Pongezi na hakikisho hilo limetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Bibi Hanifa Karamagi, mara baada ya kufanya ziara ya kukagua mradi huo, unaomilikiwa na mwekezaji kutoka nchini Uingereza, kampuni ya Sun Biofuels, ambayo inafanya mradi wa kilimo cha zao la Jatropha, au jina maarufu la Mibono Kaburi, kwa lengo la kuzalisha mafuta ya dizeli.
Bibi Karamagi ametoa pongezi kwa mwekezaji huyo kwa kutoa ajira rasmi zaidi ya 400 kwa wanavijiji wa vijiji vinavyozunguka mradi huo ikiwa ni pamoja na kuwalipia mafao NSSF, na kusema ajira hizo zitaboresha maisha ya wanavijiji hao, na akawasisitiza wanavijiji hao, wasibweteke na fedha za mishahara kwa kufanyia starehe, kulewa na kuongeza idadi ya wanawake, bali wazitumie fedha hizo kuboresha maisha yao na kujiletea maendeleo, ikiwemo kuendeleza kilimo cha mazao ya chakula huko vijijini kwao.
Bibi Karamagi amesema, kampuni hiyo ya uwekezaji toka nchini Uingereza, ilifuata sheria, taratibu na kanuni zote za uwekezaji na umilikaji ardhi ya vijiji kwa mujibu ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya Mwaka 1999, ikiwemo kulipa fidia stahiki kwa vijiji husika, hivyo serikali inafanya uchambuzi yakinifu kubaini kama kuna wanavijiji wowote ambao hawakupata malipo ya fidia zao kwa namna moja ama nyingine.
Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa amefuatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe, amejionea takriban hekari 1000 ambazo zimeshalimwa na kupandwa zao hilo, ikiwemo kushuhudia baadhi ya micheche ambayo tayari imeshazaa matunda hayo ambayo mbegu zake hutumika kuzalisha mafuta ya dizeli ambayo ni rafiki wa mazingira.
Akimkaribisha mkuu wa wilaya, Meneja wa Kampuni hiyo ya Sun Biofuel nchini Tanzania, Peter Auge, amesema, kati ya ekari 8200 ambazo kampuni yake imemilikishwa, ni 6,000 tuu ndizo zitatumika kwa kwa kilimo cha mibono, na eneo lililobakia litatumika kama eneo la hifadhi ya misitu asilia. Pia kampuni hiyo, itaongeza ajira toka 400 zilizopo sasa mpaka 1500 katika kipindi cha miaka mine ijayo.
Vijiji vya Mtamba, Muhaga, Marumbo, Paraka, Kidugalo, Kului, Mtakayo, Vilabwa, Mitengwe, Mzenga ‘A’ na Chakaye ndivyo wafaidika wakuu wa mradi huo, ambapo licha ya wanavijiji hao kupa ajira za moja kwa moja, kwenye mradi huo, mwekezaji huyo wa Sun Biofuel, atawajibika kuboresha huduma za jamii ukiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, na kuchangia huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo miradi ya afya na elimu.
Kampuni ya Sun Biofuel (T) Ltd, inamilikiwa kwa ubia kati ya Watanzania na Waingereza ambapo imejikita katika kilimo cha zao hilo la Jatropha kwa jina maarufu la Mibono Kaburi ambalo hustawi kwenye ardhi kame na isiofaa kwa kilimo cha mazao ya chakula.
