Mtoto Dickson (pichani) alizaliwa Januari 15, 2000 kwa njia ya operesheni akiwa na uzito wa kilo 2.3 katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Ni mtoto wa tatu kuzaliwa katika tumbo la mama yake mzazi.

Makuzi yake katika miezi mitatu ya mwanzo yalikuwa ya kushangaza sana kwani alinenepa sana, kuongezeka uzito mno, kulia mfululizo kupita kiasi muda wote, na shingo yake ilikuwa imelegea sana na hata alipokalishwa alishindwa kuihimili na kudondokea upande wowote. Alishindwa hata kunyonya maziwa ya mama yake vizuri mpaka kwa kulazimishwa.

Hata alipofikisha umri wa miezi mitano maendeleo yake bado hayakuwa ya kuridhisha, hakuweza kukaa wala kutambua kitu chochote kilicho mbele yake na bado shingo yake iliendelea kulegea.

Kwa mujibu wa uchunguzi na ushauri wa wauguzi na madaktari walisema kwamba mtoto Dickson ameathirika kwenye ubongo na ikatakiwa aanze mazoezi ya mwili huko katika hospitali ya Muhimbili na baadaye CCBRT hadi mwaka 2005, hadi alipopatikana mwuguzi wa kuja kumhudumia nyumbani baada ya kukosa uwezo wa kumpeleka hospitali kufanya mazoezi kila siku. Hata alipofikisha umri wa miaka wa mitatu bado maendeleo yake hayakuwa ya kuridhirisha.

Athari alizonazo Mtoto Dickson

1. Ulemavu wa viungo, miguu kupinda, mikono kulegea na uzito kupita kiasi kuliko umri wake.
2. Hawezi kusimama, kutembea, kuongea wala kutambaa.
3. Kutojitambua kama anapata haja ndogo au kubwa.
4. Kutokuwa na ufahamu wa kutambua kitu chochote.
5. Kwa sasa Dickson ana umri wa miaka kumi (10) na hakuna mabadailiko yoyote zaidi ya kuita “Dada” au “Mama”

Msaada unaohitajika
Kwa sasa Dickson ana umri wa miaka kumi (10) na hakuna mabadailiko yoyote zaidi ya kuita “Dada”au "Mama".

Mama wa Dickson anaomba msaada wa matibabu ikiwezekana mtoto apelekwe nje ya nchi kama India au popote. Mtoto Dickson anaishi na Mama yake maeneo ya Tabata hapa jijini Dar Es Salaam. Pamoja na mwili na umri wa miaka kumi (10) aliyonayo, akili yake ni kama ya mtoto mwenye miezi miwili

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na
Mama Dickson mwenyewe kwa simu:
0715 606161






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Mtoto anasumbuliwa na Celebral palsy.Ndio physical rehab ya nguvu inatakiwa/ilitakiwa tangu akiwa mdogo.Lakini si late kuanza.Results.....

    ReplyDelete
  2. Kwanza kabisa habari hii inanikumbusha kazi niliyonayo nyumbani NAMI nina mtoto ambae nae ana tatizo kama hilo la kulegea au kukakamaa kwa viungo ambayo inafanya mtoto apate ulemavuu huo kutokana na viungo kutokua katika mijongeo inayotakikana. Mwanangu ana umri wa miaka 2 alipata tatizo hili wakati anazaliwa ubongo wake uliathirika baada ya kukosa oksijeni kwani alichelewa kutoka.
    baada ya wiki moja mtoto akapata manjano ndio kumpeleka Muhimbili na kulazwa yeye na PACHA wake ambae hana shida kwa mwezi mmoja.Baada ya kutoka hospitali akaanza kushtuka ndio kumrudisha kwa DR.Masawe hapo Kona ya Moroko ndio kuanza DOZI na kumpeleka CCBRT kuanza mazoezi.
    WATAALAMU hawa wanadai tatizo hili linatatuliwa kwa MAZOEZI ambayo yanamsaidia KUMALIZA KABISA AU KUPUNGUZA MADHARA KWA MTOTO.
    Kwa huyu wangu namwona anajitahidi kidogo japo dokta anasema tuzidishe MAZOEZI.
    Nina mwomba Mama Dickson ajitahidi Mazoezi SANA huku anatafuta namna ya KUMSAIDIA ZAIDI MTOTO.
    AWE YEYE KWA KIPINDI HIKI ALICHOAMUA KUTAFUTA NAMNA NYINGINE YA KUMSAIDIA MTOTO BASI AZIDISHE MAZOEZI KILA SIKU MARA TATU AU ZAIDI.
    Wadau nategemea nanyi mnaweza kutupa mengi zaidi kwani kijiji hiki pia kina wazee.
    Wapo watoto wengi sana ambao wanasumbuka kwa ulegevu wa misuli na kukakama kwa viungo kunakowasababishia ulemavu.
    HAPA NATUMAINI TUNAWEZA PATA NJIA KUMALIZA TATIZO HILI.

