Marehemu Hamisi Kitambi
Mwanamziki mkongwe HAMISI KITAMBI amefariki dunia leo 26 February 2010 Dar-es-salaam. MAZISHI YATAFANYIKA JUMAMOSI saa 7.00 mchana 27-02-2010 MAGOMENI mtaa wa Ifunda jirani na shule ya MzimuniJijini Dar.
Marehemu Hamisi Kitambi aliwahi kupigia bendi za Msondo Ngoma, kabla ya kupata maumivu ya mguu baada ya ajali alipokuwa safarini na bendi ya Msondo Ngoma.
Marehemu pia alikuwa mwanamziki nyota enzi za Tabora jazz,ambako alipigia vijana hao wa Segere Matata kabla ya kuhamia Juwata Jazz sasa Msondo Music band.

Kwa taarifa zaidi tafadhali mnaweza kuwasiliana kwa simu na familia ya marehemu kwa simu namba
+255 713 802370 Almasi Kassanga.
au
Bi.Mwamini Kitambi simu namba +255 712 217740

Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi.
AMIN
Hayati Hamisi Kitambi akiuguza majeraha yake


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. rip mzee kitambi

    ReplyDelete
  2. Poleni sana ndugu, marafiki na wapenzi wote wa muziki. Ingawa sasa hatufahamu, nahisi hili ni pengo lisilozibika kwetu wote. Pia ni funzo kwetu sote: Tuwapende na kuwakumbuka tuwapendao wakati wako hai......
    Blackmpingo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...