Katibu Mkuu Kiongozi (Chief Secretary) Mh. Philemon Luhanjo akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo jioni hii alipofika kutoa pole kwa wafiwa wa Marehemu mpendwa wetu Reggie Mhango aliyefariki jana katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar. Kwa mujibu wa mmoja watoto watatu alioacha marehemu, Reggie jnr, Mazishi ya Reggie yanatarajiwa kufanyika kesho saa tisa alasiri katika makaburi ya Kinondoni. Misa itasomewa nyumbani kwake Magomeni Mikumi kuanzia saa saba mchana.
Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Philemon Luhanjo akitoa pole kwa waombolezaji, ikiwa ni pamoja na mtoto wa marehemu Reggie jnr (shoto)
Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Luhanjo akijumuika na waombolezaji
Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani hapo na Mh. Luhanjo
Waombolezaji kinamama wakiwa msibani
Kinamama wakiandaa chakula kwa waombolezaji
baadhi ya waombolezaji kinababa msibani



























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Asante kaka Michuzi. Yaani naangalia hizi picha,nakumbukua kuongea na Reggie Jr. Oktoba, nakumbuka kuongea na Reggie mwenyewe pale nyumbani kwake ingawa alikuwa anapata taabu kuongea shauri ya stroke. Nakumbuka siku ya kupiga sinema Bongoland 2 pale kwake mwaka 2007. Na hasa jinsi Reggie alivyokuwa mkarimu kwa crew. Crew walikuwa wanamwita Uncle.

    Rest in Eternal Peace Reggie Mhango.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...