    ReplyDelete
  3. Mama Dickson
    Una hakika ulimpeleka huyo mtoto CCBRT?
    Nilijifungua mtoto kama huyo february mwaka jana na iliwachukua miezi tu CCBRT kunyoosha miguu na ikakaa sawa kabisa na sasa anatembea mwenyewe. Ila ukizembea masharti miguu inarudi kama mwanzo.
    Usichoke mama rudi CCBRT na kama huna uwezo wa kwenda na kurudi lala hapo pana huduma nzuri za bure kabisa na mwanao atasaidiwa.
    Pole sana

    ReplyDelete
  4. Wakati unasubiri mikakati ya kumpeleka mtoto India, Pia si vibaya Wataalamu wanaompatia matibabu hapo Muhimbili na CCBRT ukawaeleza kwa ridhaa yako mzazi, wawasiliane na hospital kadhaa uliwenguni kwa intaneti, labda watafanikiwa mtoto kupatiwa matibabu sehemu yoyote duniani.

    Moja ya hospitali bora na ambazo zaweza kukutafutia ufadhili ni Great Ormond Street Hospital na anuani ya barua pepe ni:

    This is the joint website of Great Ormond Street Hospital for Children NHS Trust (GOSH) and UCL Institute of Child Health (ICH)www.ich.ucl.ac.uk .

    ReplyDelete
  5. maskini poleni sana mungu atamsaidia atapon inshaallah ch muhimu kumuombea dua

    ReplyDelete
  6. sijui hata nifanya nini.jamani umasikini huu.Sasa jaribu kutafuta gharama kwanza. weka hapa ni dola ngapi na tuanze harambee

    ReplyDelete
  7. ploeni sana kwa mtihani huu.najuwa vipi mnataabika kwani nauguza mtoto kama huyo lakini kama mnavyojuwa wenzetu wako in advance sana.wanachosema mtoto anafanya mazoezi sana.kwani matibabu yake ni yakuendelea.na kusema atapelekwa india kwakutibiwa na kurudi itasaidia lakini kazi ya ziada inatakikana sana kwenye mazoezi.mama mzazi tena nakupa pole kwakuuguza.

    ReplyDelete
  8. POLE SANA MAMA NA MTOTO. UMASIKINI HUU WA FEDHA NA FIKRA NI MBAYA SANA. SASA CHA MUHIMU NI KWANZA MADOCTA WA HUKO NYUMBANI WAFANYE ANGALAU KAUTAFITI DO SOME RESEARCH PLEASE YA HOSPITALI AMBAYO MTOTO ANAWEZA KUSAIDIWA KAMA HUKO KWETU WAMESHINDWA. UKISHAPATA MAELEZO YOTE PATICULAR KIASI GANI KINAHITAJIKA NA WAPI MTOTO ATAPELEKWA NDIO UTUAMBIE TUFANYE HARAMBEE. NI VIGUMU KUWAAMBIA WATU KUNAHITAJIKA PESA BILA KUWA NA DATA ZOZOTE ON HOW AND WHERE THE BOY WILL BE TREATED. KWAHIYO MAMA KAMA HAKUNA MSAADA WA MADOCTA TAFUTA MTU YEYOTE AKUSAIDIE UFANYE MWENYEWE UTAFITI WAKO SABABU UKISUBIRI BONGO HAPO HAUTAFANIKIWA SANA. POLE SANA.

    ReplyDelete
  9. Michuu
    Hebu msaidie huyo mama tupate gharama halisi za matibabu na mambo mengine tumsaidie tulicho nacho.

