Mheshimiwa mmoja kaniomba
niweke mwanga kwenye hili neno ambalo limetajwa hapo juu.

Katika kumbukumbu zangu, Libeneke ulikuwa mtindo wa Butiama Jazz Band, bendi iliyokuwa chini ya uongozi wa marehemu mzee Mkwega, ikiwa na mpiga solo mzee Makelo ambae yuko Shikamoo Jazz, baadhi ya waimbaji akiwemo Saidi Hamisi ambaye kwa miaka mingi mpaka kifo chake alikuwa Vijana Jazz.

Kulikuweko na wimbo ambao ulikuwa maarufu
ukiwataja wanamuziki wa bendi hiyo na kibwagizo chake kilikuwa ....
waache waseme,
watachoka wao,
mtindo libeneke utatia fora......

Mkuu wa libeneke upo?
Karibu wapenzi wa Butiama Jazz

Na mdau John Kitime
http://www.mwakitime.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. yale yale link haiko active.

    ReplyDelete
  2. Navyojua mimi Libeneke ni pombe ya "kienyeji" inayopendwa sana uswahilini.

    ReplyDelete
  3. Libeneke ni ngoma ya asili ya watu wa sehemu za Morogoro au Songea sina uhakika original yake ni Wapogoro au wandamba lakini nimeanza kusikia neno hilo miaka ya 70 katika maeneo hayo

    ReplyDelete
  4. Mdau hili neno libeneke lipo "mitaani" tokea miaka ya 70s-80s. Hao Butiama walilichukua tuu sio kwamba wao ndio waanzilishi wa hili neno. Watu tunapiga libeneke tokea long time.

    ReplyDelete
  5. Libeneke ni neno la kiswahili kisicho rasmi. Maana yake ni tendo linalofanyika kila mara na bila mwisho. Mara nyingi huwa ni tendo baya, kwa mfano. ngono, pombe, matusi, starehe kupita kiasi. Ndipo utasikia watu wanasema, "Fulani ameanza libeneke" Au mtu kalewa anaulizwa, "hilo libeneke utaacha lini?"

    Mama Gide - Tanga

    ReplyDelete
  6. Pamoja na tafsiri nyingine,Libeneke ni miongoni mwa ngoma za sie Wandamba kama ilivyo Sangula.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...