MAREALLE - THE PARAMOUNT CHIEF??

Michuzi,

Kwenye gazeti la Sunday News (February 14) ukururasa wa tatu kulikuwa na remembrance ya Babu na mpendwa wetu marehemu Thomas Marealle ambaye anaitwa THE PARAMOUNT CHIEF. Je kuna wadau wanaweza kuelezea maana ya hili neno paramount? Nijuavyo wachagga wa Kibosho na wengineo kama wale wa Old Moshi, Rombo na kwingineko walikuwa na wa-MANGI. Je nafasi ya Baba Yetu Marealle kwa mangi wengine wote ni ipi? Naomba kuwakilisha

MUSHI DEO
Mwenge DSM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ijapokuwa mimi sitoki Kilimanjaro, ninajua kuwa neno paramount maana yake ni (m)kubwa kuliko wote. Nakumbuka kuwa nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikisikia redioni Chifu Marealle akiitwa "mangi mkuu" (wa wachaga) ijapokuwa maeneo mengine ya Kilimanjaro yalikuwa na mangi wake, k.m. Chifu Shangali,wajukuu wa mangi Sina, Lemnge n.k. Kitu ambacho sikuelewa ni, je, mangi wengine walikuwa wameafikiana kumtambua mangi Marealle kuwa ni mangi mkuu wao? (kama vile Waswahili walivyokuwa na machifu, wakulu, masheha waliovyomtambua mwinyimkuu wao au watemi wadogo wa Unyamwezi na Unyanyembe walivyomtambua chifu Fundikira kuwa mtemi wao). Mdau wa historia na elimu ya jamii (sociology).

    ReplyDelete
  2. Historia inatuambia kuwa Chifu Marealle alikuwa Chifu mzuri kwa watu wake.

    Ila hili la kuitwa "PARAMOUNT" mimi naona wangepewa machifu wengine kama Mkwawa and the like...ambao matendo ujasiri na misimamo yao ilibadili historia ya Tanganyika kuelekea kwenye Uhuru.

    Great Babu yangu alikuwa Chifu kama walivyo machifu wengine, ingawa nimesoma na kuelezewa historia yake na Babu yangu siwezi kumfananisha na Chief Mkwawa au Chief Kinjikitile Ngwale. Ingawa wote walikuwa na rank sawa.

    Kama ambavyo siwezi kumlinganisha JKN na JK..!!!!!!!

    Network Engineer (NE),
    Reading, UK

    ReplyDelete
  3. historia inaseam mkoloni alipokuja hakuvunja uchifu,ila alijaribu kuwaunganisha kila sehamu sasa mariaale alichaguliwa kama mangi mkuu yani mangi wengine wote walikubaliana naye kama kiongozi anaye wawakilisha wote huko kilimanjaro kama mangi wao,mkoloni akitaka kuongea na kilimanjaro walikuwa wanaongea na paramaunt chief wamemaliza na hizo sehemu zote walichagua mtemi,chifu wa kuwawakilisha

    ReplyDelete
  4. Mangi Mkuu au Paramount Chief wa Wachagga alikuwa kiongozi wa Mangi wote wa Uchagani. Mangi Mkuu alikuwa anachaguliwa na wananchi wote wa Uchagani baada ya kuanzishwa kwa Chagga Union. Mangi Marealle ndiye aliyekuwa Mangi Mkuu wa mwisho, lakini kulikuwa na uwezekano wa Mangi mwengine kuwa Mangi Mkuu baada ya Marealle.

    MAREALLE ALIKUWA PARAMOUNT CHIEF WA WACHAGGA TU, SIYO MAKABILA YOTE YA TANZANIA.

    Mtwa Mkwawa, au Mjukuu wake Mtwa/Chief Adam Sapi Mkwawa alikuwa anastahili kuitwa kabisa Mtwa Mkuu au Paramount Chief wa Wahehe.

    ReplyDelete
  5. Naomba kuuliza swali kuhusu huyu Paramount Chief Marealle. Je ni kweli kuwa huyu ndiye chifu aliyependekeza kilimanjaro ipewe uhuru peke yake kabla ya Tanganyika? Nimewahi kusikia hili jambo sijui kama ni kweli au ni uzushi?