    ReplyDelete
  10. watu mnaoanza kutoa diagnosis ya tatizo la mtoto huyu hapa wakati information zinazoweza kotoa diagnosis hazijitoshelezi kabisa mnachokifanya sio jambo la busara.
    pia mkumbuke kwamba diagnosis ina criteria zake zinazzotumika hadi kufikia preliminary diagnosis na zinazotumika kufikia final diagnosis.
    kwa wale pia mnaosema nilikuwa/nina mtoto mwenye tatizo kama la huyo wako,pia conclusion zenu sio sahihi,maana magonjwa toffauti yanaweza kujionyesha kwa muonekano wa nje(clinical presentation) unaofanana,lakini sababu zake ni tofauti kabisa na tiba yake pia ni tofauti kabisa. hivyo basi nacho kushauri mama mwenye mtoto huyu:-
    1.Endelea kufuata ushauri wa daktari anayekushughulikia kwa sasa,kama ataona kuna umuhimu wa kukuelekeza kumuona specialist wa ungonjwa anaoona kutokana na uchunguzi wake wa awali unamsumbua mwanao basi atakwambia kufanya hivyo ndipo uanze hatua zinazohitajika.ama kama unahitaji msaada wa kifedha kwa ujumla kama sehemu ya kukusaidia kutokana na kuwa katika wakati mgumu hilo silizungumzii una haki ya kufanya hivyo.
    2.usije kushawishika kuingia katika tiba za kienyeji za kubahatisha kwani zitakusumbua tu bure.
    3.unahitajika kuwa mvumilivu kisaikolojia,kwani nafahamu unapata wakati mgumu kwa tatizo la muda mrefu la mwanao.
    4.epuka ushauri wa watu ambao sio madaktari kuhusiana na tiba ya mwanao,wataishia kukuchanganya tu.
    Dr.

    ReplyDelete
  11. wewe anoni Dr. hapo juu mama amepitia yote hayo na madaktari wa hapa wamefikia hatua yao ya mwisho ambayo wamefanya kiutaalam hivyo mama anataka kwenda India kwa kupata matibabu zaidi.Sijui kama madaktari wake wa kwanza hapo bongo wamesema kwamba India atapona au atapata matibabu gani ya kumsaidia mimi sijui. Ila kama atapata matibabu India na gharama tutazimudu basi tumpeleke.

    ReplyDelete
  12. anonymous wa feb 26,12:47:00 hapa ushauri naoutoa sio kwa ajili ya malumbano,mimi kama daktari nafahamu ninachokisema na ushauri ninaoutoa unalenga kumsaidia huyo mama. katika fani ya udaktari tunajali binadamu na lengo ni kuboresha afya kama sio kuirejesha katika uzima wake kabisa inapowezekana. sasa kama ameambiwa na daktari anayemtibu kuwa kwa uwezekano wa kutoa diagnosis kamili kwa huko tanzania haupo na wamemshauri akachunguzwe zaidi india na wanauhakika na ikiwezekana wanafahamu sehemu anakoweza kufanyiwa uchunguzi wa kina huko india,au wamesha itoa diagnosis ila tiba wanatarajia ikafanyike india hapo nitakubaliana na wazo lake la kwenda waliko muelekeza huko india. lakini kama ni ushauri tu wa ndugu au watu wanaodhani wanahuruma zaidi na wakifikiria kwenda india ndilo suluhisho ndiyo maana ninamshauri kama nilivyosema hapo juu.
    anyway hayo ni maamuzi yake,ieleweke sijazuia kuwa asisaidiwe kifedha la!hasha.hilo mimi sijalizungumzia kabisa. ukumbuke kuwa mgonjwa anachohiaji ni kuona matokeo haraka,na daktari anachofanya ni kile ambacho anafahamu kinawezekana kiasi gani kutokana na chanzo na itachukuwa muda gani na kugharimu kiasi gani pia. hata huku nilipo pia gharama za yeye kumleta kijana na kuangalia uwezekano wa kupata huduma tarajiwa sio haba. hiyo ushauri wangu narudia msikilize daktari anaye mtibu mtoto alichokushauri.
    Dr.

    ReplyDelete
  13. Dr. uko right. Kwani daktari anayemshughlikia huyo mtoto amemshauri akatibiwe India au mama mtoto ndio kiajiamulia mwenye tuu? Kila mtu ana haki ya kutibiwa popote atakapo, lakini kweli madaktari wetu wameshindwa kudeal na issue ya huyo mtoto. I think we need more information before giving more opinion on this matter.

