasioijua pesa sasa ikawa ruksa kufanya biashara yoyote. Biashara ikawa huria. Wazungu wanaiita economic law ya demand na supply. Kama mahitaji ya viwanja kwa minajiri ya wafanya biaashara wanaotaka kufungua baa yanapokuwa makubwa basi hapo panakuwa na watoa huduma, yaani Suppliers. Kwa bahati mbaya sana maofisa ardhi ndio suppliers wa viwanja ikawa ni rahisi kuhongwa katika hali ya kukidhi njaa ya wafanyabiashara uchwara.

    Sasa tumefikia pabaya, mabaa yapo kila kona na hatuna pa kupumulia. Tufanyeje??? Tatizo hakuna wa kumfunga paka kengele. Inapofikia mahali mkuu wa kaya anafanya biashara Ikulu hapo kuna jambo.Hauwezi kukemea uozo kama kiongozi mwenyewe ameoza.

    Muhafaka ni nini? TUZIDI KUPIGA KELELE MPAKA KIELEWEKE. ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete
  19. Duh kwa kweli brother michuzi ingebidi watu kama hawa waeleweshwe jinsi ajira zilivyo za shida kwanza hiyo sehemu anayoiongelea ni nzuri sana na inafaa kwa wanafamilia kwani hata baadhi ya waandishi walisha isifia sehemu hiyo kwa mandhari yake na utulivu wake. mziki unaopigwa hapo ni wa utulivu mkubwa. kwa kweli sisi wakazi wa hapa tumepata sehemu yenye hadhi ya kwenda na familia zetu.

    ReplyDelete
  20. Mimi pia nimefika hiyo sehemu brother michuzi uwezi amini ukifika hapo hiyo garden, michezo ya watoto, vyakula kama hoteli ya kitalii kwa bei nafuu,vyoo vilivyo safi hata vya baadhi ya majumbani kwetu havifikii usafi huo. kwa kweli mandhari yake ni tulivu. Jamani Tanzania kuna matatizo mengi hivi tujiulize viwanja vilivyotengwa kwa recreational centers na huduma zingine za jamii vilienda wapi? ndiyo maana watu wenye upeo wanaamua kuanzisha vitu kama hivi ili wanafamilia wawezekujumuika pamoja katika maeneo karibu na manyumbani ambapo hutuhitaji kuingia gharama za usafiri kwenda mbali. Watanzania tuna mambo mengi ya kujiuliza kuhusu mambo ya muhimu kama barabara,mahospitali na mashule.

    ReplyDelete
  21. Kaka Philipo pole sana na tafadhali zingatia ushauri uliopewa na watu mbalimbali kwani wengi wana nia njema. Unajua tatizo letu kubwa watanzania siyo umasikini tu bali umasikini wa mawazo. Watu wengi hawajui adhari ya vitu kama hivi katika maisha yao mpaka pale yanapowakuta. Na inabidi wajue kuwa mara nyingi adhari zake huwa zinajitokeza baada ya muda mrefu na jinsi ya kukabilina nazo inakuwa ngumu. Ni kama vile kwa mfano ujenzi holela ulivyo anza katika miji mingi ya hapa Tanzania huku serikali ikiwa imelala na sasa ni vigumu sana kurekebisha. Unajua waweza laumu kwa nini brother fulani kang'ang'ania kuishi ughaibuni anabeba maboksi bila kuelewa ni kwa nini kaamua kufanya hivyo. Yawezekana nafuu ya bughudha kama hizi ndizo zinamfanya aone hata afadhali kuishi huko hata kama ananyanyaswa. Nakutakia kila lakheri na ujue wapo watu wanakusoti katika hili. Sitaji jina wala wadhifa wangu lakini hii issue ikipitia karibu nami lazima niivalie njuga kwani huyu jamaa anayetoa vibali naona amezidi sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...