huyu bwana anajiita 'Nabii Tito' kila siku utamkuta na bango lake pamoja na kipaza sauti mtaa wa Azikiwe Avenue mbele ya Dar Institute akihubiri. Anayohubiri mengi ni kinyume na imani ama mapokeo ya wengi. Wadau wanashangaa na kupumbazwa na maneno yake mengi ambayo ukiyasikia utajua tunasema nini. (Kaa chonjo video yake inaandaliwa umsikilize mwenyewe.)
Ila mojawapo analohubiri akisaidiwa na kipaza sauti chake na kupingwa na wapita njia wengi ni eti kula nguruwe, kunywa pombe ama kuoa wanawake wengi si dhambi....Je, hii tuite ni uhuru wa kuabudu ama kutoa maoni?
Bongo tambarare....



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. Hakuna tatazi hapo Ankal. wewe kama kiti moto ni dhambi achana nacho na kama kuoa wanawake wengi ni dhambi usiowe. Hii ina itwa freedom of speech.Ila kama anakashifu dini zingine hii ni mabaya.

    ReplyDelete
  2. Michuzi unachekesha...nani kakwambia kula nguruwe, kunywa pombe ama kuoa wanawake wengi ni dhambi? Hizi imani za mapokeo na tamaduni za kigeni ndizo zinakufanya uamini kuwa kufanya hayo ni dhambi!

    ReplyDelete
  3. Hakuna dhambi hapo, inategemea na jamii ilivyo kukuza kama umekuzwa kula nguruwe na ukaamini nguruwe chakula bora...itakuaje dhambi.kama umekuzwa kunywa pombe na ukaamini pombe kinywaji safi...itakuaje dhambi.kama umekulia kwenye jamii ambayo mwanamke anaweza kuwa na mabwana watano na anakua na mabwa na watano...itakuaje dhambi?au umekuzwa kwenye jamii inayoruhusu mwanaume kuwa na wanawake watano na unaoa watano itakuaje dhambi?NI JAMII KWA SASA TUNA KUWA CIVILIZED NA KUONA SIO FAIR KUOWA WAKE WENGE AU KUA NA WAUME WENGI.KWA NCHI ZILIZOENDELEA ZINAWEKA SHERIA MKE MOJA MUME MOJA LAKINI KAMA HAKUNA SHERIA HAKUNA CRIME HAPO...

    ReplyDelete
  4. duh kiamaa jama atakua ana pepo la shetani berzerburi.jiadari na hao viumbe jamani

    mdau arizona

    ReplyDelete
  5. Asili yetu kabla imani zetu hazijavamiwa na wageni ilikuwa kuoa wake wengi, kula kiti moto au kiti moto pori na kushushia na uraka, mbege, ulanzi, kangara, gongo, kayoga nk. Kama kuna kosa anafanya yaweza kuwa kuhubiri katika eneo hilo-kama kuna sheria ndogo za jiji zinakataza. Ukiacha hilo kama anakashifu imani za wengine basi anatenda kosa maana anapaswa kuelezea ubora wa imani yake, sio kupiga madongo imani za wenzie.

    ReplyDelete
  6. michu wache bwana hawa na imani zao,mwambiye aitafute bibilia ya st bernabas,isisome vizuri kama akiipata, because washaificha wajanja wakuu wa imani yao na hivi sasa wamewaaachia bibilia iliyotiwa maandiko ya binadamu si ya mungu tena kwa manufaa ya kuulimwengu si kiroho tena na bibiliya hiyo ndo famous nayo ni ya kingjames,kwani mungu alikuwa kingjames?

    mnyama nguruwe kula tu kiafya si fresh,because unampika wee na kama hujampika kwa sana unaweza kufaa ukila nyama yake.YESU Hakumla nguruwe je iweje wewe ule?mapepo wabaya walikuwa wakingia kwa nguruwe na kulaaniwa iweje mnyama huyu leo awe baraka.

    unywaji wapombe unaharibu akili imesha proviwa kisayantific

    njoeni usilamuni jamani eeeh ndo dini peke ya haki mkitaka msitake mnajionea wenyewe

    big up michu

    ReplyDelete
  7. Naona "freedom of speech" inawafanya watu msitumie akili kufikiria bali kufuata moyo unavyotaka. Itafika wakati watu watasema kuoa mama yako mzazi ni sawa........kisa freedom of speech. "wake up Black man, stop picking up everything that thrown at you, use your intellect".

