Mtoro Mwinyi Bakari alizaliwa mnamo Oktoba 3, 1869 huko Donda, Bagamoyo katika pwani ya Tanganyika na kufariki mwaka 1927 nchini Ujerumani.

Bakari alikuwa mkufunzi wa lugha na mila za waswahili mwanzoni mwa karne ya 20. Ni mmoja ya watanzania wa kwanza kuishi nje ya nchi na ingekuwa leo tungesema alikuwa "mbeba mabox" wa kwanza.

Mtoro Bakari alienda nchini Ujerumani mnamo mwaka 1900 kwa ajili ya kufundisha lugha ya kiswahili katika chuo cha "School of Oriental Languages in Berlin".

Akiwa huko aliweza kuandika na kutayarisha kitabu: "Desturi za Wasuaheli na khabari za sheri'a na desturi za wasuaheli" kilichochapishwa mwaka 1903 huko Göttingen, Ujerumani.

Chapisho hili pamoja na mingine aliyoweza kuandaa zilitoa mchango mkubwa katika kusambaza kwa maandishi kuhusu tamaduni za watu wa nchi yetu.

Ningependa kuwahimiza watanzania wenzangu kujiwekea mazoea ya kusoma kuhusu watu hawa muhimu katika historia ya nchi yetu. Makala nyingi kuhusu watanzania mashuhuri zinakosekana, ila nimefurahi kuona "biography" iliyoandikwa na mtafiti kutoka Ujerumani Ludger Wimmelbcker kuhusu mtanzania huyu.

Kitabu hicho cha maisha ya Mtoro Mwinyi Bakari kinaitwa:
"Mtoro bin Mwinyi Bakari (c. 1869-1927): Swahili lecturer and author in Germany" by Ludger Wimmelbcker, Ph.D Kimechapishwa na: Mkuki na Nyota Publishers na w
aweza kuona dondoo ya kurasa za mwanzo:
kitafute na kinunue leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. duh! nimeipenda hii. lazima nikitafute hiki kitabu.

    ReplyDelete
  2. MZARAMO! Pazi.

    ReplyDelete
  3. Hiki Kitabu nitatafuta haraka Jamaaa wa Kikwete hawa na kina Mwinyi watu wa Pwani. Kimaro

    ReplyDelete
  4. I am glad the author took up the task. I read the book, and it is a great job done. A great piece of Tanzanian history there.

    ReplyDelete
  5. Sizani kama huyu ni Mzaramo Pazi sababu hata mie Mzaramo hata sehemu ya Kizaramo haijaonesha kama yeye Mzaramo na pia kweli kaondoka miaka ya Zamani kabla Wananchi wa Tanzania Asilimia kubwa hawajawa Kristo wala Waislamu walikuwa wanaabudu watu wengi Tanzania Mambo yao. Mangara Bin Mangara.

    ReplyDelete
  6. DUh Jamaa kapiga pamba alafu kakata mzizi wa Fitna kavaa Saa upande unaotakiwa sio wanavyotaka wazungu kavaa Mkono wa Kulia kama Ankal Michuzi.

    ReplyDelete
  7. Shukrani kwa aliyetuma khabari hii. I will definitely look for that book.

    The title of the book mentioned is very interesting..."Desturi za Wasuaheli na khabari za sheri'a na desturi za wasuaheli"

    Evolution of Swahili language is...well....good or bad?.

    See, so it seems that the very first speakers of the language called it Suaheli as opposed to Swahili, je lugha inakua ama inaharibika (angamia)?

    Sikuhizi tunasema Habari, zamani walisema Khabari....sheria vs shari'a. Influence of Arabic language was more evident than now.

    Ukisoma kazi za waandishi wa zamani kabisa wa lugha hii unaweza ukatoka kapa. I mean unaelewa general meaning lakini neno kwa neno ni tofauti na sasahivi. Hili jambo hutokea katika lugha nyingi, (kama sio zote).

    It's like that old "THOU, THY, THINE, DOETH" English, if you know what I mean.

    By the way, they used arabic letters back then. (kisha mkoloni wa Europe kaja eti akasema waswahili ni illiterate)

    Anyway...naombeni maoni yenu, mnaonaje...lugha yetu inaangamia ama inakua?

