Mwimbaji wa zamani wa bendi ya Orchestra Marquiz du Zaire enzi za "Kamanyola bila Jasho" na "Chekecha Telemuka" mzee Mtombo Lufungula Audax akiongea na mwandishi Woinde Shizza wa Globu ya Jamii jijini A-Taun nyumbani kwa mtoto wake ambapo anaugulia mzee Audax amemtumia salamu za pole Babu Seya na hongera kwa watoto wawili walioachiwa. Pia anawasalimu wapenzi wote wa Maquiz waliokuwa wakiselebuka wote enzi za White House, DDC Kariakoo na kwengineko.
ALIYETUNGA KIBAO CHA `MPENZI RUTA`
ATUMA SALAMU KWA BABU SEYA.

Na Woinde Shizza, Rombo
Mmoja wa wanamuzi mahiri na wa siku nyingi nchini ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo ya Mpenzir Ruta ,Mzee Mutombo Lufungula Odax ambaye kwasasa yupo mkoani Kilimanjaro ,ametuma salamu za pole kwa mwanamuziki mwenzake ambaye walishirikiana naye kuimba pamoja katika bendi ya Gabijazzy kabla ya kubadilishwa na kuitwa Marquiz du Zaire.

Mzee Odax, akiongea nyumbani kwa mtoto wake katika wilaya ya Rombo, alisema kuwa anasikitishwa na kitendo cha Babu Seya na watoto wake kukumbwa na matatizo hayo na kwamba anamuombea kwa Mungu aweze kufarikjika na kutoka kwa msamaha wa Rais.

Odax alisema kuwa kibao cha Mpenzi Ruta ambacho alikitunga mahsusi kwajili ya mpenzi wake alishirikiana kuimba na waimbaji mbalimbali akiwamo Babu Seya ambaye alishiriki katika uimbaji na kusherehesha kwa gitaa nyimbo hiyo kiasi cha kupendwa na nchini na hata nje ya Tanzania .

Alisema kwamba anamkumbuka Babu Seya hasa katika umahiri wake katika nyimbo na maudhui ya nyimbo alizoimba na kushirikiana katika utunzi na Babu Seya ni pamoja nyimbo iitwayo 'Seya ya Mwivalo' ambaye alimtungia mwanamke mmoja jiji Dar es salaam.

Alisema kuwa uwanja wa muziki nchini Tanzania imepata pigo kwa masahibu yalimkuta mwanamuzi huyo mkongwe na kuwataka watanzania kuombea ili aweze kuachiwa kwa msamaha wa Rais na kwamba bado anamkumbuka na kumpa pole.

``Namkumbuka sana Babu Seya kwa kuwa tulikuwa naye katika bendi moja na tulishirikiana katika kila jambo na hasa katika nyimbo ya Seya wa Mwivalo ambaye tuliimba naye kwa umahiri mkubwa na hata katika vibao nvingine tulishirikaiana vizuri ``Alisema Mzee Odax.

Alisema kuwa neno liitwalo `Seya wa Mwivalo`linamaanisha msichana ambaye alipaswa kuwa mpenzi wa Babu Seya na walitunga nyimbo hiyo wakiwa vijana katika kikundi cha Skauti. Alisema Nyimbo hiyo iliyotungwa katika ya miaka ya 1984 na 1986 ilibeba ujumbe wa kweli na kwamba kila anapousikiliza anamkumbuka Babu Seya .

Amesema kibao chake cha 'Mpenzi Ruta' alishirikana kuimba na Babu Seya, Kasaloo Kyanga, Farashi Bukumbule na Kiniki Kieto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Huyu mwandishi wa blogu ya jamii apunguze trupa na nyama choma ambazo zinapatikana kwa wengi sana A-tauni

    ReplyDelete
  2. ka mithupu namimi nataka nihojiwe na huyo mwandishi wa globu ya jamii nyumbani kwangu

    ReplyDelete
  3. wewe "ankali" picha nyingine unazo weka huku uwe makini, watu wanaweza kula ugali kwa picha ya samaki. Hohooooo!!!

    ReplyDelete
  4. Mwandishi wa Blog safiii sana. Kabeba vifaa adimu ambavyo ni chachu ya ...no.

    ReplyDelete
  5. Halafu pesa atakayosevu huko kwenye nyama choma na bia basi anunue kamera yenye resolution nzuri.

    ReplyDelete
  6. jijini A-taun? sijaelewa

    ReplyDelete
  7. teh teh teh teh aaaaaanha!! teh teh teh, haka kapicha kazuri kwelikweli ankooooo!! teh teh teh teh teh ankoo poa sana man. Jamani karibuni mezani Ugali Umeiva, leo ni ugali kwa sangara toka mwanza teh. karibuni sana teh teh teh niko tonge la tatu sasa teh teh teh eeeeeeenhe globu yetu hii bwana!!! te teh ahsante sana mwanangumwenyewe michu taswiraz hizi zinantoa sana kiana.

    Mdau wa Pajazzz+titizzz

    ReplyDelete
  8. naomba uniwekee namba ya ya simu ya audax please ni mimi jean claud londre.

    ReplyDelete
  9. Naapa kwamba comments nyingi zitakuwa ni juu ya mapaja ya huyo msichana. NAAPA...tAYARI WANALALAMIKIA RESOLUTION MBAYA

    ReplyDelete
  10. DUH, WABONGO KWELI TOME-LOST. DADA WA ATU KAVAA MAVAZI YA KAWAIDA, LAKINI WATU TAYARI MACHO YANAWATOKA. GREW UP PEOPLE!!! HUYU DADA KAVAA KAMA WANAVYOVAA WAKE ZETU NA DADA ZETU MAJUMBANI.

    ReplyDelete
  11. Nakuunga mkono anon wa 12:53 am yaani mtu akiona mwanamke mwingine lazima aanze kumchambua, oh hiki kiko hivi mara vile na kuweka tamaa mbele. Watu hao hao utakuta mkewe yuko safi tu lakini hata muda wa kumwangalia hana. Kazi kutamani tu wake za watu wengine. Tabia mbaya sana.

    ReplyDelete
  12. kudadadeki! kweli blog ya jamii ni starehe tosha! maana hizo comments hapo juu zimenifanya nicheke mpaka basi! hasa huyo wa pili anayetaka akahojiwe na huyo dada nyumbani kwake!

    ReplyDelete
  13. Woinde Shizza is hot kasoro hiyo minyama nyama ya tumbo ... yaani inachukiza kweli. Hebu fanya mpango uiyeyusha dadaangu.

    ReplyDelete
  14. Samahani wadau naona nimepitwa wakati nipo shambani, kwani Babu Seya ana matatizo gani ambayo inabidi msamaha mpaka utoke kwa Raisi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...