Tanzania ina maeneo mengi yasiyofaa kwa kilimo, hivyo kuishia kukaa bure, hali inayopelekea kilimo cha zao hili la mibono, kuonekana kama mkombozi wa matumizi sahihi ya ardhi iliyokuwa inakaa bure, na wakati huo huo kutoa ajira kwa maelfu ya waTanzania.Mwisho.
kuza lisha biofuel si dhani kama ni hatua ambayo tungetakiwa kufanya kwa sasa, nchi bado haiana auwezo wa kuzalisha chakula kwa wananchi wake still tunataka kuzalisha biofuels, ambayo kwa tanzaniaa hatuna mahitaji nayo, serikali ingehamasisha wawekezaji wazawa kujiingiza kwenye kulima kilimo cha chakula kwa ajili ya wananchi wake na excess ingeweza kuuzwa njci za jirani ( regional market). ikumbukwe biofuel ni mojawapo kilichosababisha kupanda kwa bei ya vyakula duniani, siwezi kuelezea the way ningetaka kueleweka kwa ajili ya muda ila ukweli kama nchi tunachemka kumega ardhi kwa ajili ya biofuel
ReplyDeleteBwana Michuzi, Kuna Wazawa Ki-bongo wengi wanaweza kuwa wawekezaji huko nyumbani, Kuna watu wana mapesa huko Oman, Qatar, Uingereza, America , Australia, Canada na kwingineko ila tunawekewa zengwe kuwekeza.Ila wakija hawa watu wenye kuhamisha uchumi ndio tunababaika, Hili sio suala la Kibaguzi kwani wao hawajali muwekezaji anatoka wapi ni pesa yako, Ila Huko Bongo tunawekewa zengwe mara ooh umekana Uraia mara ooh tuelezee hizi pesa umetoa wapi!!??Yaani inaboa!
ReplyDeleteSijui lakini wengine mna maono gani!!??
Tunawaomba wawekezaji hao wazingatie maslahi ya taifa na jamii kwa ujumla.
ReplyDeleteMi nina wasiwasi kwamba haya mafuta ya biofuel yatakuja kututokea puani kama sio mdomoni na afadhali yatutokee mdomoni kuliko puani. Naishangaa serikali inapochukua ardhi nzuri yenye rutuba na mvua za kutosha inawakabidhi wawekezaji kwa makunmi ya miaka eti walime jatropher! Hivi hapa duniani hakuna nchi nyingine ambayo haya majatopher yanastawi isipokuwa Tanzania tu? Au kwa kuwa sie ni bongolala kila mzungu tukimuona tunadhani ni mwekezaji?
ReplyDeleteHii mimea ktk nchi zingine zenye akili hulimwa ktka ardhi isiyokuwa na rutuba(barren land) na ardhi yenye rutuba hutengwa kwa ajili ya mazoa mengine ya maana. Hapa kwetu tunagawa ardhi nzuri inayostawi mazao mengine ya maana huku tukiendelea kulia njaa. Hv sie Watanganyika tutaamka lini hasa?
wizi mtupu, sijui watu mnababaika na ngozi? wewe hizo hekari 1,000 kwa nini uweke wafanyakazi 400? Jamaa anawalimisha kwa jembe la mkono nini? Tizama hata hao wafanyakazi hali zao zilivyo duni?
ReplyDeleteKama kweli mwekezaji si aweke mashine, maana huku "danda unate mkanyage asinye, hekari 10,000 wanalima watu 3 kwa mashine.
Enzi za mwalimu Nyerere upumbavu huu usingeruhusiwa kufanyika.
ReplyDeletemnampongeza kwa lipi? mbona inavyoonekana kwa macho tu huyo mwekezaji ajali wafanyakazi wake? mbona wafanyakazi hawana hata vitendea kazi?
ReplyDeleteHii imekaaje? Mwekezaji raia wa Uingereza amepewa ardhi ya wananchi, ameanzisha mradi, wananchi hawajalipwa fidia ya ardhi. Yangewezekana haya Uingereza?
ReplyDeleteWatanzania kazi yao kupinga kila kitu, WIVU mtupu. ... Enzi za Nyerere upumbavuu usingeruhusiwa'???.. huu ni uongo wa wazi kabisa. Kama asingefanya madudu huyo nyerere asingestaafu 1985. Alishaharikoroga akaamua kujitoa ili lawama apewe mwingine.
ReplyDeleteWacha wenye hela wawekeze, iwe Mtz au mgeni. Huna hela kaa kimya tafuta vibarua, siyo kuleta lawama lisizoeleweka hapa.