    ReplyDelete
  6. Anonymous uliopost post ya tatu.

    Nakupongeza na nakushukuru kwa kuelezea vizuri. Ni kweli kabisa Mangi Marealle alichaguliwa kwa kura. Kuitwa Paramount ni sahihi kabisa kwani alikuwa ni Mangi wa Mamangi a huko uchaggani.

    Uchaggani kulikuwa na Machifu (Mwitori) wakuu watatu. Chifu Abdiel Shangali (Hai), Chifu Maruma (Rombo) na Chifu Petro Itossi Marealle (Vunjo).

    Wachagga waliamua kuwa na Mangi Mkuu pale walipobaini hujuma zilizokuwa zinafanywa na wakoloni. Kwani walikuwa wakitumia upenyo kwa kuwagawa na kisha kuwayumbisha wachagga. Basi wachagga wakaamua kuunda Chagga Union.

    Kura ikapigwa na Thomas Marealle akawa Mangi wa Mangi, yaani mkuu wa Maruma, Shangali na Marealle.

    Kwa kweli maendeleo ya wachagga hususan katika elimu yaliletwa na fikra na utekelezaji Mangi Marealle kwani yeye ndiye aliyependekeza kuwa kila kilo ya kahawa ikatwe shilingi moja kwa ajili ya kuchangia elimu hususan ujenzi wa shule mkoani Kilimajaro.

    Kuhusu Kilimanjaro kupewa uhuru peke yake, sijawahi kulisikiwa wala kuwa katika kumbukumbu.

    ReplyDelete
  7. kupendekeza Kilimanjaro ipewe uhuru haimaanishi kupendekeza Majimbo mengine yasipewe uhuru. kuna kipindi harakati za kudai haki mbalimbali za wananchi wa Tanganyika hazikuwa na sura ya kitaifa. hiyo ni kabla ya Tanu kuanzishwa. hakuna taarifa za uhakika kama Marealle alipinga maeneo mengine ya Tanganyika kuwa huru.

    kabla ya Tanu kuanzishwa Wachaga walikuwa na chama chao kinaitwa Chaga Union. pia walikuwa na siku yao maalum iliyokuwa ikitambuliwa na serikali ya mkoloni ikiitwa Chagga day. Wachaga walikuwa mbele zaidi katika kujiamulia mambo yao ya kiuchumi na kijamii kuliko maeneo mengine ya Tanganyika.

    harakati za kueneza Tanu Kilimanjaro zilipata upinzani kutokana na kutanguliwa na Chagga Union. hili ni jambo la kueleweka kabisa.

    VIJANA WASOMI WA KICHAGA KAMA ELIUFOO WALIMPINGA MANGI MKUU NA KUIPA NGUVU TANU KTK MKOA WA KILIMANJARO.Eliufoo alikuwa ameoa kwenye ukoo wa Chifu Shaghali wa Machame.

    dhana kwamba Wachaga walipinga uhuru wa Tanganyika inakosa nguvu kutokana na juhudi za wananchi kama Eliufoo,Nsilo Swai, na wengine walioshiriki kueneza Tanu maeneo ya Kilimanjaro.

    ReplyDelete
  8. Ni kweli wachaga kutokana na asili yao hawakuwahi kuwa na mangi mkuu. Inasemekana karibu kila kitongoji uchagani kulikuwa na mangi (au mtawala) wake na kwa kadiri mwanahistoria mwingereza Kaithleen Stahl alivokadiria miaka ya hamsini kulikuwa na machifu karibu 129 uchagani kote, lakini inaonekana wengi kama 90% walikuwa mashariki mwa uchagani, yaani chaga ya kati (uru, mbokomu, old moshi, kahe), vunjo na rombo.

    Magharibi ya uchagani yaani kibosho na machame ndiko kulikuwa na tawala kubwa zaidi, kibosho ikijumuisha eneo lililojulikana kwa asili kama kibosho, mweka, umbwe, na kwa wakati fulani kindi, na narumu. Machame ilijumuisha kwa miaka mingi eneo lilioitwa machame lakini pia lyamungo, kwa sadala, boma ya ng'ombe, masama, yuri, na siha (ingawa kwa kipindi fulani hasa baada ya kuporomoka kwa utawala wa machame miaka ya mwanzoni mwa 1880 waliunda tawala zao wenyewe kutegemeana na koo kama vile mmari, mwanri, kileo, urio, n.k.).