    ReplyDelete
  8. kama chizi au mzima sijui, lakini nielewavyo mimi ni kwamba kwenye biblia yesu hakutukataza kuoa wake wengi.

    ReplyDelete
  9. Michuzi ,

    I can't wait for that video;and by the way, I concur with you that Bongo is tambarare!

    ReplyDelete
  10. HUYO JAMAA YEEE INAMAAANA ANA DINI YAKE ALIYO ANZISHA MWENYEWE.KAMA VILE WAKRISTO ALIANZISHA JAMAA FLANI, WAISLAMI NAYO PIA, LEO TUNA AMINI MTUME NA YESU, NA UYO JAMAA NAE PIA KAANZISH ISHU YAKE KIVYAKE, WAZUNGU WANA INVENT KILAQ SIKU HAMSEMI ILA MNABAKI KUIGA TU. JAMAA KAAMUA KUTOKA KIVYAKE KWA STYLE YAKE KAMA MNAAMUA KUABUDU ABUDUNI KAMA MNAISHUZENU BASI MINDINI MPANGO SIO ETI MNATAFAKARI SAAAAAANA. AISAIDII CHOCHOTE. ASA NIKIKAA GETO NIKANYWA NGANO ZANGU NANE NIKALEWAAA NIKA LALA TU MWENYEWE ASA APO NIMEMTENDEA DHAMBI NANI. NDO MJUEGE IVYO JAMAA KADEKU ISHU KWA JICHO LA TATU AAAFUUU KATUILIAAAAA, KAONA ATA II HAIWEZEKANI KWAIYO KUMBE DINI ZIPO NYING TU ILA INATEGEMEANA NA MTU TU WE MWENYEWE UNATAKA KUFANYA NINI. KAAMUA KUANZISHA YAKE. AAAAH, AYA BASI TUSALI WAJAMENI. MAAAAAANA. KAAAZ KWEL KWEL!!!

    ReplyDelete
  11. anajaribu kuja na dini nyingine ambayo ni blend ya Islam na Christianity.

    ReplyDelete
  12. siku za mwisho manabii wataongezeka na bado

    ReplyDelete
  13. MBONA KUNA DINI BINADAMU WAWAKUHUMU ADHABU YA KIFO BINADAMU WENZAO KISA ETI WAMETENDA DHAMBI NA BADO DINI INA WAFUASI WENGI TU NA HAO HAO KILA SIKU WANAHUBIRI NI MUNGU PEKEE NDIYE ANAYEJUA HATIMA YA MAISHA YA BINADAMU?

    ReplyDelete
  14. ``
    Jamani mbona manamsakama Michuzi? Ninavyoamini siye aliyeileta hii ishu ama kuna mlokole mmoja au Islam mmoja kama huyo hapo juu anayesema Islam ni dini ya haki. Michuzi hawezi kuweka kitu kama hicho kwani yeye mwenyewe anakandamiza ulabu kama komba, Kisha anawake kila nchi ya Afrika mashariki. Vekesheni za Bujumbura kampala Maputo mnadhani ni bure?
    Wewe uliyeposti hii acha majungu tatizo liko wapi hapo?

