Katibu Mkuu Kiongozi (Chief Secretary) Mh. Philemon Luhanjo akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo jioni hii alipofika kutoa pole kwa wafiwa wa Marehemu mpendwa wetu Reggie Mhango aliyefariki jana katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar. Kwa mujibu wa mmoja watoto watatu alioacha marehemu, Reggie jnr, Mazishi ya Reggie yanatarajiwa kufanyika kesho saa tisa alasiri katika makaburi ya Kinondoni. Misa itasomewa nyumbani kwake Magomeni Mikumi kuanzia saa saba mchana.
Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Philemon Luhanjo akitoa pole kwa waombolezaji, ikiwa ni pamoja na mtoto wa marehemu Reggie jnr (shoto)






poleni
ReplyDeleteAsante kaka Michuzi. Yaani naangalia hizi picha,nakumbukua kuongea na Reggie Jr. Oktoba, nakumbuka kuongea na Reggie mwenyewe pale nyumbani kwake ingawa alikuwa anapata taabu kuongea shauri ya stroke. Nakumbuka siku ya kupiga sinema Bongoland 2 pale kwake mwaka 2007. Na hasa jinsi Reggie alivyokuwa mkarimu kwa crew. Crew walikuwa wanamwita Uncle.
ReplyDeleteRest in Eternal Peace Reggie Mhango.