    ReplyDelete
  14. Dr,
    Kama kweli wewe ni Daktari ni wale wenye vyeti vya kufoji. Medical Assistant siyo Daktari ni mganga msaidizi. Utabishanaje na watu ambao wmeiishi/wanaishi hali hiyo? Kama kweli ungekuwa Daktari walau hata ungechambua kidogo tatizo kuliko kung'ang'nia achiwe daktari anaye mtibu. Anayemfahamu daktari ni mama mwenye mtoto au ni wewe. You suck!

    ReplyDelete
  15. NAOMBA KUCHANGIA KIDOGO SIO MALUMBANO ILA NI UREFU WA MAWAZO YANGU NA HALI NILIYOIONA KTK MAISHA. - HATA MIMI NI MWANAMKE NIMEUGUZA MTOTO KAMA HUYU NA KWA GHARAMA YA KUBWA NAMSHUKURU MUNGU ALINIPA UWEZO NA MTOTO ANAENDELEA VIZURI.

    CHA KWANZA NI MAZOEZI (MATIBABU)CCBRT - NAJUA INACHOSHA JAMANI HUNA GARI KUGOMBEA DALADALA KILA SIKU, NA MTOTO, NAULI, ILA KWA UWEZO WA MUNGU UTASHINDA, NILIENDA MIAKA 2 BILA KUKOSA ILA J2 TUU NA SIKUKUUU ZA TAIFA (MAMA JIPE MOYO)NYUMBANI USIPUMZIKE TENGENEZA VYOMBO YA MAZOEZI KM VYA CCBRT TUMIA LOCAL MBAO.

    PILI DAWA ZA KIDAKITARI (NAMAANISHA KWAMBA DAWA UTAKAZOSHAURIWA NA DAKTARI TUU, PIA WASILIANA NA MADAKTARI TOFAUTI, HASA SPECIALIST, WATAFUTE SANA ( NA PIA HIZI DAWA ZA VITAMINS - KAMA GNLD, FOREVER LEAVING)


    MIMI NAMUUNGA MKONO HUYO MAMA KUJARIBU KILA KINACHOWEZEKANA. HATA DR ANAWEZA KUSEMA USIENDE HATAPONA LAKINI UTAALAMU UNATOFAUTIANA (1) SAMAHANI, KWA ASILIMIA KUBWA UGONJWA KAMA HUO NI NI MZIGO WA MAMA. (2) MAMA KAZA MWENDO KAMA UMEPATA MATIBABU HAPA JIPE MOYO USIOGOPE UTAPATA WASAMARIA ATAPONA TUU.

    MADAKTARI WANACHONIUDHI HASWAA HAPA TZ, WANAKATA TAMAA KULIKO MGONJWA, UTASIKIA MAMA HUYU HAWEZI KUPONA TENA NAKUMBUKA NILIAMBIWA PALE MUHIMBILI WODI YA WATOTO NILILIA SANA NURSE WALINIONE HURUMA HADI KUNIBEMBELEZA, NILIMWANGALIA MUNGU NAJUA NIKAKAZA MWENDO KILA KWA DR NILIYE MSIKIA.

    PILI DR HAWAFANYI UCHUNGUZI NA KUPATA SOLUTION YA MATIBABU, SIJUI KAMA NIMEELEWEKA. (MTOTO AKIPATA NAFUU KIDOGO TUU UTASIKIA MAMA MTOTO AMEPONA ACHA USUMBUFU - JAMANI UDR HUU WA TZ)

    NINA MENGI ILA mama jipe moyo najua umeathirika kisaikolojia ila jishike kwa mungu atakupa nguvu.

    MWISHO MPELEKE KWENYE MAOMBI YA MUNGUUUUUU USIACHE.

    ReplyDelete
  16. Anoni anayemjibu Doctor anoniFebruary 26, 2010

    Anoni(Dr. hapo juu) hapana wewe umenielewa vibaya hata na mimi sina malumbano na wewe. kwanza mimi si dokta. Ila nilichosema na wewe umekirudia ni kwamba iwapo madaktari hapo bongo wamesema kama atakwenda India atapona(kutibiwa mpaka apone) au kubolesha afya yake kama si kuitibu kabisa basi tumchangie aende India. Je ushauri wa kwenda india kapewa na nani hapa ndio sijui na wewe umesema kama madaktari wake wamemshauri hivyo baada ya kujua tatizo nini basi aende. mimi ninaunga mkono aende India. Ni kama ulivyo sema kwamba asiende tu bila ushauri wa Madaktari wake. OMBI KWAKO DOCTOR-JE KAMA UPO TANZANIA UNAWEZA KUONGEA NAYE HUYO MAMA HATA TU IWE ORAL CONSULTATION KWA NIAMBA YA MTOTO WAKE ILI UPATE PICHA .Mimi nime-hisi wewe ni real Doctor and you are a Honesty Guy Please Help.