    ReplyDelete
  15. Naamini kabisa kulingana na maandiko yuko sahihi, especially kwenye kipengele cha nguruwe na wake wengi. Kuhusu pombe, kuinywa sio dhambi,kwa mujibu wa maandiko, ila dhambi ni ulevi. Tatizo wengi hawajajuimaana ya neno ulevi,..ulevi uko wa aina nyingi,sio pombe tu.

    ReplyDelete
  16. DINI NI ZILEZILE ILA WAHUBIRI NA VIONGOZI NDIO WAMEZUKA WENGI MNO. NA KILA KUKICHA WANAPATA WAFUASI KWA WINGI SANA NI KUTOKANA NA KUTOZISOMA DINI WANAFUATA MKONDO. MUHIMU UNATAKIWA USOME NA UIELEWE DINI SIO KUKURUPUKA NA UWE NA MSIMAMO.LEO WATU WANANEEMEKA NA HIZI DINI NI MIRADI ANZISHA YAKO UONE MAMBO MSWANO. SIO MTU ANATOLEA MFANO ADHABU YA KIFO KTK DINI ZINGINE SOMA UELEWE NA UJUWE NI IPI DINI YA HAKI KABLA HUJATOLEA UAMUZI NA KUDHARAU WENGINE

    ReplyDelete
  17. Jamani huyu mdau wa Tarehe Wed Feb 17, 01:18:00 AM,mbona simuelewi anaposema mapepo mabaya yaliwaingia nguruwe enzi hizo na wakalaaniwa. sidhani kama hiyo ni sababu ya kutokumla Nguruwe wa sasa maana walioingiliwa na mapepo ni wale manguruwe wa zamani na ni miaka mingi imepita sidhani kama wale nguruwe bado wapo sasa, kama ni hivyo basi itabidi tuache kula kuku wa kienyeji maana nimekwisha washuhudia mara kadhaa wakila nyoka au vinyesi vya binaadamu.

    Pili anaposema nguruwe kumla kiafya hairuhusiwi inaonyesha ana kariri mambo maana ukiangalia karibu kila chakula kina Saidiifekti usipokula kwa kufuata taratibu fulani kama vile kuzidisha kipimo kutokuosha na kadharika nakadhalika, na hata yeye hapa anakiri kwamba waweza kufa usipompika vizuri nguruwe amesahau kwamba hata maji ya kisima ukiyanywa bila kuchemsha pia waweza kufa. (Huyu jamaa nahisi mda wake mwingi aliutumia kusoma mambo flani na si elimu dunia ndo maana kawa kituko)

    Unaponiambia nije kwenye dini yako kwasababu ni dini ya haki unamaanisha nini? Unajua haki za binaadamu wewe? Ngoja nikuambie moja ya haki za binaadamu ni HAKI YA KUWA HAI BILA KUJARI UNAKOSA GANI, BINAADAMU HUNA HAKI YA KUHUKUMU MTU KIFO KISA ETI AMEFANYA NGONO KWANI WEWE MUNGU? NA UMEKUWA MSAFI KIASI GANI MPAKA UNAMHUKUMU MTU AFE ILA WEWE UBAKI HAI?

    BINAFSI SIJI KWENYE DINI YAKO NI KHERI NIFE NIKIWA SINA DINI KULIKO KUJA KWENYE DINI AMBAYO KWA MTAZAMO WANGU NAIONA NI YA KINYANYASAJI.

    ebanaee kama vip usiipost koment yangu sibembelezi maana nawewe michuzi kwa hili nahisi umeniboa flani maana tulikukataza kuanzisha mijadara ya kidinidini(sijataja dini ya mtu hapa)