    Inasimuliwa hata hivyo miaka ya nyuma sana ya mwanzoni mwa 1800, watawala wawili wa uchagani walioitwa Rengua (wa machame) na Horombo (wa rombo) waliunda tawala zenye nguvu sana hata kukaribia kuigawanya uchagani kwenye maeneo mawili makubwa kwa kutumia mpaka wa mto ngassa, yaani mashariki (orombo) na magharibi mwa uchagani (rengua). Hata hivyo vita visivyoisha vilifanya orombo auawe katika mashambulizi makali yaliyotokea magharibi kutokea kibongoto kupitia nyuma ya mlima wa kilimanjaro yakijumuisha wangaaseni (waliokuwa na uhasama mwingi na wa muda mrefu na orombo), wakilema (waliokimbilia machame kutokana na vita vya orombo kule mashariki), wamachame, na wamasai (waliokuwa na chuki na orombo kuwanyang'anya ngombe zao). Tunafahamu kihistoria kwamba mmishionari johannine rebmann alipofika uchagani miaka ya 1848/9 aliripoti kwamba mangi mamkinga mtoto wa rengua wa machame ndiyo alikuwa mtawala mwenye nguvu zaidi kule uchagani. Lakini hata hivyo uchagani hakukuwahi kuwa na aliyefahamika rasmi kwamba ndiyo mangi mkuu wa wote ingawa kwa miaka mingi sana mangi wa machame waliheshimika uchagani kama utawala wenye nguvu zaidi, mpaka ilipofika miaka ya 1870 ndipo mangi rindi (mandara) wa moshi na mangi sina wa kibosho walipochukua hatamu za uongozi wa kisiasa kule uchagani baada ya machame kuangukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu baada ya kifo cha aliyekuwa mtawala, na hivyo kuanguka kwa utawala wa machame katika miaka ya mwishoni mwa 1870.

    Miaka ya 1890 ilianza kushuhudia tena kuibuka kwa mtawala mwingine kule uchagani aliyeitwa marealle (wa marangu) aliyeanza kushika hatamu ya kisiasa baada ya kufa kwa mangi rindi wa moshi (1890) na sina wa kibosho (1897). Ingawa alionekana kama ndiyo mwakilishi wa wachaga wote kwa serikali ya kijerumani hasa katika miaka ya mwisho ya 1890 na mwanzoni mwa 1900, lakini kama alivyokuja kuwa mangi abdieli shangali wa machame wakati wa serikali ya kiingereza, hawa hawakuwahi kuwa rasmi kwamba ni mangi wakuu wa uchagani, ila inaonekana wakoloni waliwafanya hivyo kinyemela kwa sababu walizozijua wao wenye za kisiasa kule uchagani. Ukweli ni kwamba mtu wa kwanza kuitwa mangi mkuu kule uchagani alikuwa ni thomas lenana mshumbue marealle ambaye alipewa madaraka hayo baada ya uchaguzi uliofanywa na wananchi uchagani mwaka 1951.

    Vuguvugu hili lilitokana hasa na wachaga kumlalamikia mangi abdieli shangali wa machame kwamba amekuwa ni kibaraka wa wakoloni na kumtuhumu kutumiwa kuwahujumu wananchi ardhi. Hivyo walilazimisha kwenye baraza kuu la uchagani yaani chaga council uchaguzi ufanywe ili wananchi wapate mtu wa kuwasikiliza na kupanua wigo wa kidemokrasia uchagani. Wakoloni walikubali na uchaguzi ulipofanyika wananchi kwa kauli moja na kwa kishindo wakamchagua thomas marealle kuwa ndiyo mangi mkuu huku wakiwa na matumaini makubwa ya kumdhibiti mangi abdieli shangali. Hii kwa ufupi ndiyo historia ya kisiasa ya uchagani hasa kuhusiana na suala la umangi mkuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...