    ReplyDelete
  8. huyu lazima alikuwa traitor ,wa babu zetu alikuwa anawafundisha wajeremani kiswahili ili watutawale vizuri na kufichua siri na weakness zao.

    sisomi habari zake wala kitabu chake hakufanya kitu chochote kwa nchi wala watu wake ,ndo maana hakuna aliyemsikia kwenye historia. kama wakina mkwawa ,nyerere a wengine

    Mr Bakari ,sorry sikufagiliii

    ReplyDelete
  9. unajua vijana wengi wa kitanzania ni wa kipekee hapa swali la kabila gani halipo kabisa lakini tunangalia asilia ya majina mwinyi ni watu wa pwani mabali na hayo watu wa bara kiswahili kiliwa bado akijaenea vizuri sasa mada ni je mnamkumbuka huyu jamaa kwa shujaa wa taifa kwa nje ya mipaka kama huna data hacha usindike upuuzi wa-tanazani wa-asili tafouti na USA ukitamka jina la ukoo tu mtu anajua huyu mtu wa wapi

    ReplyDelete
  10. Hii lugha yenu ya kuita watu wabeba mabox itawapotosha sana vijana wetu hasa vizazi vijavyo ambavyo baadhi yao watakosa opportunity kwa kufikiria kuwa kila aliye nje ya nchi ni mbeba box...Ohooooooo..shauri lenu na maneno yenu....!!

    ReplyDelete
  11. Duh! Kuuliza si ujinga. Usafiri enzi hizo ulikuwa wa namna gani? Pipa au majini tu?
    Jamaa alikuwa jasiri.

    ReplyDelete
  12. florian rweyemamuFebruary 23, 2010

    Hii nimeipenda, asante kwa kutuimiza.

    ReplyDelete
  13. ADILI NA NDUGUZEFebruary 23, 2010

    Tell us more please. Inaelekea alifariki akiwa ana umri wa miaka 57. Hakuacha mke au watoto au jamaa zake huko Bagamoyo?

    Hata mimi nimeipenda hii khabari. Kumbe sisi wasuaheli tuna historia?

    ReplyDelete
  14. kumbe uyu ndo alituuza kwa wakoloni wa kijeremani???alienda km mtumwa

    sasa alikua hajui kuwafundisha kiswahili ndo kuliwafanya waje kiulaini kututawala??nyambaf

    wazungu bwana?apo uyu prof anajidai kututukuza ooh lugha yetu utamaduni wetu sijui nn uko ujeremeni

    ReplyDelete
  15. Hawa watu story zao zimezibwa na na JK wa kwanza ili watu wazidi kuamini kama yeye ni baba wa taifa ndio maana mpaka leo hauoni story za wababe wa jadi

    ReplyDelete
  16. wewe mdau wa Tue Feb 23, 01:41:00 AM uislam upo miaka 1000 iliyopita tanganyika soma storry za kilwa na kaole utaona

    ReplyDelete
  17. Nakumbuka pale Nyaraka za Taifa (National Archives), Kisutu, katika miaka ya 1980's na 1990's kulikuwa na maelfu ya nyaraka za Kihistoria, zikiwa pamoja na nyingi zilizoandikwa kwa kijerumani. Kulikuwa na mtaalamu mmoja mtafiti m-TZ aliyekuwa akijua kijerumani (kidachi) akiitwa Dk Mose (?). (nasikia alifariki). Tunatumai nyaraka hizo zitaendelea kutunzwa na watafiti wengi zaidi, hasa wa vyuo vikuu, watajituma kuzitumia nyaraka hizo kabla hazijatoweka kama vile majengo ya kihistoria DSM yanavyotoweka. Pia nampongeza Mzee Walter Bgoya na kampuni yake ya Mkuki na Nyota kwa jitahada yao ya kuchapisha vitabu vyenye kutupa mwanga ya historia yetu (vikiwemo vitabu vya Shaaban Robert). Mdau mtafiti.

    ReplyDelete
  18. Huyu jamaa si Mzaramo bali ni Kabila la Kimaniema kutoka Kongo ni wale ma Slave walioletwa kuuzwa Zanzibar,siunaona ana jina la Mtoro kama Ramazani Mtoro Ongala aka Remmy.