    ReplyDelete
  18. YUPO SAHIHI

    ReplyDelete
  19. TEH TEH TEH ....JAMAA NI MJASIRIA MALI PASEE,KAMA WENGINE WALIOANZISHA MAKANISA NA KUTUMIA DINI KEUNDESHA MAISHA YAO..DUNIA YENYE WATU 6BLN..ASILIMIA 60% EITHER WANAAMINI BIBLIA AU QURAN..NI MTAJI MKUBWA SANA KWA MWENYE AKILI AKI CHANGANYA KIDOGO VITABU HIVYO VIWILI..ATAPATA WANYWA POMBE,WAPENDA WAKE WENGI,NA WALA KITI MOTO (BY THEWAY HIKI NI KITOWEO TU KAMA MBWA,NYOKA,PAKA,PANYA,SUNGURA,MBUZI,SWALA..NK) ...NI MTAZAMO TU.NA MAPOKEO,NA TAMADUNI NA MILA,TULIO LETEWA NA WAZUNGU NA WAARABU..(WALIO TULETEA VITABU HIYO..KISHA WAKATUUZA KAMA NGOMBE KWENYE MNADA KUA WATUMWA,KUTUTESA,KWA VIBOKO NA KUKATWA VIUNGO VYETU..NA KUUITA UTAMADUNI WETU NI WAKISHENZI...LEO TUNA SEMA POMBE DHAMBI,KUOA WAKE WENGI DHAMBI (HII HAIJAANDIKWA POPOTE)KULA BAADHI YA VYAKULA DHAMBI....NANI KASEMA ..WAMAKONDE WANA USEMI ,,CHAUMBILE MNUNGU CHAKUMEMENA....SO NABII HUYO ANATAFUTA MKATE WAKE WA KILA SIKU..KAMA WENGINE WALIANZA HIVI SASA WANA MILIKI HAMMER,ARMADA NK..NA NIMA MULTI MILIONEA...WANA MABENKI,TV,RADIO...NA ALOT OF LIQUID CASH IN ACCOUNTS...WAUMINI WANABAKI KUSIFU NA KUAMINI NAO SIKU MOJA MUNGU ATAWAFUNULIA NA KUWAWEZESHA...DREAM ON GUYS AND WAKE UP...BY THE WAY HUU NI MTAZAMO
    TU

    MDAU ..LOBOKO LOBII PAPAA

    ReplyDelete
  20. WENGI MLIOCOMMENT HAPA HUYU MTU HAMJAWAHI KUKUTANA NAE MIMI NILISHAKUTANA NAE NA KWA HARAKA HARAKA ANAONEKANA KAMA MTAMBO FULANI NI MBANGAIZAJI ILI APATE KITU CHA KUSUKUMA SIKU. KUCHUKUA BIBLIA KUINGIA NAYO BAA NA KUANZA KUHUBIRI KUWA POMBE SIO HARAMU NA YEYE MWENYEWE ANAAGIZA NDOVU NA KUNYWA NA UKIGUSWA MCHANGIE AENDE MIKOANI KUHUBIRI NI JAMBO LISILOKUBALIKA HATA KAMA WEWE NI WA IMANI NYINGINE

    ReplyDelete
  21. Hata mimi naamini kunywa pombe, kula nguruwe na kuoa wanawake wengi si dhambi. Hayuko pekeyake

    ReplyDelete
  22. ANKO MICHUZI HONGERA SANA KWA KUTULETEA HABARI ZA KIJAMII.KWA UJUMLA HUYU ANAFANYA KILE AMBACHO NI CHEMA SANA KUTOKA KATIKA MOYO WAKE MWENYEWE.KWA WASOMAJI WA BIBLIA NAWAOMBA WAENDELEE KUSOMA NA KUTAFAKARI MANENO YA YESU KATIKA YOHANA 8:32.MADOKEZO YANAPATIKANA KATIKA MSTARI HUU NI MUHIMU SANA KWETU SOTE AMBAO MSINGI MKUU WA IMANI YETU NI BIBLIA.NI LAZIMA TUWE WATAMBUZI KATIKA HOJA YA NGUVU NA NGUVU YA HOJA.KWA HIYO NI JUKUMU LA WADAU WA GLOBU YA JAMII KUACHA KUMBEZA HUYO ANAYEJIITA NABII NA KUJIHOJI NAFSINI MWAO IWAPO KWELI IMANI YA KILA MDAU AMBAE NI MKRISTO IMEJENGWA IMARA KATIKA MSINGI WA BIBLIA NI IMANI YENYE KUYUMBISHWA NA KILA UPEPO UVUMAO.