Kuna busara kwa nchi ya 'wakulima na wafanyakazi' kuleta 'wawekezaji' ili watulimishe?
ReplyDeleteKuna busara kutumia ardhi 'iliyokaa bure' kuzalisha biofuel wakati kwanza tuna uwezo wa kujizalishia gesi asilia ya kututosha na pili kila unapolima mazao unaondoa virutubisho kwenye ardhi kwa hiyo itakapofika kipindi tunahitaji ardhi hiyo kwa ajili ya kilimo cha mahindi na maharage ya pure, ardhi itakuwa haina kitu.
mnahamisha wananchi kabla hata hamjawalipa haki zao, mnawafanya kuwa watumwa kwenye nchi yao kwa maslahi yenu binafsi na mitoto yenu mizembe, ipo cku cha moto mtakiona.
ReplyDeleteHilo zao linaalibu mazingira kupita maelezo ndo maana wanalileta Africa na huku kny rutuba watumalize kabisa maana ukilima hilo hakuna kitakachoota mahali hapo zaidi ya hilo zao
ReplyDeleteMlipoambiwa KILIMO KWANZA ikawa nderemo na shangwe. Wengine tulisema ni ngonjera zile zile tulizozizoea. Sasa mnaonyeshwa mfano hai wa KILIMO KWANZA mnaanza kulalama! jamani Wabongo m wagumu!!
ReplyDeleteAMA KWELI BORA UNYIMWE MALI UPATE AKILI KULIKO KUWA NA MALI UKOSE AKILI,JAMANI HATUWEZI KUSOMA HATA LUGHA YA PICHA MBELE YETU HATUIELEWI?HAPO NYINYI MNAVYODHANI MWENYE SHAMBA NANI?HUYO MAMA AU MZUNGU AU MAMA KATUMWA AJE KUKAGUA??
ReplyDeleteAMA KWELI KIKULACHO KI NGUONI MWAKO,MBWA MWITU KWENYE NGOZI YA KONDOO.HILI NI ZIMWI LITUJUALO LITATULA BILA YA KUTUMALIZA WALAHII
Waacheni waje tu bwana tuache kulalamika sababu UPUMBAVU NA UJINGA ni wetu wenyewe. Watanzania kutwa starehe mala leo Miss Tanzania oo twangapepeta sijui pekechapekecha wako wapi leo, uzinzi na ufirauni uko juu si kwa wananchi wala viongozi na usanii wa kipumbavu kutwa kuelezana matatizo tuuu na kukosa ustaharabu. Blaablaa zimekithiri watu hawatilii mkazo umuhimu wa kilimo na ufugaji acheni basi WAKOLONI warudi kimtindo tunalalamika nini sasa. JAMANI MI MWENZENU NNA HASIRA NA UCHUNGU SANA NA NCHI YANGU BASI TU YAANI.
ReplyDeleteMIMI NILKUWA SIAMINI KAA NCHI INAUZWA KWA KASI YA NAMNA HII,WAKEZAJI WAZAWA WAKITJWA UTAKUTA NI VIONGOZI WA NCHI AMA JAMAA ZAO BILA KUSAHAU WANATENGENEZA MZINGIRA YA UMWAGAJI DAMU KWA KIZAZI CHETU KIJACHO,WATAKAPO DAI ARDHI NAWAZUNGU AWATA KUBALI,ITABIDI VITA NYINGINE YA UKOMBOZI,UWEKEZAJI NI UKOLONI MAMBOLEO,TUWAMBIE WATOTO WETU UKWELI AFRICA FOR AFRICANS,CHINA FOR CHINES,EUROPE FOR EUROPIAN ALUTA CONTINUA.
ReplyDeleteyani ni hivihivi tunakaribisha ukoloni,ivi ulaya ni wapi we mwafrika utamilikishwa ardhi namna hii,dah inaskitisha sana
ReplyDeleteKwakweli nimeshindwa kuvumilia jamani hizo ekari 1000 za mibono kiwanda cha kutengeneza hayo mafuta kiko wapi? au ndiyo tunaendelea na historia ya watengeneza malighafi?