    ReplyDelete
  17. Mama kwanza nakupa pole sana. Mimi natamani sana ningekuwa karibu nikaongea na wewe ana kwa ana maana najua haswa unachokipitia kwani hata nami nimekuwa kwenye mahangaiko hayo huu ni mwaka wa 12 sasa na mtoto wangu hajafanikiwa kutembea. Nakuomba tu kwanza ukubaliane na ukweli kuwa mtoto anaweza kupona au asipone kabisa apate nafuu tu inategemea ubongo wake uliathirika kiasi gani. huo ndio ukweli ukiukubali itakusaidia sana usiumie nafsi yako maisha yako yote. Tiba kubwa ya watoto hawa ni mazoezi yasiyokuwa na mwisho yanabadilika tu kulingana na hatua mtoto anayofikia na hili utalipata kwa wataalam wa watoto wenye matatizo kama haya. Ukikazana na mazoezi atabadilika kwa kiasi fulani na ataweza kujisaidia mwenyewe baadhi ya vitu. Hili swala linatesa sana ukiamka, ukilala haswa mwenzio wa karibu anapokimbia na kukuacha peke yako. Wakati ukisubiri kupata mfadhili kazana na mazoezi sana sana bila kuchoka. Amini pia kuwa mungu anajua faraja yako iko wapi na hakika atakupatia.

    ReplyDelete
  18. Anonymous wa feb26,08:53:00 ninaweza kufanya consultation na huyo mama japo siko hapo tanzania,nikampa muongozo wa nini kinahitajika kufanyika,lakini pia nitahitaji daktari ambaye ata mfanyia examination nitakazo hitaji zifanyie physically ili anipe majibu ya kidaktari. pia nitahitaji lab tests zikiwemo biochemical tests,genetical analysis,radiological immaging na functional diagnostic test zingine kama myography n.k na majibu pamoja na image nilizotaja zitumwe kwangu. ningependa kama atapata mtu wa kurahisisha hilo kwa njia ya computer ili niwe zazidownload,na ikiwezekana tunaongea moja kwa moja na ikiwezekana atakaye msaidia mawasiliano ya computer awe web camera.
    napenda tu kusema nitahitaji daktari awepo(yeyote)kwa ajili ya kushirikiana naye.sasa sifahamu kama vipimo nitakavyohitaji vinafanyika hapo tanzania.tunaweza kuwasiliana kwa garama nafuu kupitia internet services,kupitia skype.kama hili linawezekana nipe taarifa zaidi hapa.
    Dr.

    ReplyDelete
  19. sasa maelezo mbona hapa hakuna?mf.akaunti yake,je ameshauriwa na daktari aende uko?cheti tukione,,ili tujue tunatoa msaada kwa mtu genuine sio wala mboga tu

    nina maana yangu michuzi,au labda utuhakikishie unamfahamu vizuri uyu mtu,au yoyote alotoa hii mada

    jamani dinia mjini apa?ohoo

    ReplyDelete
  20. pole sana mama,mtoto hujachelewa mtumainie mungu atapona kabisa.kama upo dar nakushauri mpleke mtoto kwa mwakesege pale biafra mwezi wa tatu anakuja.au kwasasa unaweza ukaenda pale EFATHA MWENGE IJUMAA SAA MBILI HASUBUHI KUNA SALA YA UKOMBOZI.YESU ANAWEZA YOTE KWA YEYE AAMINIYE. USIHANGAIKE KUOMBA KAMA OMBAOMBA YESU ANAPONYA BURE.

    ReplyDelete
  21. jamani sa ingine watu tuwe na lugha nzuri! Dr amejitolea ushauri wewe mtu unamwita Dr fake! yeye ni dr ndo maana hii habari imemgusa na ametoa ushauri kidaktari, sasa wewe unayemwita fake unasaidia kweli au ndo kukatishana tamaa kusiko na maana? naamini mama mwenye mtoto ata appreciate kuona kuna doctor anachangia kuliko wewe unayemponda, grow up man, kama ni wivu acha, this is a serious matter, ondoa utoto wako hapa!mfyuuu(and yes, huo ni msonyo!)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...