    ReplyDelete
  23. KWA WASOMAJI WAZURI WA BIBLIA WANA KUMBUKUMBU NZURI YA MANENO YA YESU KATIKA YOHANA 8:32.
    KUPITIA MSTARI TUNATIWA MOYO TUJENGE IMANI YETU JUU YA MSINGI WA BIBLIA TUKIWA NA NGUVU YA HOJA NA SIYO HOJA YA NGUVU HUKU TUKIENDELEA KUTAFAKARI JUU YA YALIYO MEMA NA KUEPUKA KUPEPERUSHWA NA KILA UPEPO UVUMAO.
    R.Njau
    Dsm

    ReplyDelete
  24. mdau Wed Feb 17, 01:18:00 AM umenena. lakini mbona suala la wake wengi hujalizungumzia? ebu rudi utuambie kama angalau hapo unampongeza au unampinga kama ilivyoandikwa kwenye hiyo biblia ya st.bernabas.
    haramu yako, halali ya mwenzako.

    ReplyDelete
  25. Kweli nimesoma kwa makini comments zote hapo juu kuna waliotumia busara na wengine kwa kweli ni makanjanja wa hoja yangu ni mawili tu
    1 Hizi dini za sasa zimetoka wapi?hazikwandikwa na binadamu wenzetu wenye maono?

    2Mmesikia hoja zake kwanini anahubiri hivyo?
    mwisho mababu zetu walioa wake zaidi ya 4,wakala kitimoto,wakabwia na mvinyo wakaishi miaka mia na zaidi kwa baraka za huyohuyo mola je mmejiuliza hayo?akiwa mzungu tunatafakari ku msupport au kumpinga but huyu mweusi hana nyimbo with direct conclusion tubadilike sisi wabongo ndiyo maana kwenye ma Interview tunafeli because of level of analysis

    ReplyDelete
  26. JAMANI DINI NI IMANI YA MTU DINI NYINGINE WANAISHI NA MAJINI ETI NI VIUMBE WA MWENYEZI MUNGU,WENGINE MUNGU WAO NI NG'OMBE HUKO INDIA KWA HIYO TUMUACHE HUYO NABII AHUBIRI ANAVYOJUA

    ReplyDelete
  27. mababu zetu waliamini kuna MUNGU anaitwa KYALA au NGULUVI ambaye ni sawa na huyo mungu wa waarabu au wayahudi waliishi maisha safi tu leo wamekuja wageni wametubadilisha hata majina yetu ya asili kweli huu ni ukoloni maomboleo unakuta mtanzania hujui hata jina la ukoo wake kisa dini za wayahudi na waarabu!it is very sad

    ReplyDelete
  28. jamaa anahubiri safi tu ila hayo mahubiri yake aendelee kuhubiri hapo hapo bongo akienda kwa waarabu watamuua kuhusu kiti moto

    ReplyDelete
  29. mtoa maoni unayesema kuwa hizi dini ziliandikwa na wanadamu kama sisi hapo unakosea je hujui kuwa kuna kitabu kilishuka toka mbinguni kama kilivyo hii leo?je kuuliza wahusika wakusimulie usiwe unakurupuka na makanjanja yako

    ReplyDelete
  30. jamani watanzania wale ambao wanaona dini yao ni safi tunaomba waombee amani kule somalia kwani nao ni watu kama siye wanahitaji amani ilil kujadiliana mijadala kama hii ya kwetu

    ReplyDelete
  31. VITABU VYA MUNGU VIMESEMA '...WATAKUJA MANABII WA UONGO...' kwakweli matapeli kupitia dini wakitumia jina la YESU wamezidi bongo. WAJINGA NDIO WALIWAO!!!