    ReplyDelete
  19. Nagal WashngtonFebruary 23, 2010

    VIZURI HII HABARI IMEWEKWA HAPA KIFUPI MTORO MWINYI BAKARI ANA FAMILIA YAKE NAWAJUA,MTAA WA DUNDA SIO DONDA,KULIPOKUWA DUKA LA NYMA MAARUFU MGONELA KARIBU NA GARDEN,KWA WANAOTEMBELEA HAPO KUNA CHUO CHA KIISLAM KINAITWA KWA MWALIM MWARIKO,BAADHI YA NDUGU ZAKE NI MCHORAJI MSACHO,FUNDI MWARAMI,SHARIFF AHMED,MWENYEKITI MASOUD MPILI,WENGINE WAMETANGULIA MBELE YA HAKI.INNALILLAH WAINNA RAJN.kwa ufupi mkitembelea Bwagamoyo pia mtajua kwa nini ukaitwa mtaa wa Dunda

    ReplyDelete
  20. Michuzi,

    Bagamoyo kwetu hakuna sehemu inaitwa DONDA ni DUNDA.

    Misituharibie majina ya mitaa yetu... ukiendelea ntasoma albadili nimkaange mtu sasa hivi usicheze kabisa na wazee wa Bagamoyo!!

    Ni mimi ALHAJI MITOSO wa mangesani!

    ReplyDelete
  21. Hi ni product ya Slave trade. Jamaa alichukuliwa mwishoni mwishoni mwa slave trade, na wakati slavery ingali inaishia ishia wajerumani walihitaji kuja ututawala. Walichuua slaves wale walio wajanja wakawapiga msasa kidogo wakawafundisha lugha. Jamaa liliuwa kipanga na wajerumani wakalitumia vilivyo. NDio maana alifia hukohuko na hakurudi lakini kidogo kwa mbali alijua ametokea wapi na mwaka alio zaliwa ulikuwa wa ubuni tu

    ReplyDelete
  22. yaani nimechekaaaa

    DONDA vs DUNDA....

    michuuuu utauawa?ooohooo

    ReplyDelete
  23. Tuwe objective jamani. Kukosea jina la mtaa kwa herufi moja si hoja. Pili si vema kujadili masuala ya makabila, huyu ni Mtanzania, basi. Na kisha, Wajerumani waliongoza shughuli ya kuigawa Afrika mwaka 1885 na wakaichukua Tanganyika rasmi mwaka 1891 na kufikia mwaka 1892 wakapora maili kumi za Sultan zilizokuwa kwenye ukanda wa pwani ya Tanganyika pamoja na kisiwa cha Mafia. Mwinyi Mtoro alikwenda Ujerumani mwaka 1900 wakati tayari Wajerumani wameshaichukua nchi yetu. Tusimlaumu. Pia ukisoma historia ya elimu Tanzania, utaona kwamba Wajerumani ndio walikuwa wa kwanza kutumia Kiswahili kufundishia mashuleni, hivyo akina Mtoro wanastahili sifa. Tujifunze mambo ya nchi yetu wajameni mwe!.

    ReplyDelete
  24. Nimefuatilia huu mjadala. Mimi ndie nileyemtumia bw Michuzi khabari hii.
    Nilifanya 'typo' katika kuandika, kwani ni kweli mahala atokapo Bakari ni Dunda huko Bagamoyo na sio Donda.
    mdau,
    mfaume abdalla

    ReplyDelete
  25. nagal washngton unasemea garden ya kinondoni mkwajuni au ya wapi?kama mkwajuni inaonyesha wewe mwenyeji pale loh!au unasemee garden gani?ok labda nakujua mwenzangu hata mimi wa kinondoni huko.kama mwenzangu nitakutafuta

    ReplyDelete
  26. Kwa hiyo hao wajerumani waliokuja kututawala wlaifundishwa na huyo. Wazee walikuwa wanasema mjerumani alikuwa mkatili sana. Walisema kuwa bora Mwingereza alivyokuja alikuwa na utu kidogo.

    Mimi nitasoma hicho kitabu nikipata nafasi. Ningependa kupata picha halisi ya German East African/Tanganyika kutoka kwa jicho la MTanganyika.

    ReplyDelete
  27. Nimebaki ofisini hadi saa hizi nikisoma hicho kitabu, na nimekimaliza. Historia nzuri mno iko humo ndani. Pia yapo mambo ya desturi za watawala wa wakati ule, hayo 'mahongo' waliyokuwa wanatoza sijui ndio rushwa au ushuru, lakini walikuwa wanayafaidi hao watemi peke yao. Lifestyle za watemi pia zimeniacha hoi: kuketi amezungukwa na mabinti pande zote, huku binti mmojawapo akimnywesha pombe, na hili linafanyika akiwa amebarizi anasubiri wageni! Mambo ya biashara pia, na transaction za wakati ule, yote yamenivutia sana.

    Hongera Michuzi, tafadhali endelea kututafutia mambo kama haya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...