Mheshimiwa mmoja kaniomba
niweke mwanga kwenye hili neno ambalo limetajwa hapo juu.
Katika kumbukumbu zangu, Libeneke ulikuwa mtindo wa Butiama Jazz Band, bendi iliyokuwa chini ya uongozi wa marehemu mzee Mkwega, ikiwa na mpiga solo mzee Makelo ambae yuko Shikamoo Jazz, baadhi ya waimbaji akiwemo Saidi Hamisi ambaye kwa miaka mingi mpaka kifo chake alikuwa Vijana Jazz.
Kulikuweko na wimbo ambao ulikuwa maarufu

ukiwataja wanamuziki wa bendi hiyo na kibwagizo chake kilikuwa ....
waache waseme,
watachoka wao,
mtindo libeneke utatia fora......
Mkuu wa libeneke upo?
Karibu wapenzi wa Butiama Jazz
Na mdau John Kitime
http://www.mwakitime.blogspot.com
waache waseme,
watachoka wao,
mtindo libeneke utatia fora......
Mkuu wa libeneke upo?
Karibu wapenzi wa Butiama Jazz
Na mdau John Kitime
http://www.mwakitime.blogspot.com

yale yale link haiko active.
ReplyDeleteNavyojua mimi Libeneke ni pombe ya "kienyeji" inayopendwa sana uswahilini.
ReplyDeleteLibeneke ni ngoma ya asili ya watu wa sehemu za Morogoro au Songea sina uhakika original yake ni Wapogoro au wandamba lakini nimeanza kusikia neno hilo miaka ya 70 katika maeneo hayo
ReplyDeleteMdau hili neno libeneke lipo "mitaani" tokea miaka ya 70s-80s. Hao Butiama walilichukua tuu sio kwamba wao ndio waanzilishi wa hili neno. Watu tunapiga libeneke tokea long time.
ReplyDeleteLibeneke ni neno la kiswahili kisicho rasmi. Maana yake ni tendo linalofanyika kila mara na bila mwisho. Mara nyingi huwa ni tendo baya, kwa mfano. ngono, pombe, matusi, starehe kupita kiasi. Ndipo utasikia watu wanasema, "Fulani ameanza libeneke" Au mtu kalewa anaulizwa, "hilo libeneke utaacha lini?"
ReplyDeleteMama Gide - Tanga
Pamoja na tafsiri nyingine,Libeneke ni miongoni mwa ngoma za sie Wandamba kama ilivyo Sangula.
ReplyDelete