ReplyDeleteBaada ya kuvuna mibono, ardhi haitafaa kwa kupanda chochote.
Mpaka tutakapoweza kuthamanisha uoto wa asili na miti yetu ya asili ndio tutaacha kugawa ardhi kwa waekezaji pasipo kutathmini thamani yake.
Heri kuwa na akili na mali kuliko kuwa na mali bila akili
"Tanzania ina maeneo mengi yasiyofaa kwa kilimo, hivyo kuishia kukaa bure, hali inayopelekea kilimo cha zao hili la mibono, kuonekana kama mkombozi wa matumizi sahihi ya ardhi iliyokuwa inakaa bure, na wakati huo huo kutoa ajira kwa maelfu ya waTanzania" Hii sentensi nani kaifanyia utafiti? ardhi inayokaa bure ni ipi? Maelfu ya wapata ajira au cheap labour? Kama hamna mipango endelevu ya hiyo ardhi si muiache wazi inyonye gesijoto tupunguze kasi ya global warming? Yaani mi wananikera..... viongozi wanaofanya maamuzi kwa kuangalia maslahi ya wageni na yao!
ReplyDeleteMkuu wa Libeneke,
ReplyDeleteNafurahishwa kuyaona maendeleo ya vijijini kwa bibi na babu zetu,lakini yananipa wasi wasi kama ni maendeleo ya mtazamo wa karibu au wa mbali.
Makuzi yangu yalikuwa kwenda likizo vijijini na kuona kilimo cha msimu cha mahindi,mtama,mboga mboga na matunda ndiyo kilikuwa kilimo cha jadi miaka nenda rudi,hapakuwa na njaa ya chakula zaidi ya kutokuwepo na huduma zote muhimu kama shule za msingi na mazahanati ya matibabu,maisha ya wanavijiji yalikuwa kujituma kwa kilimo cha chakula kwa familia.
Kilimo hichi cha mafuta ya "disel" ni mabadiliko ambayo kimtazamo wa mbali yanaweza kutuletea ukame wa njaa na maisha vijijini,kama haya majaribio ya kilimo cha mafuta hayatoleta matokeo ya kutosheleza mahitaji ya wanavijiji,taifa na soko la ulimwengu.
Kinachotakiwa kwa wanavijiji vilivyotajwa ni mwelekeo mpya wa "micro finance" mikopo midogo midogo kwa wakulima wa vijijini, mafunzo mapya ya uzalishaji wa kilimo cha "organic" chakula kwa wanavijiji,taifa na soko la ulimwengu.
Hainipi wasiwasi kutumika kama majaribio katika mashamba ya bibi na babu zetu ni mojawapo ya maendeleo ya vijijini kupatiwa ajira na mitazamo mipya ya maisha ya uchumi kwa wanavijiji kama wawekezaji na wahusika wa wilaya wanavyosema, kinachonipa wasi wasi ni aina gani za ajira wanazopatiwa kimtazamo wa mbali kilimo cha mafuta hakitowasaidia wanavijiji.
Miaka ya nyuma wanavijiji wilaya zingine walilazimishwa kilimo cha pamba, katani bei za soko la ulimwengu zikashuka,wakulima wa vijijini wakasauliwa,wengi wakaja mijini kutafuta maisha na vibarua.
Kizazi kipya cha sasa kisirudishwe tena katika mipangilio ya miaka iliyopita ya kilimo cha katani,pamba kimtazamo kilimo cha mafuta hakitowaletea tofauti ya maendeleo ya maisha vijijini zaidi ya kuwaletea hali ngumu ya maisha.
Wahusika wa wilaya/Mkoa na Serikalini wanahitajika kuteua kamati maalumu kwa kufanya utafiti wa msimamo wa mbali katika mabadiliko haya ya kilimo cha mafuta badala ya kilimo cha chakula kwa wanavijiji na taifa.
Mickey Jones
Denmark