Uncle Michuzi,
Hivi sisi wa TZ ni nani aliyeturoga.Naomba siku moja upite barabara ya Kilwa road huu upane wa Service road kuanzia maeneo ya Mivinjeni hadi ufike kwenye kona ya bendera tatu ushuhudie uharibifu mkubwa wa mifuniko ya mifereji,na kingo za barabara.
Hata kituo cha basi pale karibu ofisi za Mabruda wa Benedictine kimelambwa na magari na hakuna mtu anayejali wakati watu wa Tanroads wapo,na Polisi wanapita njia hiyo kila siku.Barabara haina hata mwaka lakini ukifika hapo uone huo uharibifu unaofanywa na madereva wanaotanua hakika kama kweli ni Mzalendo utalia.
Mdau Kurasini.
Uharibifu ni mkubwa. Sasa tuanzie kwako mtoa malalamiko: Je ulichukua hatua gani zaidi ya kuripoti kwa globu ya jamii? Je ulifikisha taarifa hizi kwa mamlaka husika
ReplyDeleteWaliofunga viwanda ndo walioturoga, ajira hakuna, pesa hakuna, maisha magumu, si unaangalia namna ya kusogeza siku tu. Na vijijini maisha ni magumu.
ReplyDeleteBwana weee! kama kuna vitu hunitia hasira ni hayo mauharibifu ya barabarani, licha ya huo uharibifu wa kugongagonga na magari lakini pia kuna mambo ya uchafu! unakuta barabara inajengwe vizuri na mitaro mizuri kabisa cha ajabu watu tena nafikiri ni watu wazima na wala si watoto anabeba uchafu alioukusanya huko nyumbani kwake au kwenye biashara yake anaende kutupa kwenye mtaro wa maji ya mvua pembeni mwa barabara!! Ukitaka kuona maajabu nenda kwenye barabara inayokarabatiwa kwa kiwango kizuri kabisa ya Mandela. Ule mtaro ni mrefu kimo cha ng'ombe lakini wauzo bidhaa pembeni hufagia mabaki takataka zote hata samaki waliooza hutupiwa humo. Huko uchoroni Ilala kwa mfano mitaro sijui ilishatuamisha maji lini hadi ya rangi ya kijani na watu wanakaanga vitumbua hapa kando tu ya uchafu huo. Hivi vichwa vyetu vina nini hata hatuelewi huu ni uchafu hata mkatafutana watu hata wawili watatu wanaokaa karibu na mitaro hiyo na kuizibua. Hivi kweli maralia haikubariki kwa kulala kwenye chandarua tu wakati sebuleni na sehemu za mapumziko yenu kama bar mbu wanawang'ata mamilioni ya watu, mimi naenda mbali zaidi na kusema lengo la kusambaza vyandarua sio kutokomeza maralia ila ni biashara za watu tu.
ReplyDeleteLakini wakulaumiwa ni viongozi wetu hawahawa, ukitaka kuwaongoza watu hutakiwi kuwabembeleza kwa sababu inatakiwa kuweka sheria za miji kuwa kali kidogo, inatakiwa kuwekwa watu wa doria mtu akikamatwa anatupa taka ya aina yoyote au kuharibu sehemu za public apewe adhabu kali, na wataadhibiwa watu wachache tu kila mtu atatia adabu. Lakini sheria huzo zisifanywe na watu hao kuwa za kukusanyia 'kitu kidogo' na watu kubambikiwa makosa ya uharubifu huo.
Mimi nikipewa ukuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa mfano nafikiri watu wengine watarudi vijijini kwao kwa kuzishindwa sheria za mji, kweli kabisa.
Inatia uchungu sana.
Mdau wa Dar
Nimesema na narudia "matatizo ya Tanzania yanasababishwa na Watanzania wenyewe"
ReplyDelete(US Blogger)
tatizo kubwa hapa Tanzania kwetu ni watu kutofuata taratibu ambazo naamini zipo na ndio maana ukipita barabarani wakati mwingine unakuta foleni ndefu ambazo nyingine ni za kujitakia. uharibifu wa barabara zetu huchangiwa na watumiaji wabovu, mimi hukerwa na wanaotanua barabarani, kuwazibiti hawa ni ngumu kwani miongoni mwao ni hao hao wanaotakiwa ku-enforce sheria na taratibu, kama traffic anamiliki daladala atawezaje kukemea wanaotanua barabarani - kidhati?
ReplyDelete