    ReplyDelete
  32. KUHUSU SUALA LA KUOA JAMANI NAOMBA TUSOME MATHAYO 19;1 au kitabu cha torati ya musa yaani MWANZO 2;24

    ReplyDelete
  33. jamani tusibishane kuhusu wayahudi au waarabu nani ni nani wote tunaongozwa na amri 10 za mungu tusome kutoka 15;22-20;26 au kumbukumbu la torati 5;1-17

    ReplyDelete
  34. mtoa maoni wa WED FEB 17 08;54;00 AM NAKUPONGEZA KWA COMMENT yako nzuri nakuomba tuwasiliane nami makoyehayes@yahoo.com

    ReplyDelete
  35. hongera kaka mithupu kuhusu dini ya kweli na haki ni usimtendee binadamu mwenzio jambo ambalo wewe hauwezi kujitendea au unaliogopa ok tuache ubabaishaji ni haki ya kwanza ya binadamu ni KUISHI HURU

    ReplyDelete
  36. hii bongo tambarale ya kamanda wa ffu oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  37. Huyo ni KAMANDA, keshajipindia msimsumbue mwacheni na raha zake

    ReplyDelete
  38. du tz nomaaaaaaa nimepamisi vimbwanga vyake

    ReplyDelete
  39. Mi nawashanga wengi humu kwa kumjadili huyu mtu,Huyu jamaa hajazidisha kitu katoa hadi AYA UKASOME tena za Bibilia mbona mnamlaumu kuwa dini yake sijui hii mara mmbabaishaji SASA HAYO SI MAANDIKO JE KUNA AYA ALOTOA PALE INASEMA NABII TITO 3:7 AU AMETOA MATHAYO NA WENGINE?KAMA HAYO ALIYOYAHUBIRI NI SAHIHI HAJAENGEZA BASI YUPO SAHIHI OTHERWISE APATE MTU WA KUMUELEWESHA NINI MAANA YA HIZO AYA ZAKE AU LABDA BIBLIA INA JI CONTRADICT WENYEWE.KWA KUONGEZEA NENDA KASOME WIMBO ULIO BORA 7.1 UONE MWANAMKE ANAVOSIFIWA JE UTASEMA NI KASHFA AU PEPO? SITI MSHARIFU MAPAJA YAKO MAPAJA YAKO KAMA JOHARI,KITOVU CHAKO KITOVU CHAKO...TUMBO LAKO TUMBO LAKO...HIYO NI AYA YA BIBILIA JE NA MWANDISHI ANA PEPO?(UGIRIKI)

    ReplyDelete
  40. Anon wa Wed Feb 17, 03:28:00 PM,

    Nijuwavyo kuna Mungu(Muumba) na viumbe (watu, malaika, majini, ngombe, miti, nchi, wewe n.k.).

    Majini wako katika kundi lipi au walipatikanaje?

    ReplyDelete
  41. Huyu mpatieni ticket afike hapa New York times square watu kama yeye wapo kwa wingi tu! Hata naked cowboy yupo na gitaa lake. Hivyo atapiga domo mpaka achoke tu.

    ReplyDelete
  42. hivi dhambi nini?nachojua mimi mtu mweusi ana hicho kitu,na kama kweli hicho kitu dhambi kipo ni cha waarabu na wazungu,lets go back to the history,dini tumeletewa tu na hao watu niliowataja hapo juu,mtu mweusi ana dini sema tunajipendekeza tu

    ReplyDelete
  43. MAJINI = MASHETANI

    ReplyDelete
  44. Nabii wa uwongo huyo...msidanganyike, agent wa kuzimu mtumishi wa shetani, mwisho wake ni mbaya sana, siwezi kusema hajui atendalo...anajua atendalo na anamikataba na shetani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...